Je Ni wakati sasa kwa utumishi kutumia mfumo wa Aptitude test katika kuwachuja waomba kazi

kizito2009

Senior Member
Jan 6, 2010
172
223
Habari wadau;

Binafsi huwa napenda kufikiri nje ya Box.Gharama na muda wanaotumia Utumishi katika kuwaita watu kwa mitihani kusahihisha n.k.unaweza kusahihishwa kwa kuleta mfumo wa Aptitude test ambayo inafanyika online.Yaani baada ya kuomba nafasi,muombaji atafanya timed tests online kwa ajili ya mchujo.

Hii itaondoa usumbufu wa kuita watu 1000 kwa ajili ya nafasi moja.Na pia itasaidia sana kuwapima watahiniwa mara nyingi ili kupata watumishi wa umma ambao waanendana na kasi ya sasa.

Nawakilisha
 
Itasaidia lakin aptitude test za online zote ziko mitandaoni siku hzi ukiwa na internet nzur na laptop majibu yote unayapata ndan ya muda mfupi.
 
Haina shida,kujua tu yalipo majibu inahitaji mtu uwe resourceful
Yeah ni kwel ila kwa idad ile ya watu wanaoitwa bora tu wawe wanakuja kufanya manual maana access ya hvyo vitu kwa jamii yetu nayo ni changamoto
 
Yeah ni kwel ila kwa idad ile ya watu wanaoitwa bora tu wawe wanakuja kufanya manual maana access ya hvyo vitu kwa jamii yetu nayo ni changamoto
ni fursa ya kufanya watu tujifunze hizi mambo
 
ni fursa ya kufanya watu tujifunze hizi mambo
Inteview yoyote ya kazi mara nyingi huvutia waomba kazi wengi. Siyo Tanzania tu bali ni nchi nyingi. Ila tatizo la nchi yetu ni pale waombaji wanapoitwa karibia wote bila mchujo. Hii ni kosa kubwa kabisa. Huwezi kuita watu 1000 kwenye interview. Kwanza huu ni usanii na wanafanya hivyo ili wapata fursa ya kupenyeza watu wao. Kitu cha kwanza kabisa walitakiwa wapitie maombi yote na wachague waombaji wachache wenye vigezo. Hawa ndiyo wangefanyiwa inteview.
 
Hapa inabd watu wapewe mitaji wajiajir ,maana walioshikilia ofisi wao kuziacha waingie kuzisaka noti mtaana kama wanavyohubir hawawezi,.viongozi na mliojiriwaa msifikir kujiajir ni kazi rahis
 
Usiishie tu kusema "wazo zuri"
hebu tufafanulie sisi ambao hatujalielewa.

Nafasi ya kazi ikitangazwa,

badala ya kuita watu wanaotafuta ajira mamilioni ya watu,

wanaopoteza nauli na wakati kuja kwenye sehemu ya interview.

Mchujo ungeweze kufanyika online,

Wanaotoa ajira,wanaweka tests online na mchujo unafanyika kwa waliopass kwenda stage nyingine

Mkuu anachosema maswali ya interview yawe online na sio physically kwenda ofisini...
 
Back
Top Bottom