Je, nimekosea kuomba msamaha?

Daydream

Member
Oct 26, 2023
58
328
Niliwahi kuwa kwenye mahusiano na binti fulani ambae alikuwa nami bega kwa bega.

Kuna muda tulitengana lakini alikuwa ana tabia ya kunitafuta na kunisalimia, hata kama utapita mwezi au miezi miwili lakini lazima tu atanitafuta na kunisalimia na mimi namjibu vizuri kabisa.

Ingawa alikuwa akionesha dalili zote kwamba anahitaji turudishe uhusiano wetu lakini binafsi sikuona tena umuhimu wa kufanya hivyo.

Kuna siku moja alinikera kitu fulani na nikamtolea maneno ambayo kiukweli lazima tu alijiskia vibaya maana mara baada ta kunikera nilimkataza asinitafute katika maisha yote yaliyobaki.

Baada ya kama mwezi nilikaa nikafikiria na nikagundua kwamba kauli niliyomtolea sio nzuri na napaswa kumuomba radhi kwa kauli yangu ile iliyokosa staha, maana sote ni binadamu sasa sio vizuri kumkataza binadamu mwenzako asikutafute katika maisha yake yote.

Je, kwa kufanya hivyo nitakuwa nimekosea kumuomba msamaha au atakua ameniona dhaifu?

ZINGATIA
Kumuomba msamaha sio kwamba nahitaji kurudiana nae kimapenzi hapana mana tayari nina mpenzi, lengo ni kubaki na amani ya moyo.
 
Niliwahi kuwa kwenye mahusiano na binti fulani ambae alikuwa nami bega kwa bega.

Kuna muda tulitengana lakini alikuwa ana tabia ya kunitafuta na kunisalimia, hata kama utapita mwezi au miezi miwili lakini lazima tu atanitafuta na kunisalimia na mimi namjibu vizuri kabisa.

Ingawa alikuwa akionesha dalili zote kwamba anahitaji turudishe uhusiano wetu lakini binafsi sikuona tena umuhimu wa kufanya hivyo.

Kuna siku moja alinikera kitu fulani na nikamtolea maneno ambayo kiukweli lazima tu alijiskia vibaya maana mara baada ta kunikera nilimkataza asinitafute katika maisha yote yaliyobaki.

Baada ya kama mwezi nilikaa nikafikiria na nikagundua kwamba kauli niliyomtolea sio nzuri na napaswa kumuomba radhi kwa kauli yangu ile iliyokosa staha, maana sote ni binadamu sasa sio vizuri kumkataza binadamu mwenzako asikutafute katika maisha yake yote.

Je, kwa kufanya hivyo nitakuwa nimekosea kumuomba msamaha au atakua ameniona dhaifu?
Ukauzu wa Baba yangu Mzazi umenisaidia sana kwenye mapenzi hadi leo hii naendelea kula mema ya nchi katika mapenzi.

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Mwanamke haombwi msamaha, unajivua uwanaume.
Emu fikiria leo hii raisi atoke mbele aombe msamaha kwa wananchi, si lazima mtatia dosari uraisi wake?
Vivyo hivyo kwa wanawake.
Chukua maamuzi songa mbele wapo wengi hawa.
 
Back
Top Bottom