Saguda47
JF-Expert Member
- May 1, 2016
- 11,136
- 19,872
Ni desturi ya watu wengi sasa wamekuwa wakiamini kuwa maisha hayana formula, desturi hii imejijenga katika fikra za waliowengi na kuondoa dhana ya kujiuliza maswali kuhusu maisha miongoni mwa wahusika.
Je, formula ni nini? Kwa lugha yetu tukufu, formula ni utaratibu uliokatika mpangilio maalumu wenye kusudio la kufikia hitimisho/jibu fulani.
Je, ni kweli maisha hayana utaratibu/formula?, jibu ni kuwa si kweli kuwa maisha hayana formula, maisha ili yawe mazuri au kufanikiwa lazima hatua fulani zifuatwe na mhusika, hatua hizi huakisi lengo na mbinu za mhusika katika kufanikisha kusudio hilo.
Yafuatayo huthibitisha uwepo wa kanuni/formula/utaratibu maalumu katika maisha ya mwanadam:-
1. Lengo, hapa ni wazi kila binadamu ana lengo mahususi maishani mwake, hivyo lengo ni hatu/kanuni ya kwanza katika maisha.
2. Mbinu, hili liko wazi kwani kila mtu hupendekeza mbinu maalumu ili kufikia malengo aliyojiwekea.
3. Bidii/juhudi, huu ni utaratibu/kanuni ya tatu katika maisha, baada ya kubainisha mbinu zinazofaa katika maisha bidii ndiyo msukumo mkuu unaoweza kuharakisha au kuchelewesha kufikiwa kwa malengo ya mhusika maishani mwake.
4. Ujasiri/kutokata tamaa, hii ni kanuni mhimu ambayo imekuwa ikiimbwa katika kila eneo la maisha, hapa ni namna ambavyo mhusika atakuwa na ari juu ya malengo yake, kutokata tamaa humpa ujasiri mhusika wa kuendeleza bidii zake ili kufikia malengo yake.
5. Akiba, hii ni kanuni halisi ambayo huimarisha na kuakisi juhudi au bidii za mhusika katika maisha yake, akiba hutoa taswira ya utoshelevu kwa mhusika hivyo tathmini nzima juu ya mafanikio yake hupimwa kwa kuangalia akiba (wingi na thamani). Mfano utaskia bill gates ana utajiri wa dollar milioni kadhaa.
Je, ni kweli maisha hayana kanuni/formula?
(Saguda47)