Je, nianzie wapi kufikia lengo langu?

Je, nianzie wapi kufikia lengo langu?

Anza na usajili wa biashara. Hakikisha kampuni au brand yako imesajiliwa kupitia Business Registrations and Licensing Agency (BRELA). Hii ni foundation—bila hapo huwezi kuendelea vizuri na mamlaka nyingine.
Baada ya hapo, nenda TBS. Hawa ndio wanahakikisha bidhaa yako inakidhi viwango (quality & safety). Utatakiwa:
Kupeleka sample ya kinywajiKufanya vipimo (lab tests)Kupata TBS certification mark
Hii ni muhimu sana hasa kwa kinywaji kinachoingia sokoni. ila ukitaka kupita shortcut inawezekana japo ni RISK sana inategema zaidi na mkoa uliopo. kwa dsm unaweza piga hata miezi mwaka ndio ukaja kushtukiwa
 
Anza na: 1. Eneo la kufanyia uzalishaji 2. TIN 3. Brela- Jina la biashara 4. TBS- (usajili wa product)-https://oas.tbs.go.tz/ 5. Tausi -leseni 6. TRA- kodi
 
Hongera kwa kupambana Mkuu 👏👏

Tanzania ni miongoni mwa Nchi zenye Taasisi nyingi sana ambazo kimsingi ni kama zinatumika kurudisha nyuma fursa ya Uwekezaji

Unapotaka kuanzisha biashara ya Vinywaji, ni lazima ufuate masharti yote ya hizo Mamlaka za udhibiti

Ukiwa tayari, kuna mtu naweza kukuunganisha naye akakusaidia pale TBS maana anajua hatua zote muhimu kabla hujapewa kibali cha kusambaza bidhaa yako kwa mlaji
 
Back
Top Bottom