Je NGO'S zinapataje funds ??

Mar 26, 2018
76
38
Habari wana JF, natamani sana nifungue NGO ya ambayo itajihusisha na kuwaangalia na kuwatetea watoto wenye ulemavu na waishio katika mazingira magumu kwa kuwapa misaada midogo midogo na kuhakikisha wanapata haki za msingi kama elimu, afya nk. Nimeshafuatilia jinsi ya kusajili na ada za kusajilia.

Swali langu je, nikishaifungua nitawezaje pia kupata msaada wa funds kutoka mashirika mbalimbali na serikalini ili iniwezeshe kukamilisha malengo nilojiwekea katika kuwasaidia hawa watoto angalau, na je kwa Tanzania ni rahisi kupata hizo Funds. Mwenye ufahamu wa haya mambo atoe ufafanuzi
 
Inawezekana lakini siyo rahisi sana!

Kiufupi watoto yatima,walemavu,na wale waishio mazingira magumu,kwa miakaa kadhaa wametumika na wajanja kujipatia mitaji ya kuendesha biashara zao,kwamaana hiyo NGO za namna hiyo ni ngumu kupata misaada kutoka wa wafadhiri na wasamalia wa mataifa yaliyoendelea maana wanaona kama wanapoteza muda fedha zao.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom