Nakumbuka nilikuwa south Africa,,naishi kule,,nilikaa kama miaka 3 bila kurudi Tanzania,, nilikuwa single kipindi hicho,.sina hata mtoto wa dawa.,
Jamaa yngu fulani mwenye busara sana akanambiya hivi una umri gani? nikamjibu,,akanambiya umri huu tunapaswa kurudi nyumbani,, south tuwe tunakuja kwa business na kurudi nyumbani,, sababu maisha ya kukaa huku mbali na nyumbani tutashindwa kujenga family...tutashindwa kuoa na kupata watoto wema..maana tunatatufa maisha lakini hatutafuti family,,mwisho wa siku pesa tutakosa na family pia tutakosa.turudi nyumbani.
Jamaa nilimuelewa sana,,maana nilivuta picha kuna watu wapo ulaya lakini no kids nothing hadi sasa,,na maisha pia hawana..jamaa akanambiya unaweza ukakosa maisha Leo,,lakini ukafanikiwa kujenga family,,means utakuwa na watoto,,huenda mwanao akakuokoa,,akanambiya ni wazazi wangapi Leo wameibuka na kuwa na maisha mazuri sababu ya watoto wao?
akanambiya hata kama utapata watoto huku south still hawana faida na wewe,,,pia maadili yao zero,,,sababu watoto wa huku 90% hawajali baba zao..wao wanaangalia sana mama zao,,,jamaa nilimuelewa sana tu.
Jamaa yngu na mimi tukarudi nyumbani ,,nashukuru Mungu leo ninao watoto lakini bado nasafiri na kurudi nyumbani,,lengo ni kutafuta maisha na kutafuta family at the same time....kuliko kutafuta maisha nikakosa na family pia nikakosa..
Wakuu ...nimeleta story hii ambayo ni true ktk maisha yngu ili kukazia huu uzi,,mtoto ni muhimu sana sana wakuu,,watu wasiofahamika wasikudanganye mtoto hana umuhimu wakati yeye anao kibao nyumbani kwake.. Amini maneno yngu kadiri nguvu zinapokuishia ndy kadiri utakavyokuwa na umuhimu wa mtoto...akili za kuambiwa changanya na zako..nakusihi tafuta maisha na pia usisahau kutafuta na family,, unaweza ukakosa maisha na family ikakuokoa siku za baadae.,,au hata ukapata hayo maisha lakini yana faida gn bila kuwa na watoto?uhitaji wa mtoto ni muhimu sana wakuu..,na anayejinadi mimi sitaki mtoto niwakuigopwa sana sana..