NIMPENDENANI
JF-Expert Member
- Nov 2, 2014
- 6,114
- 5,398
Aaaah mbona kitu cha kawaida! Tatizo watu wengi huogopa macho ya watu lakini ni jambo la kawaida.
Umeona eeh!!!.
Aaaah mbona kitu cha kawaida! Tatizo watu wengi huogopa macho ya watu lakini ni jambo la kawaida.
na hela nani anatafuta? Huyo atakuwa kala ile dawa inaitwa LIMBWATA.
wewe unaona ni sawa sawa kuwa na mwanaume anayekufulia nguo!!??, utakua ni mwanamke wa ajabu sana kutaka kuwa na mwanaume inferior, imagine mwanaume wako mtaani wanamuita Bushoke sababu ya kukufulia nguo utakua unajisikiaje!!??
Yani hayo ndiyo mahaba yenyewe sasa,yani mie nikimpata na wakunipikia ntampendaje.embu rudi tena ukamuangalie sasa ivi,maana unaweza mkuta njemba anakuna nazi tena huku anatabasamu.hahahahahahaaa!hayo ndiyo mahaba ninyonge.
Ndo inavyotakiwa..mie binafsi nkiwa npo free ntamfulia nguo zake mke wang hata chupi zake
Bandallah you are a real man..unajua kinachosumbua watu wengi humu ni ushamba na lack of exposure...kwa mtu aliyezaliwa na kukulia Tarime kuona hili jambo alijakaa sawa naweza kumuelewa, but kwa mtu wa kawaida namshangaa anaposhangaa....watu wanachukulia as if ukimfulia wife/gf it will reduce your mahnood!!!! mawazo mgando is a name for it.
AFTER ALL KATIKA NYUMBA ZA WATU WANAOJIELEWA HAKUNA KAZI YA KIKE, UKINIAMBIA KWENDA LABOR NITAKUELEWA, LAKINI SIJUI KUPIKA, KUFUA, GARDENING N.K ZOTE WAPENZI WANASHIRIKIANA.
"thus a woman shall leaver her mother and her father and follow her husband and they shall become one flesh" kama unakubali umekuwa mwili mmoja na mkeo, ina maana kutomfulia ni kutojifulia wewe mwenyewe.
this is 2015 boy! acha mawazo na misimamo ya 14th Century, grow up for Chrissake!
Bright Smart;
Nashindwa kuamini kuwa leo karne hii kuna watu wanaoishi kwa kusikiliza maneno ya huko kitaa. Sitegemei yupo mtu wa jinsi hiyo. Tutoke huko sasa. Siogopi kufua nguo ya My Wife hata siku moja. Siogopi kupika ugali nimletee mezani hata siku moja. Tena yeye yupo hapo na mtoto wetu mchanga.
Usipovuka hapo, weye ni wa ajab saana. Mkeo ni mtu ka weye pia. Mnatoka asubuhi, mnaenda kazini, mnachoka wote kwenye foleni, iweje weye mmefika pamoja nyumbani ujilalie hapo, mwenzio ananyonyesha mtoto, weye unaogopa hata kuweka mboga jikoni ati ni kazi ya kike??
Basi hata kula iwepo na chakula cha kike. Tumeoana hakuna bora zaidi
I don't know how to explain to you by the way. Unaweza lakini sio kwa kulazimishwa my be she's doing something else or she's sick just like that.but not by force
swissme
Katika pita pita zangu nkakutana na mwanaume anafua nguo za kike, hata nilipojaribu kusogeza karibu mboni za macho yangu ili kushuhudia kitendo hiki jamaa alichokuwa anakifanya, ndipo macho yetu yalipokutana na kumuona jamaa akijiskia aibu na kuanza kuangalia chini, naam hali hii ilinifanya nijiulize je haya ni mapenzi au adhabu?
suala siyo ku impress jamii, suala la msingi ni vipi unaishi kwenye jamii maana hauishi kwenye vacuum hivyo basi suala la jinsi gani unaishi kwenye jamii halitakuja kuisha milele...
Kwani mwanamke anapofua nguo za mumewe ni lazima?
Katika pita pita zangu nkakutana na mwanaume anafua nguo za kike, hata nilipojaribu kusogeza karibu mboni za macho yangu ili kushuhudia kitendo hiki jamaa alichokuwa anakifanya, ndipo macho yetu yalipokutana na kumuona jamaa akijiskia aibu na kuanza kuangalia chini, naam hali hii ilinifanya nijiulize je haya ni mapenzi au adhabu?
Mtani yule shemeji yangu anakufulia?? Mi namfulia wifiyo mpaka andawea, kwa raha zangu.Kwa mahubiri ya jana ya mzee wa upako nilitegemea mada kama hii JF, hakuna ubaya wowote alimradi anafanya hivyo kwa moyo wa upendo na si kulazimishwa.
Ujue umeingia kwenye kundi la watu ambao napenda sana kuwasoma hapa jamvini. Ahsante sana Mkuu.