Je, ni kweli wanawake hawapendani?

Je, ni kweli wanawake hawapendani?

Basi tuseme wanawake hatupendani na wanaume hamtupendi. Au wanaume wote wanampenda mama ???
Huo ni mfano mdogo sana, nikiwa chuo niliwahi ishi nyumba moja na mabinti wawili, waliishi pamoja from 1st year mpaka wakamaliza, na ndio wadada pekee waliowahi ishi pamoja mda mrefu. Waliwahi kukiri kuwa wanawake wengi hawapendani ndio maana hata kuishi pamoja wengi hawawezi.

Bado kuna wale wa kujirahisisha kwa mwanaume alale nae kwa sababu tu hampendi mkewe 😐

Huko ukweni wanaoongoza vita ni wanawake, mke na mama mkwe hawapendani tena hii ipo sana wengine hadi kufikia hatua ya kutamani kusitisha uhai wa mwingine.

Maofisini mtanisaidia.
 
Tangu ninakua nimekuwa nikisikia kauli za wanawake hawapendani, adui wa mwanamke ni mwanamke mwenzie, je, ni kweli wanawake hawapendani au ni nadharia tu ilitengenezwa kuwagawa wanawake wasiaminiane kuwa hakuna anayempenda mwingine?

Nauliza hivi kwa kuwa msemo huo umekuwa ukisikika zaidi kusemwa na sisi wanaume japo wapo na wanawake wamekuwa wakisema ila huwa inatokea pale wanapokwazana kitu ambacho napata mashaka kwa kuwa kukwazana hutokea pande zote, kwa nini ihusishwe na wao kutokupendana?

Je, kisaikolojia ni kweli hawapendani? Jamiicheck naombeni mtusaidie katika hili, ukweli ni upi?
Naskiaga eti hawapendani. Kwani wanawake wenyewe wanasemaje
 
Wanawake wanapendana usije danganyika kuwa hawapendani jua mtu anayekupenda lzm awe na wivu na wewe

Kinachowafanya wanawake waonekane hawapendani ni wivu tu, kuta wanawake wanagombana waacheni msiwafanye chochote muwapuuzie harafu muone mwisho wao

Tena utashangaa kesho ni marafiki ila wakiachana kila mmoja anamsema mwenziye isivyo vzr

Narudia wanawake wanapendana
 
Huo ni mfano mdogo sana, nikiwa chuo niliwahi ishi nyumba moja na mabinti wawili, waliishi pamoja from 1st year mpaka wakamaliza, na ndio wadada pekee waliowahi ishi pamoja mda mrefu. Waliwahi kukiri kuwa wanawake wengi hawapendani ndio maana hata kuishi pamoja wengi hawawezi.

Bado kuna wale wa kujirahisisha kwa mwanaume alale nae kwa sababu tu hampendi mkewe 😐

Huko ukweni wanaoongoza vita ni wanawake, mke na mama mkwe hawapendani tena hii ipo sana wengine hadi kufikia hatua ya kutamani kusitisha uhai wa mwingine.

Maofisini mtanisaidia.
hawakuwa mume na mke hao?
 
Mimi nafikiri dhana hii ililetwa na wanaume pamoja na mfumo dume katika kumdumaza mwanamke katika jamii, ili kuwafanya wanawake wawe katika ushindani na kuondoa ushindani kwa wanaume.
Pia kuondoa dhana ya ubaguzi wa kijinsia wa wanaume dhidi ya wanawake na ionekane kwamba wanawake ni wapinzani badala ya washirika katika jamii.

Hivyo wakafanikiwa kusambaza hii dhana potofu ambapo maranyingi, taarifa na dhana za uwongo zinaweza kuenea katika jamii na kusababisha imani potofu kujengeka na kuwa sehemu ya maisha ya wanajamii.
 
Kuvunjika kwa urafiki na kusutana
Lame.........Worse than kuuana, kufanyiana ujambazi, kusnichiana? Maana wanaume mnafanyiana haya sana, hii inawafanya muonekane, mnapendana? Kama na nyie hampendani mbona hakuna kampeni ya misemo ya "wanaume hampendani" ? Why? Think and for reference soma comment ya Atoto na wengineo.

Ukitaka kuwatawala vizuri, wagawe......
 
Sisi hatununiani, ukizichapa ukadundwa mnaenda kukaa meza moja bado
 
Siku 1 nimeingia restaurant nipo na mama yangu mdogo (Mungu amrehemu) sasa baada ya kufika pale tukakaa baada ya dakika kama 1 hivi akaja waitress akatupa Menu pale tukaagiza. Vitu vikaenda kutengenezwa after kama 15 minutes mzigo ukaletwa mezani lakini chaajabu mama alisema ile restaurant wahudumu wanajisikia sana na kiukweli hakuwa comfortable kabisa. Mimi binafsi sikuona makosa ya yule dada (labda yeye kwa jicho la tatu la kike aliona kitu au labda yule waitress nae alifanya kitu kwa jicho la 3 la kike ili nisione mi sijui) nikapata wakati mgumu sana kumuuliza mama kosa la huyu muhudumu ni lipi? Tulimaliza pale tukaondoka akiwa amechukia tu na kujuta kuingia pale. Hao ndio wanawake

NB.
Visa vya aina hii vimeshanitokea sehemu mbalimbali na hii imenifanya kuwaelewa wanawake ni watu wa ku mind mambo madogo madogo ( ila kwa upande wao ni makubwa)
 
Ngoja waje kukupa muongozo...

download-1.jpg
download.jpg

Cc: Mahondaw
 
Mimi nafikiri dhana hii ililetwa na wanaume pamoja na mfumo dume katika kumdumaza mwanamke katika jamii, ili kuwafanya wanawake wawe katika ushindani na kuondoa ushindani kwa wanaume.
Pia kuondoa dhana ya ubaguzi wa kijinsia wa wanaume dhidi ya wanawake na ionekane kwamba wanawake ni wapinzani badala ya washirika katika jamii.

Hivyo wakafanikiwa kusambaza hii dhana potofu ambapo maranyingi, taarifa na dhana za uwongo zinaweza kuenea katika jamii na kusababisha imani potofu kujengeka na kuwa sehemu ya maisha ya wanajamii.
Hivi kwanini haya madini msiyaanzishie nyuzi mnakuja kuyaficha huku kwenye comments ambako wanaosoma ni wachache
 
Sio kweli.

Kwanini?

Ukitaka kuamini angalia watu waliohamia makazi mapya itakuchukua muda mrefu sana wewe mwanaume kuwajua majirani na kujichanganya nao lakini muda uouo wanawake unakuta wana adi kisakosi au kikoba chao kina mwenyekti katibu kijumbe na wanachama akinamama wenzao kibao.

Chukua hiyo!
 
Mimi kwenye makuzi yangu nimeshuhudia marafiki/majirani wa kike wengi wakiishia kuwa maadui kuliko marafiki/majirani wa kiume
 
Back
Top Bottom