Je, ni kweli wanaume hawataki mke 'golikipa' na mwenye kipato kikubwa?

Ncha Kali

JF-Expert Member
Sep 19, 2019
14,501
27,000
Leo nimeulizwa hili na huyu mtoto wangu mkubwa.

Eti, wanaume wa leo hawataki mke ambaye ni mama wa nyumbani (asiye na shughuli ya kipato).

Wakati huo huo, wengi wao hawataki mke mwenye kipato kikubwa au 'mishe' kubwa/nyingi kuwazidi. Ni kama haieleweki wanataka yupi.
  • Je, huu mtazamo ni kweli?
  • Sababu ni nini, uoga?
Nini mtazamo wa wanaume juu ya kipato cha mke?

Tujadili.
 
Duuh aisee yamekukuta yapi mkuu, hizi hasira zote kwa wanaume tuu.
Sina hasira ni ujinga wanaume kila siku kulalamika Mara kile mara hivi haipendezi wakati nikikua tuliaminishwa nyie vichwa Sasa nukiona huu utopo I ask myself hawa viumbe wamevamiwa au tuliaminishwa virce versa
 
Sina hasira ni ujinga wanaume kila siku kulalamika Mara kile mara hivi haipendezi wakati nikikua tuliaminishwa nyie vichwa Sasa nukiona huu utopo I ask myself hawa viumbe wamevamiwa au tuliaminishwa virce versa
Hakuna jinsia isiyo lalamika mkuu, na mtoa uzi kajumuisha wanaume wote ilhali wapo wanawake wenye vipato na wameolewa na hao wachakarikaji kibao wameolewa ni vile tu kua na mitazamo tofauti kuhusu hio ishu sio kwa mwanaume hata mwanamke mwenye kipato kuishi na mwanaume asie na kipato ni ngumu hiyo.

Tumejionea kwa mwanaharakati wenu Joyce Kiria alivyomuumbua mumewe alipoyumba kiuchumi, sasa utaoa mtu wa ivo kweli eti kisa tu wakuone ni kidume.
 
Wanaume tumeumbwa kutawala, heshima ikiwa mashakani tu umekwisha.

Kwa golikipa imekuwa mzigo kwa maisha ya kisasa, eti upambane peke yako halafu ije siku sheria inasema pasu kwa pasu!
 
Golikipa kwa maisha ya sasa ni ngumu inatakiwa awe anajishughurisha hii inakuwa kama backup pindi mwanaume mambo yakigoma uwezo wa familia kusurvive uwepo.
Swala na kuogopa wanawake wenye vipato vikubwa sio kwel japo kuna ukwel kidogo ndan yake. Kila mwanaume anapenda kuwa na mama bora kwa watoto wake, mke bora(mwenye heshima na utii)pasipo kuangalia uwezo wa kiuchumi alionao, sasa wanawake weng wanapofanikiwa kiuchumi kuwazid waume zao ujisahau na kujipandisha kutaka kuwa kama baba ndan ya nyumba
 
Back
Top Bottom