Je ni sawa baba kuanua nguo za ndani za binti yake?

Je ni sawa baba kuanua nguo za ndani za binti yake?

Yaani mleta uzi wataka sema mtoto wa kike haruhusiwi kumfulia mshua wake boxer?
 
Huo uchi wake nauona tangu anazaliwa na nguo namnunulia zote sasa cha ajabu ni kipi?. Tuchupi twake?.
 
Baba ni baba tu whatever what!!.....Hilo la kuanua chupi ni dogo sana,mimi nikiwa baba hata kama binti yangu mkubwa(mwenye umri wa kuolewa) anaumwa hadi hawezi kuoga na anapaswa kuogeshwa nitamuogesha pia!
Watch out ,not to that extent
 
Unaanua tu..Na ukiona hajazitakatisha unaweza kumpa somo
 
Kuna siku nguo za mdada mpangaji mwenzangu zilidondoka sasa nikawa nazirudisha kwenye kamba.

Ile namalizia chupi nimeishika kuitundika akafungua geti face to face aliona nimeishika... Aidha alijua nilikuwa nairudisha kwenye kamba au nilikuwa naiangalia alijijua mwenyewe.
ulikuwa unaiangali wewe, kwanini bhukurudisha yakwanza
 
Inategemea jinsi na namna ulivyomlea , anakuchukuliaje? Baba rafiki au baba mkaksi
 
Niaje wakuu

Leo nikiwa kitaa nimekuta watu wakibishana eti kama wewe ndo baba unarudi nyumbani alafu unakuta mvua inanyesha na nyumbani hakuna mtu alafu juu ya kamba kuna nguo za binti yako mkubwa tu zikiwa zimeambata pamoja na nguo za ndani alafu zimekauka je utaanua au utaziacha ziendelee kunyeshewa
Kabla hamjapata hilo jibu jiulize kwanza hadi baba anafikia umri wa kuwa na hao mabinti wa umri huo kaona hizo chupi ngapi na sehemu ngapi nyeti? Hajaogesha au kubadili nepi hao bintize utotoni? Sasa hizo nguo zao muda huu zina maajabu au laana ipi hadi zimzuie baba kuzishika?
 
Chupi ni nguo kama nguo nyinginezo sasa mtoto wangu mwenyewe nitashindwaje kumuanulia chupi wakati huko nyuma nilikua nikimvisha na kumvua pindi amejikojolea
 
Niaje wakuu

Leo nikiwa kitaa nimekuta watu wakibishana eti kama wewe ndo baba unarudi nyumbani alafu unakuta mvua inanyesha na nyumbani hakuna mtu alafu juu ya kamba kuna nguo za binti yako mkubwa tu zikiwa zimeambata pamoja na nguo za ndani alafu zimekauka je utaanua au utaziacha ziendelee kunyeshewa
Mkuu nikusaidietu mzaz ni mzazi tuu mie nina binti ambaye ni kila kitu kwangu chochote anapata hata pedi na nunua ukiwa mzazi tena hayo ni madogo
 
Niaje wakuu

Leo nikiwa kitaa nimekuta watu wakibishana eti kama wewe ndo baba unarudi nyumbani alafu unakuta mvua inanyesha na nyumbani hakuna mtu alafu juu ya kamba kuna nguo za binti yako mkubwa tu zikiwa zimeambata pamoja na nguo za ndani alafu zimekauka je utaanua au utaziacha ziendelee kunyeshewa
Hujawahi kuuguza mwanamke?
 
Back
Top Bottom