Je, ni siri gani yoyote ya Mafanikio unayoijua tofauti na kuroga?

Prakatatumba abaabaabaa

JF-Expert Member
Aug 2, 2022
1,465
4,675
Humu ndani Kuna watu waliofanikiwa Lakini "Wanacode" ambayo wanahisi kwamba ni mbinu mojawapo iliowasaidia wakaanza Kuona Mwanga.

Je, ni siri gani yoyote unayoifahamu ya mafanikio? Au juhudi peke yake na consistency?

Mimi ninaona Siri pekee ya Mafanikio ni kuanza kufanya (Action) au kuanza mapema kabisa kuyatafuta mafanikio, watu wengi tuna plan Nyingi kichwani Lakini tunashindwakufanya hizo plan/idea kuwa halisi.
 
Hangaika na soko kubwa au wateja wakubwa. Kazi za Elfu hamsini, laki mbili na kadhalika zitakupa kula tu ila hamna kutoboa.

Mafanikio makubwa yapo kwenye wateja wakubwa na miradi mikubwa ya serikali, mashirika na makampuni makubwa size za Millioni 10, Millioni 100, Billioni na kadhalika.
 
unamzungumziaje Bakhresa na biashara zake za mikate ya buku buku, juice za jero jero na biscut za mia mia ?
 
Humu ndani Kuna watu waliofanikiwa Lakini "Wanacode" ambayo wanahisi kwamba ni mbinu mojawapo iliowasaidia wakaanza Kuona Mwanga.
Je ni siri gani yoyote unayoifahamu ya mafanikio? Au juhudi peke yake na consistency? Mimi ninaona Siri pekee ya Mafanikio ni kuanza kufanya (Action) au kuanza mapema kabisa kuyatafuta mafanikio, watu wengi tuna plan Nyingi kichwani Lakini tunashindwakufanya hizo plan/idea kuwa halisi.
1.Kuwa king'ang'anizi katika jambo unalolifanya.
2.Wekeza katika elimu katika jambo hilo..
3.kuwa na nidhamu ya fedha
4. Saidia wenye uhitaji

5. Usisahau kumwomba mungu
 
Back
Top Bottom