Je, ni sahihi kuchangisha watu michango kwa ajili ya kutoa msaada?

DALALI MKUU

JF-Expert Member
May 7, 2022
1,486
2,739
Nimekuwa nikiona mara Nyingi watu huandaa matukio ya kuchangia watoto wanaoishi katika mazingira magumu,yatima,Wafungwa ma wagonjwa kisha kushirikisha ndugu au watu wengine kuchangia.

Yaani unajikuta tu upo kwenye Kundi la Whatsap na kisha unaombwa kutoa ahadi yako kwa ajili ya tukio Husika.

Ni jambo jema Kuchangia na kuwasaidia watu katika amkundi hayo yaliyotajwa, Lakini Je ni sahihi kuomba mchango wa kwenda kusaidia hao watu?

Mim kwa upande wangu sio sahihi nafikiri jambo Jema ni kuchukua kila chako ulicho nacho na familia yako itakuwa jambo jema Zaidi.

Kuliko Kushirikisha watu wengine wakati hayo ni maono yako na sadaka yako Binafsi, Mimi wakati mwingine nafikiri kuna aina Fulani ya upigaji wa hayo matukio.

Siku hizi kuna hadi harambee zinaandaliwa kwa ajili ya kuchangia wagonjwa mfano wenye matatizo ya Kansa. Wenye matatizo ya Usikivu, watoto wenye matatizo ya Moyo N.K linaandaliwa tukio kIsha munaalikwa na kutakiwa kutoa ahadi zenu kubwa kubwa ama Fedha taslimu na wakati mwingine mgeni Rasmi anakuwa ni Kiongozi wa Serikali.

Napenda kuchangia ila kwa Kusukumwa ndani yangu binafsi ila sio kulazimishwa, hadi nafikiri kuna kaharufu ka upigaji.
 
Napenda kuchangia ila kwa Kusukumwa ndani yangu binafsi ila sio kulazimishwa, hadi nafikiri kuna kaharufu ka upigaji.
Kwan nao wakija kuomba support, huwa wanakulazimisha?

I mean huwa wanasema kila aliyepo kwenye ilo group ni lazima atoe chochote?
 
Kwan nao wakija kuomba support, huwa wanakulazimisha?

I mean huwa wanasema kila aliyepo kwenye ilo group ni lazima atoe chochote?
Kuna aina nyingi za kulazmisha mtu kuna direct na indirect. Je kama mm utaratibu wangu ni tofauti na wa kwake je? kitendo cha kukuweka kwenye group tu tayari amekulazimisha na ukijaribu kujitoa ndio utajua ulilazimishwa ama uliombwa
 
Nishakutana sana na situations kama hizo. Huwa wanaweka ilo tangazo, na kuomba utayari wa members.

Binafsi sikumbuki kama kuna tangazo ambalo nilishawahi kuchangia, na sijawahi kufatwa inbox au kuulizwa chochote.

Sasa hapo indirect pushing force inatoka wapi?
 
Basi inategema na aina ya marafiki zako sio wasumbufu mm nilishawahi kusumbuliwa sana na mtu ikabidi nimchane
 
Basi inategema na aina ya marafiki zako sio wasumbufu mm nilishawahi kusumbuliwa sana na mtu ikabidi nimchane
Labda, lakini pengine huwa unajishtukia au kuona aibu. So yakiwekwa matangazo ya hivyo, lazima uchangie mada zao na kuweka maoni
 
Back
Top Bottom