Je, ni halali kwa kisimbusi cha Azam kuiondoa TBC kwenye free local channels?

PAZIA 3

JF-Expert Member
Jan 30, 2018
1,074
1,857
Rejea kichwa Cha taarifa, Azam kisimbusi wameitoa tbc 1 kwenye orodha ya free local channels, hakuna sababu zilizotolewa isipokuwa watu wanahisi ni sababu za kuonyesha kombe la Dunia, je, inaweza kuwa ndiyo sababu ya kisheria?

=====
Updates

Waziri Nape Nnauye ameandika Twitter, amesema tayari ameshawaelekeza TCRA kufuatilia swala hilo.

1668973135077.png
 
Rejea kichwa Cha taarifa, Azam kisimbusi wameitoa tbc 1 kwenye orodha ya free local channels, hakuna sababu zilizotolewa isipokuwa watu wanahisi ni sababu za kuonyesha kombe la Dunia, je, inaweza kuwa ndiyo sababu ya kisheria?
Inasikitisha sana
 
Ndio tatizo la kuwa na mtoa huduma mmoja alieshika soko. Azam kiukweli wapo "too arrogant" na wao hawajapata haki ya kurusha matangazo WC so far.

Wapigwe faini maana sheria ipo wazi.
Mimi ndio maana nilijiapanga kununua DSTV nalipa mwezi mzima Kucheki Super Sport mechi zote 64 maana nilijua kutakuwa na uswahili kitendo cha TBC na ZBC kupata haki ya kurusha mechi hizi.
 
Possibly wao TBC ndio wametaka waondolewe. Huwezi wewe kua unajua sheria kuliko wao walivyokubaliana kibiashara.

Mteja yaani TBC analipa AZAM ili channel yake ionyeshwe, katika makubaliano hayo azam hawezi tu kuondoa channel kwenye huduma kibabe tu tena channel ya serikali
 
TBC ni waongo sana kudai kuwa wameshinda tenda kutangaza kombe la dunia.

Ikumbukwe national media zote wanapewa free to air hili kombe sasa Rioba anadangaya watu hapa kutaka kupiga hela, TAKUKURU ingilieni kati, TBC wanapata huduma kupitia kodi zetu sasa iweje wauze kuangalia kombe la dunia.
 
Ndio tatizo la kuwa na mtoa huduma mmoja alieshika soko. Azam kiukweli wapo "too arrogant" na wao hawajapata haki ya kurusha matangazo WC so far.
Wapigwe faini maana sheria ipo wazi.
Mimi ndio maana nilijiapanga kununua DSTV nalipa mwezi mzima Kucheki Super Sport mechi zote 64 maana nilijua kutakuwa na uswahili kitendo cha TBC na ZBC kupata haki ya kurusha mechi hizi.
Azam hajazuia ila DSTV ndio wamewazuia Azam kuonyesha hiyo michuano kupitia channel nyingine ambazo zinarusha hiyo michuano ambazo zipo kwenye king'amuzi.
Sababu DSTV ndiye mwenye haki ya kuonyesha hii michuano Tanzania, so Azam anaogopa faini.

Channel zote zinazo onyesha mpira kama Rwana TV,TV ya taifa za Kenya zote Azam kazipiga pini.
 
Back
Top Bottom