Msweet
JF-Expert Member
- Mar 26, 2014
- 3,241
- 4,441
pamoja na ya yote yaharibikayo nitarudi na masters zangu mbili....
Hongera Sana sana dear. That's good news Indeed
pamoja na ya yote yaharibikayo nitarudi na masters zangu mbili....
Asante lov. Afadhali mimi nilikuwa japo na udhamini so hizo kazi nilifanya niongeze kipato. Kuna ambao hawana udhamini hata wa dawa so bila hizo kazi hawawezi kujikimu (walipe kodi, wale, walipie semester fees, Walipie usafiri n.k). Aftenposten sio kabisaHongera Sana sana dear. That's good news Indeed
Kwahiyo mkuu unamwongeleaje mtu kama huyu; mmemaliza naye form 4 akaingia kwenye majeshi either JWTZ, Police etc, wewe ukafaulu ukaenda advance huku ukipongezwa baadae unafka chuo kikuu unasomea ualimu na kuwa mwalimu. Yule aliyefeli mtihani kidato cha nne ana mshaara mzuri na maisha mazur kuzidi mwlm mwenye degree. Kama maisha yana formula nani alistahili kuwa na maisha mazuri kati ya hao niliowasema?Umenena vema mkuu, dhana hii huwa naiona ni upotoshaji mkubwa mno usio na sababu ya kuendekezwa, kudai kuwa maisha Hayana formula ni mawazo hafifu ambayo yamejikita kuamini katika bahati nasibu maisha ilihali maisha ni taswira iliyowazi na ili iboreshwe mbinu na utaratibu maalum lazima ufuatwe ili kutimiza adhima kusudiwa.
Duuh ndugu yangu umenikumbusha mbali mno nakumbuka miaka ya themanini,niliifanya hiyo kazi Sweden nusura nikiue kibb cha kizungu,ile naweka gazei mlangoni kwake alfajiri na chenyewe kinafungua mlango, tukakutana uso kwa uso,na vile nilivyo mweusi kibibi kikajua ni gorilla, kikaanguka na kuzimia.
kwahyo ulaya magazeti watu wanapewa bure?![]()
![]()
kwahyo ulaya magazeti watu wanapewa bure?
Asante sana JessicaJapo hujaniuliza mimi ila naomba nikujibu. Yapo magazeti ya bure na yapo yakulipia. Siku hizi magazeti ya bure mengi yashafutwa kwa kuwa wengi walikuwa hwayasomi. Wanaopelekewa home ni wateja wanakuwa na monthly subscription ya magazeti (wanafanya malipo na wanakuwa na mkataba na kampuni ya magazeti) hivyo wanapelekewa hadi Nyumbani kwao. Asilimia kubwa ya wateja kwa nchi niliyokuwa nafanyia ni wazee.
Unakesha njecgizani kwenye baridi ukifanya nini? Umenikumbusha kazi ya kugawa magazeti majumbani saa saba usiku hadi saa 12 alfajiri (aftenposten) niliyoifanya miaka ya 2012/13 nchi flani ulaya. Unapanda ngazi hadi ghorofa ya 8 kwa miguu kwa masaa 2.30, unasukuma torolikipindi cha winter unateleza kwenye barafu, mvua , baridi vyote vyako.
Toroli limejaa magazeti kazi ya kusukuma sasa uwe umeshiba kweli....
Acha upotoshaji wa kijinga, wewe ni conspiracy theorist usiyetumia akili yako kung'amua mambo,kila saa unawaza ushetani na mambo ya kufikirika, jaribu kujishughulisha kuliko kushinda JF kutwa nzima na usiku kucha! Rudi kwenye thd zako za kichawi unazo ongopea watu ili wakuamini wewe ni mganga fulani kumbe mweupe tu huna lolote zaidi ya kuwa brainwash wenye uelewa mdogo,Punguani wewe!!Mpotezee aliita reply zetu zisizo na maana matokeo yake ule upuuzi wake wote umefutwa pamoja na reply nyingi sana zilizokuwa zimejaa ujinga huku nyingine zilirekebishwa lugha
Angekuwa kaandika vitu vya maana kama anavyojinasibu naamini visingefutwa... hapa ndio unapata kwa usahihi ile tafsiri ya usemi usemao DON'T ARGUE WITH A FOOL...
Jeshi gani linaajiri waliofeli? Division four nzuri sio kufeli ni ufauluKwahiyo mkuu unamwongeleaje mtu kama huyu; mmemaliza naye form 4 akaingia kwenye majeshi either JWTZ, Police etc, wewe ukafaulu ukaenda advance huku ukipongezwa baadae unafka chuo kikuu unasomea ualimu na kuwa mwalimu. Yule aliyefeli mtihani kidato cha nne ana mshaara mzuri na maisha mazur kuzidi mwlm mwenye degree. Kama maisha yana formula nani alistahili kuwa na maisha mazuri kati ya hao niliowasema?
Wewe endelea tu kuishi na maisha ya kusikia,tega Sikio tu endelea kusikia tu maisha yako yote.Nasikia wewe ni Gentamycine.. Kwanini unakua na account nyingi Jf?
Usikariri maisha. mimi niliifanyia Denmark.Ha ha ha hiyo nchi ni Norway Ulaya kazi tunazozikataa tz huko ndio tunazifanya
Sawa tuseme ni ufahulu hafifu, sasa unaonaje hapo nani alistahili kuwa na maisha mazuri?Jeshi gani linaajiri waliofeli? Division four nzuri sio kufeli ni ufaulu
Facts...!!!!Usikariri maisha. mimi niliifanyia Denmark.
Lingine ni kwamba hayo masaa 2 niliyogawa hilo gazeti kwa siku 6 (masaa 12 kwa week) niliweza kukunja milioni zaidi ya 5 kwa mwezi ( 48.hours) jumlisha na scholarship yangu ....majibu unayo. Hizo kazi ulaya zinalipa. Tanzania ya wapi kazi ya siku mbili (48 hours) ikupe milion japo 5???? Hapo bado hujaweka kazi za usafi wakati wa mchana... sema vigezo vya kwenda hUko huna na hata ukiomba hutapata visa japo ya mwAnafunzi. So unapojichekesha chekesha utambue hilo. The hustle is worthy
Katika ulimwengu huu uliojaa mahangaiko na machungu watu tunazaliwa tukiwa hatuna ufahamu wowote wala kuelewa mambo ya mbele zaidi ya kutabili namna mambo yatakavyokuwa.....ndio maana kwenye masuala ya kutafuta ridhki haishangazi kumuona mtu aliyetumia miaka mingi kusomea masuala ya sheria anakuja kuwa mfanyabiashara maarufu......
Kwa kifupi ni kuwa maisha ni vita vinavyohitaji jitihada na maarifa ili kuweza kuvishinda na hatimaye kuyaona mafanikio.....lakini jitihada zetu na maarifa yetu havitafaa kitu bila ya kumtegemea muumba na kumtumainia yeye kwani yeye ndiye mtoaji na RIDHKI na humpa amtakaye kwa muda anaoona unafaa......wapo watu waliokuwa mafukara lakini neema zimewaangukia sasa hivi wanaogelea katika fedha.....ili hali kuna watu kibao nyuma ya pazia bado wanapambana na muda unazidi kwenda.......
Watu wenye vipaji kama alichonacho Diamond ni wengi sana mitaani na kila uchao wanajitahidi kwa kadri ya uwezo wao ili kufikia alipofikia huyo msanii lakini jitihada zinashindikana.....
Wapo watu walianza biashara pamoja na watu fulani lakini leo hii wenzao wakipiga hatua huku wao bado wakiendelea kusua sua kwenye biashara hiyo hiyo....
Kitu kimoja kikubwa kinachokosewa na vijana au tuseme kuwa wachakarikaji wa miaka hii ni kutafuta maisha au ridhiki kwa nia au kujiringanisha na fulani au nimpite fulani.....hiyo ni mbaya kwani kamwe hutakuja kuyaona wala kuyafurahia mafanikio yako kwani maisha hayataki haraka wala pupa...bali yanataka uvumilivu na busara za hali ya juu......huwezi kujua kuwa huyo unayetaka kuwa kama yeye imemchukua miaka mingapi hadi kufikia hapo alipo sasa na je upo tayari kupita njia hizo ili nawe ufike hapo.....!!!???
Stori na sifa huvuma baada ya mafanikio kuja lakini nyuma ya hayo mafanikio kumejaa vita kubwa sana hadi kufikia hapo....??
Usitafute maisha kwa kushindana na fulani bali jiwekee malengo yako na mikakati yako na upambane kwa uwezo wako wote ili kufanikisha mipango yako huku ukiwa na ndoto zenye kutekelezeka.......pia tujifunze kushukuru hata kile kidogo tulichojaaliwa.......
Maisha yana formula tena iko very clear. . .haya mengine ni maneno ya wakosoaji kujikataa na kukata tamaa
Wanatumia mifano michache ya watu waliofanikiwa kisha wakaanguka au ambao hawa kwenda shule lakini leo ni matajiri! Lakini jiulize wako wangapi?
Kama ingekuwa maisha hayana formula basi
Tusingeenda shule kusoma na kupata ujuzi na maarifa mbalimbali
Au tusingedamka na kuwahi kazini au kukesha nje gizani kwenye baridi na hatari zote za usiku kama mimi![]()
![]()
![]()
Badala yake tungejifungia majumbani mwetu na kusubiri kupata kwa njia ya muujiza
Hiyo kufanya kazi kwa bidii ndio formula pekeeMaisha hayana fomula..muhimu ni kufanya kazi kwa bidii na kujiwekea malengo..pia tusisahau kumtanguliza Mungu kwa kila jambo..
Ni kweli kabisa hakuna kitu ambacho hakina formula duniani...! Hata uchawi unaochukukuliwa ni kitu cha kufikirika una formula zakeKiongozi turahisishe, mtazame mtoto toka anaziliwa hadi anazeeka, utajua kuna fomula. Na pia akili haina mipaka, naweza nikafeli alama za mwisho darasani lakini ninazo akili za kufanya kingine. Kwahiyo kila mtu anazo akili labda awe mgonjwa. Mwangalie Samata, akili darasani hamna lakini akili uwanjani zipo, anamefanikiwa na mpira na amefata fomula ndo amefika pale, huwezi kufanikiwa kiholela holela tuuu, hutafika kilele cha hayo tuyoyaita mafanikio.