Jamani tuelewe kuwa kila tasnia hutawaliwa na kanuni zilezile tu mfano, elimu, biashara, sanaa na muziki, kilimo na ufugaji, ujuzi, michezo n.k.
Chukulia mfano msanii wetu mkubwa Diamond platinums, amefanikiwa lakini kuna utaratibu uliomfanya mpaka afike aliko. Siyo bahati nasibu, ni mipango yake aliipanga vyema akianza na lengo, juhudi zake, kukabiliana na changamoto, kutokata tamaa na mwisho ni Akiba. Mbinu au kanuni hizi hizi zinaweza kutumiwa na mkulima aliyeko shambani, kwa maana atajiwekea lengo, juhudi, kukabiliana na changamoto, na uwekaji akiba.
Pia mfanyabiashara atatumia zilezile.. Ndio maana zinastshili kuitwa kanuni za maisha maana zinatawala mafanikio kwa ujumla wake.