Tate Mkuu
JF-Expert Member
- Jan 24, 2019
- 28,410
- 81,905
Samehe tu 7 mara 70! Hakuna namna. Ulitakiwa kuusoma mchezo kuanzia mwanzo. Sasa wewe ukawa unatoa tu kila uisikiapo sauti yake nzuri na ya kumtoa nyoka pangoni!Utapeli ulikua hivi.
Nilianzisha mahusiano nae nikiwa kwenye plan ya kuanzisha office ya kazi na nilijichanga sana kutafuta hela kwa ajili ya lan hio.
Mimi nilikua muwazi kuhusu plan yangu hio na niliamini kua ni mwenza wangu wa maisha.
Mimi nilimuamini kwasababu ya upendo wetu na jinsi tulivokua tunatambulishana kwa ndugu zetu nimeenda kwa ndugu zake.
Utapeli upo hapa
Alinambia kuna nyumba kanunua hivi karibuni na alikua analipia kwa awamu, muda huo niloanzasha mahusiano nae ndo alikua anakaribia kumaliza deni hilo.
Lakini yeye anaishi nyumbani kwao na nyumba tayari amekabidhiwa, hapo kwenye nyumba aloinunua alimuacha kaka mmoja awe anaishi ili nyumba iwe na mtu, kaka huyo alikua pia anashughulika na mambo yote ya pale.
Aliichokua anakifanya ananipigia simu mimi kuniambia nimtumie hela kaka ili baadhi ya mahitaji yafanikiwe, nilikua natoa hela kwasababu aliniaminisha kua hela zake zote alizitumia kwaajili ya kununua nyumba hio na mimi nilikua nampatia hizo hela hizo alizohitaji muda huo.
Nikimwambia nataka kuiona nyumba hio alinambia kua anaitaji anifanyie saprazi, kwahio sikupata kuiona nyumba hio, nipo nasubiria sapraizi lakini muda umekua mrefu.
Kisha nikagundua kua kumbe hakununua nyumba na hakuna kaka bali nilikua namtumia hela wakala wa Mpesa ambae yupo karibu nae nayy anaenda kuzifata hela hizo. Nikajaribu kupiga namba za mtu ambae alikua ananitumia ili nitume hela kwa namba hio, nikapata ukweli wote kuhusu yeye. Kiukweli alidanganya kila kitu na kikubwa zaidi alinitapeli. Ushahidi wa maongezi yetu wote upo kwa voce call hadi kwa text.
Kwangu mm nilikua na kazi na seheme yangu ya kazi, bali nilikua sina mwenza muda huo
Alitumia njia hio mkuu
Ukienda kumshtaki kila mtu atakushangaa.