Je, ni biashara ipi nzuri kwa mtaji mdogo?

geekizuri02

Member
Oct 16, 2022
19
58
Changamoto kubwa katika jamii yetu kwa sasa ni AJIRA hasa kwa vijana, watu wamemaliza vyuo wakiwa na degree nzuri na matokeo mazuri lakini wako mitaani, hakuna ajira pia serikali yetu kila kukicha ni "Kujiajiri".

Kwa maoni ni biashara ipi mtu anaweza kuanzisha akiwa na mtaji mdogo kabisa kama laki moja(100.000) na akatoka kimaisha mjini?. Biashara inahitaji uvumilivu kwahivyo atakama huchukua muda au kuleta faida pole pole nayo bado ni biashara.
 
Badala haruhusu paypal watu wapokee pesa, wapunguze tatizo la ajira.

Yeye anaenda kuuza bandari. Hakuna mkataba wa milele duniani kote, mtu na matakle yake anasaini mkataba wa milele. Hapo hapo huyo mwenye matakle mawili ameshindwa kuruhusu paypal.
 
Laki 1 ni kubwa sana itagemea upo mji gani...biashara ukielewa mitaa utaelewa aina biashara itakayofaa
 
Fungua kanisa.
Njia nyingine
Omba msaada kwa waarabu, unahitaji kujenga msikiti na kisima cha kujitawazia halafu hela nyingine weka mfukoni.
Kuna mkoa mmoja kuna misikiti kila mtaa, watu wanapiga hela tu.
 
Kwa mtaji wako huo, utafute biashara ndogondogo na ambazo hutalazimika kulipa kodi au ushuru wowote ule. Maana kiukweli ni mdogo. Ungefanya biashara ya uchuuzi, ungepiga hatua.
 
Aliyejenga mlimani city alikuwa na nusu ya mtaji wako (elfu 50 tu)

Believe in yourself kabla hujauamini mtaji
 
Changamoto kubwa katika jamii yetu kwa sasa ni AJIRA hasa kwa vijana, watu wamemaliza vyuo wakiwa na degree nzuri na matokeo mazuri lakini wako mitaani, hakuna ajira pia serkali yetu kila kukicha ni "Kujiajiri". Kwa maoni ni biashara ipi mtu anaweza kuanzisha akiwa na mtaji mdogo kabisa kama laki moja(100.000) na akatoka kimaisha mjini?. Biashara inahitaji uvumilivu kwahivyo atakama huchukua muda au kuleta faida pole pole nayo bado ni biashara.
Matundamatunda,mkaa nk,Tatizo la Nchi hii wasomi wengi mawazo ya ni kuajiriwa!mtu akiwa na degree.Kwa wenzetu ni tofauti,Mfano vitality chrincko bondia wa Ukraine ni Dr bingwa lakini kajiongeza kuwa bondia.
 
Huko Ndio kwenyewe,kuuza maji jerojero,miwa,mihogo ya kuchoma,chips mayai,mayai ya kuchemsha,matunda kama matikiti unayaosha kwenye chombo Kisafi na kuyakataka vipandevipande zipo nyingi mkuu hata voucher stand ya mabasi!
 
Piga mitumba .
Zungusha. Usione soo.wanaume wanakamatika sana. Wanawake wananununua sana. Akili yako tu.
 
Back
Top Bottom