Je, nimekosea kummwaga?

Museven

JF-Expert Member
Aug 22, 2011
629
447
Habari za pilika waungwana? Naombeni busara zenu wajameni! Mpenzi amenitia jeraha la moyo? Mi nilikuwa na demu, tulipendana sana na ukweli nilimuamini sana na nikawa namtimizia kila kilichokuwa ndani ya uwezo wangu. Yeye aliishi na wazazi wake nami nikiwa kwangu nimepanga. Siku moja nilipata safari ya kikazi kwenda mkoa mwingine. Asubuhi moja nikiwa huko kama saa 1:30 nilimpigia cm kumjulia hali. Sikuamini masikio yangu, kwani nilipokelewa na matusi mazito ya nguoni kutoka kwa mwanaume akiniambia ati nikome kumpigia mke wa mtu! Sauti nilíitambua vema sana, ni ya mfanyakazi mwenzangu pale kazini. Kukwepa shari, nikaikata.Siku 4 baadaye demu akanipigia akilaumu ati mbona simpigii! Nilimsimulia matusi yale na nikamwambia simtaki tena aendelee na huyo "mume" wake. Juzi tena kaja kwangu ati anataka tena penzi! Nilipouliza kuhusu mwanaume wake aliyenitukana, hasemi ukweli. Nilimfukuza. Je, wanaJf, nilikosea kuamua hivyo.
 
Demu??. . .mke wa mtu?

Tafuta mwanamke tu uepuke shari na matatizo.
 
Sasa unafeel guilty ya nini? Au umemkataa huku ukiwa unampenda bado? Maana kila mwenye akili timamu angefanya kama ulivyofanya wewe!
 
enzi za magonjwa hizi,mpenzi wako akionyesha tabia za wazi wazi kuwa sio muaminifu,mpige kibuti or else utapelekwa kaburini.......
 
Cha ajabu zaidi, hata kabla hatujamaliza mgogoro wetu, tayari akaanza kuniambia anahitaji sh.10,000. Aliniboa vby!
 
ndo matatzo ya kudate na mademu wachovu haya,sasa demu anagongea hadi sh elfu kumi,si njaa tu zimemjaa!kwanza na wewe una umri gan?
 
Sasa mkuu mke wa mtu ni wa nini?
After all takwimu zinaonyesha kuwa idadi kubwa ya binadamu ni Wanawake.
 
achana nae,njaa zake ndio zimemrudisha kwako.inaonyesha bado unampenda,piga moyo konde tafuta mwingine mkuu.
 
Habari za pilika waungwana? Naombeni busara zenu wajameni! Mpenzi amenitia jeraha la moyo? Mi nilikuwa na demu, tulipendana sana na ukweli nilimuamini sana na nikawa namtimizia kila kilichokuwa ndani ya uwezo wangu. Yeye aliishi na wazazi wake nami nikiwa kwangu nimepanga. Siku moja nilipata safari ya kikazi kwenda mkoa mwingine. Asubuhi moja nikiwa huko kama saa 1:30 nilimpigia cm kumjulia hali. Sikuamini masikio yangu, kwani nilipokelewa na matusi mazito ya nguoni kutoka kwa mwanaume akiniambia ati nikome kumpigia mke wa mtu! Sauti nilíitambua vema sana, ni ya mfanyakazi mwenzangu pale kazini. Kukwepa shari, nikaikata.Siku 4 baadaye demu akanipigia akilaumu ati mbona simpigii! Nilimsimulia matusi yale na nikamwambia simtaki tena aendelee na huyo "mume" wake. Juzi tena kaja kwangu ati anataka tena penzi! Nilipouliza kuhusu mwanaume wake aliyenitukana, hasemi ukweli. Nilimfukuza. Je, wanaJf, nilikosea kuamua hivyo.

tena ungemfukuza kwa mateke na magumi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom