Je, ni wangapi wasiotamani kupata watoto?

mgumba uyo au hana sehemu za uzazi ndio maana anajifariji kwa kauli tata ivyo.. hakuna mwanadnu asiyetamani kuwa na mtoto..
 
Soma Kitabu unachokiamini, kama ni Biblia soma Mwanzo sura ya 2,3.

msome Ayubu, msome mhubiri, soma maombolezo. Ukifa umekufa. Mengine ni kufarijiana.

Shetani alidanganya ukila tunda hamtakufa, alipoona tunakufa sasa anadanganya watu kuna kufufuliwa. Hahahaha!

Mungu hana muda na wanadamu tena Mkuu. Alishamaliza kazi.

Wanadamu wanachohangaika sasa hivi ni kupambana na kukidhibiti kifo. Wajinga wanasubiria kufufuliwa. Hahahaha!

Nikuambie tuu kifo kitadhibitiwa na sisi wenyewe wala hatakuja mtu kutufufua.

Usiponielewa basi Mkuu
Tatizo huna ushahidi unaandika kama unawasimulia watu hadithi za "Ethopo" au "Pamela na kipini" au "Awafu mwenye nguvu" na mfano wa hadithi za kubuni.

Nikikuuliza umejuaje kama watu watakuja kuzuia kifo, hapo hapo nikikuuliza kifo ni nini, utajibu kifo ni kifo tu. Sasa ujasiri wa kuandika mambo msio yajua huwa mnaupata wapi ?

Ajabu ya binadamu hao ambao wanahangaika na kitu ambacho hukumu imepita na wao watakufa, ni ujinga ulioje kuhangaika na jambo ambalo haliwezekani. Imeshaandikwa kila nafsi itaonja umauti.

Wapi shetani amesema kuna kufufuliwa au umejuaje kama Mola ameachana na binadamu ? Najua huna ushahidi wa haya.

Ifikie hatua ukijua huna ushahidi juu ya jambo fulani ni aidha uulize au ukae kimya.
 
Kuzaa au kuzalisha ni jambo ambalo hata kichaa anaweza kulifanya maana ni sex tu inahitajika lakini hiyo haimaanishi ana uwezo wa kuwa mzazi.

Kuzaa ni jambo halichukui mwaka kukamilika ila jukumu la mzazi ni kujenga au kuharibu msingi wa maisha ya mtoto. Ni jukumu la kumsimamia mtu hadi pumzi yako ya mwisho.

Kuzaa na kulea ni zaidi ya kutumia maumbile yako uliyojaaliwa . Its more than that
Jurjani Jokajeusi mumeona point hii
 
Wapi Mungu alisema utaenda Mbinguni?

Mwanadamu aliumbwa Ili aishi duniani. Dunia ndio kwetu, hizo zingine porojo.

Kumbe uoga wa watu wajinga ni kwa sababu ya kwenda mbinguni Dooh! Wewe badala uwe muoga kwa kutofuata maagizo ya Mungu unakuwa muoga wa matokeo. Huna ulichoepuka hapo.
Teh kwa taarifa yako sababu ya watu kufuata maagizo ya Mungu ni kutaka kuenda mbinguni na siyo motoni!
Sasa kama hakuna mbingu mtu afuate maagizo ya Mungu ajili ya nini ilihali anajua akifuata hayo maagizo hatapata zawadi yoyote na asipoyafuata hatapata adhabu yoyote?
 
Hii nimeikuta kwenye mahojiano sehemu kwenye blog moja, mdada mmoja mrembo tu umri 32yrs yeye anadai hataki mtoto kwa vyovyote vile.

Kaenda mbali sana hadi kuwa na watoto sio garantii ya wao kukusadia uzeeni, uzeeni unatakiwa ujiandalie mwenyewe sio kuwatwisha watoto burden.

Cha ajabu kwenye comment section ya hiyo video, wadada wengi nimeona wana-share the same view.

Hii mwaionaje wakuu? Huko tunaelekea ni salama kweli?

Kumbe kuwa na mtoto ni ili aje akusaidie? Asilimia kubwa ya wanaosema hivyo huwa kuna kuna vitu wanepitia ndo vinawa-influence kufanya maamuzi hayo lakini sio kwa akili zao za kawaida, Ni rahisi kuamua kutooa au kuolewa maisha yako yote lakini sio kutokuwa na mtoto, Kwa mtazamo wangu hii sio sahihi, mtoto kuja kukusaidia ni matokeo tu bali unahitaji kujiandalia maisha yako ya baadae mwenyewe
 
Upo sahihi, lakini mada imejikita kwenye kuzaa. Na ndio maana nami najikita humo humo. Haimaanishi sijui kunakulea.
Huwezi kutenganisha kuzaa na kulea maana kitu kinachomfanya mtu mara nyingi asizae ni kutokuona kama anaweza kuweka commitment katika malezi ya mtoto. Kutokujiona kama life lake linahitaji mtu mwingine wa kumtegemea na ndio maana wanaume wengi wanakataa mimba si kwa sababu hawapendi watoto ila wanajua uzito wa jukumu la kuwa baba.

Ingekuwa mtu anazaa afu wengine wanalea hadi mtoto ajitambue na kuanza maisha yake , Hakuna ambaye angeona ni shida hususani wanaume ambao hatuingii labor lakini mbegu zinamwagwa kama kawaida kwa ngono dhembe..

Kama concept hii ndogo inakupa shida pengine unajadili kitu ambacho bado hukielewi
 
Watu wa Africa wanaona ni lazima kuwa na watoto ili watakapo zeeka watoto hao waje kuwasaidia .. Yaani kuna watu wanawaona watoto wao kuwa ni mifuko ya pension kama ilivyo NHIF.. so ukiwaambia kuwa kuna watu hawapendi kuwa na watoto wanaona maajabu kabisa .. Kwa sababu wameshazoea kuwageuza watoto zao chuma ulete
Usisahau kuna makabila wanazaa watoto wengi ili wapate nguvu kazi ya kulima na kuchunga ng'ombe. Wengine ni ufahari na wengine ndio kama hivyo kupata msaada pale unapozeeka ama kupata matatizo yatakayohitaji watu wa karibu sana..

Ukiangalia wengi wanafanya si kwa sababu ya kuijenga furaha yao ama kuhitaji kutoka ndani yao ila ni standards za jamii tu.

Na sasa hivi watu wanajua elimu ni bure bhasi kazi imekuwa rahisi maana unazaa af mtoto akapatiwe facilities muhimu na mtu mwingine
 
Mkuu huyo dada kaolewa kwanza, tuanzie hapo
Kuna wanandoa walikuwa wanahojiwa bbc ni wakenya wakasema wakiwa wachumba walikubaliana kutozaa kabisa uamuzi huu waliwaeleza na wazazi wao japo ilikuwa ngumu kwa ndugu kukubaliana nao lkn ilibidi kwakuwa wao waliamua iwe hivyo.

Wapo kwenye ndoa miaka 20 sasa na wanauwezo mzuri tu kiuchumi.

Halafu kutokuolewa hakumzuii mtu kuzaa mbona kuna watu kibao wamezaa bila ndoa.
 
Nafurahi kuona Watanzania wenzangu mna mawazo chanya kabisa,
Nafurahi kuona Watanzania wenzangu mmechoka kua watumwa wa jamii,
Nafurahi kuona Watanzania wenzangu wachache wa JF mnawafumbua macho wengine waliofungwa na jamii zao,

Kwa mitazamo hii, kutasaidia kupunguza utoaji Mimba(watatumia kinga), Watoto wa Mitaani(kila mtu atalea mtoto wake), na ukatili dhidi ya watoto,

Mwisho kabisa, niwaambie ndugu zangu mnaosema haiwezekani mtu kutokupenda watoto, hakuna kisichowezekana ndio maana kila mtu kapewa akili zake na matamanio yake,
Tuwe wepesi wa kukubaliana na mawazo ya wenzetu walio tofauti na wewe, hii itakufanya uishi maisha yenye amani na furaha sana.

Saba Saba njema kwa wote.
 
Back
Top Bottom