Keynez
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 3,620
- 6,510
Sijajua mchakato wa kumfanya Nyerere kuwa mtakatifu umefikia wapi ila nakumbuka moja ya kitu ambacho Kanisa Katoliki inafanya na kuchunguza kabla haijamtangaza mtu kuwa Mtakatifu ni uchunguzi wa matendo yake alipokuwa hai pamoja na miujiza iliyotokea wakati wa uhai wake na baada ya kifo.
Wengi tunajua Nyerere pamoja na mapungufu yake alikuwa na nia njema na taifa la Tanzania. Hata wale waliotofautiana naye na waliompinga kwa maamuzi na sera zake sidhani kama watabisha kuhusu hili.
Kutokana na taifa kupitia katika sintofahamu kubwa huku kukiwa na ombwe kubwa la kiuongozi, nia hii njema thabiti ya Nyerere kwa Tanzania aliyokuwa nayo alipokuwa hai inaweza kutumika katika sala ya Novena kwa taifa kupitia kwa "roho" ya Nyerere.
Kama maombi hayo yatajibiwa na miujiza kutokea, ushuhuda wa maombi hayo ndiyo unaweza kutumika kuwafanya wamtangaze Mtakatifu.