Je, nimuache au nimvumilie?

Je, nimuache au nimvumilie?

Nina mke wa ndoa ambae nina watoto nae watatu, umri wangu sasa ni miaka 32 na umri wa mke wangu ni miaka 28. Zamani nilikua na uwezo mkubwa na alinipenda sana, ila tokea pesa zimepungua ndiyo nimeona mapungufu yake, kuna kipindi alitoroka akaniachia watoto, nikapambana kumrudisha maisha yakaendelea ila sasa hivi naona tena dharau na maneno yameanza tena.

Anawadharau wazazi wangu, yeye anasikiliza sana maneno kutoka kwa mama yake, mimi hata niseme nini sisikilizwi, ila mama yake chochote anachomwambia ndiyo anakifuata.

je nini nifanyeje, nimuache aendelee na maisha yake, au nifanyeje ili akae sawa? Na je, vipi kuhusu watoto wetu watatu, mkubwa miaka 5 (Ke), wa kati ana miaka 3 (Me) na wa mwisho ana mwaka mmoja (Me)?
Amepata mwingine anayemheshimu na kumsikiliza, baadhi ya wanawake wako hivyo.
 
Hujasema hatima yake ni nini mkuu ?
Tuiache kwenye mabano mkuu

Mazishi ya mtu hai kishirikina
 
Kuna page fulani nilikuwa nasoma watu wanaomba ushauri kwa sana..sasa niliona mdada fulani anaomba ushauri kwamba tangu mumuwe afukuzwe kazi na hawana pesa basi mapenzi kwake yamepotea na wakifunga ndoa kabisa kama miaka 6 nyuma.. Aisee nimejiuliza sana kwamba ukikosa pesa na status nayo inashuka kama mwanaume kweli? Dunia inaenda wapi ? Ukweni wanataka mtu atakuwa msaada kwao kwa sana ndo wanamthamini
 
mukalishe chini muulize, kuazia leo akusikilize wewe akikataa piga chini hakufai
 
Yeyote atakayefanyiwa hivyo atajengewa nuksi na hakuna atakalofanya likawa, iwe kazi, biashara au mahusiano kutegemeans na manuizi
Akienda kwa mganga si ataona Kama ulimchezea
 
Kuoa mwingine ndio shughuli pevu hakuna mwanamke anayependa kutawaliwa bali anapenda mtu amwambie kitu fulani ili aone kama atafanya au laah alipenda life stlye fulani sasa huna basi .
Vitimbi vimeanza ushauri huu hapa .
1.kaa naye chini mweleze kiuzuri tu ikishindikana mpeleke kwao kaelezee kwao mwambie mama yake ukweli acha kumdanya mtoto hakuna mume atakaye mwoa single mother mwambie aache utoto atulie ni mama sasa wawa toto 3. Na asiridi mpe talaka ya mwaka 1 bila matumizi yeyote mwambie mama yake ampe na umnyime kuona watoto ili aone. Umuhimu mwambie asije kwako tena wala asije ofisini kwako akitaka kitu awaambie ndugu zake na mama yake hadi pale atakapoona maisha ni magumu. Ajifikirishe kudharau wazazi wako ni kujiona mama wanya vua cheo hicho .
2.Mpeleke kwa mchungaji muelezee muombewe mweleze nikioa ningumu kuanza kitu kipya tena.
Elezea ila akiendelea unaweza kuoa tena

3. Vikao vya familia na useme namuacha naoa kipya ila usikae oa tena mmh hapana men haya maisha nu taff
 
Jukumu kubwa kwa Sasa ulilonalo ni Kuwalinda hao watoto wako

Hakikisha unawapenda Sana watoto wako.
Hakikisha unamu ignore kabisa huyo mwanamke na asiwe kabisa kwenye ratiba za maisha yako.

Fanya mpango uwe na mwanamke wa pembeni ambaye ndiye atakuwa mwandani wako.

Hakikisha huongezi tena mtoto mwingine na huyo mama.

Hakikisha huteteleki kwenye kipato.

Hakikisha unafanya Maendeleo yako kimya kimya bila kumuhusisha kabisa.

Huyo tayari ameshakuwa adui yako. Tatizo kubwa tulio nalo sisi wanaume tunachukulia poa Sana mwanamke akishabadilika kwa namna hiyo.

Usichukulie poa kabisa.

Ushauri mzuri.
 
Back
Top Bottom