Binti alituchanganya mimi na classmate wangu, tukampangia tukio

willpower

JF-Expert Member
Dec 3, 2019
404
2,271
Salamu za Januari wajumbe,
Miaka ile ya ujinga, nilikuwa na mahusiano na binti mmoja, mahusiano yalinoga haswa kuna wakati nikadhani kabisa kuwa sasa huyu atakuwa mke na mama wa watoto wangu.

Binti mweupe, sura na haiba ya kike, mwili wa wastani, kiuno kimejitenga vyema kama kisiwa cha Mbudya, huku akiwa na makalio ya wastani lakini laini kama mkate wa Gloria(wale walioishi Dar miaka ya 90 wataijua hii mikate) yamebinuka vyema.

Kwa kweli mtaani na kwa marafiki nilikuwa ninatamba kwa kuwa na binti mrembo kiasi kile. Nikajihakikishia kuwa nipo mwenyewe. Maana binti alikuwa anakuja na kulala pale karibu weekend zake zote.

Sasa kuna siku sehemu niliyokuwa ninaishi ikawa na hitilafu ya umeme; nikamwita fundi ambaye alikuwa na ofisi yake kama mtaa wa tatu hivi.

Fundi akafika na kurekebisha hitifalu, akiwa anajiandaa kuondoka, binti mrembo akaingia na wakasalimiana, binti akanikaribia na kunipa salamu kwa mahaba yote; nikampatia fundi ujira wake, akaondoka. Nikabaki na binti kujilia mema ya nchi, maana kwenye sekta hiyo alikuwa anajiweza haswa.

Jioni majira ya saa 11 naona Nokia 1100 inaita; jina la anayepiga simu ni ''Fundi Umeme''; nikahisi labda jamaa amesahu bisibisi au kuna maelezo anataka kunipa.

Nikapokea; fundi akasema '' kaka kuna mambo nataka tuzungumze ukiwa na muda niambie'' nikamjibu hatuwezi kuzungumza kwenye simu maana nina muda sasa hivi'' , jamaa akasema ''itakuwa vyema tukionana'' nikamwambia basi sawa; tuonane kesho karibu na ofisi yako, pale Bar 9 (hii ilikuwa Sinza sijui kama bado ipo).

Kweli siku ya pili nikamcheki jamaa, akaja pale Bar 9. Tukiwa tunapata chakula na vinywaji ndio jamaa akaanza kufunguka kama ifuatavyo; ''Kaka unajua sisi wote ni wanaume, kuna jambo nimeliona pale kwako; yule dada inaonekana ni mpenzi wako lakini mimi kuna jamaa namjua wana mahusiano na yule binti tena jamaa anataka kuoa kabisa''

Dah nikashtuka kidogo; nikawaza kweli huyu mwanamke ana mpenzi mwingine? Jamaa akaendelea kufunguka zaidi; namfahamu jamaa vizuri mahusiano yake na binti ni ya zaidi ya mwaka sasa'' Mpaka wakati huo mimi na huyo binti tulikuwa na miezi 6.

Fundi akaendelea; kiufupi katika hili wewe ndio mwizi wa mpenzi wa jamaa. Nikamweleza jamaa kuwa mimi na huyo dada tumekuwa wapenzi kwa miezi sita.

Akasema; hili jambo naomba twende nalo kiume kwa kuwa ulikuwa hujui chochote basi nitakukutanisha na jamaa ili muone namna ya kufanya.

Kufikia hapo nikasita; kuonana na mwanaume ambaye tumeshea mwanamke; tena huku jamaa akiwa anataka kuoa kabisa.

Nikamwambia sipo tayari ila nitaongea na huyu mwanamke kuhusiana na hizo habari ulizonipa. Fundi akaendelea kusema ''ila jamaa nimeshamwambia kuwa mwanamke wake nimemkuta mahali na nahisi ana bwana mwingine, japo sijasema ni wapi.''

Na hata ile jana huyo mwanamke alitoka kwa jamaa kisha akaja kwangu. Yaani kiufupi nilijitosa kwenye mabaki ya jamaa; yale ya kusema alikuwa ameshaloana kumbe robo saa iliyopita amemwagiwa vitu na mwanaume mwingine.

Kufikia hapo nikamuaga fundi ili nikaendelee na mambo mengine. Kwa mara ya kwanza kwenye maisha nikajikuta natembea lakini kichwa kama hakifanyi kazi.

Nikakumbuka stori zote za wanawake na masuala ya usaliti, iliniumiza sana japo nilikuwa najipa moyo kwamba inawezekana jamaa amemfananisha.

Jioni ile nikamcheki yule binti, akaniambia kuwa yupo nyumbani anapika, nikamuuliza unaweza kuja? Binti akasema sasa jana tu nilikuwa hapo mpenzi, nambo nije kesho'' tukaishia hapo.

Fundi akaniambia yule jamaa anasema mnaweza kumfundisha adabu huyu binti, nikauliza kwa namna gani? Yaani yeye kufikia hapa hataki tena kuendelea na huyu binti ila anataka binti ajue kuwa yeye anajua mambo anayofanya.

Nikasisitiza kwa namna yoyote ile, isiwe jambo la kumdhuru wala kumdhalilisha huyu mwanmke; Nikapata namba ya jamaa na kuongea naye, jamaa alikuwa ameumia sana maana alikuwa ameshamtambulisha kwa baadhi ya ndugu zake.

Katika mazungumzo tukaja kugundua kuwa tumemaliza Advance Level katika shule moja hapa mjini, tena mwaka mmoja tofauti ya combination. Tulipokutana kwa yule fundi ndio tukajua kuwa tunafahamiana kwa sura.

Jamaa akanipa stori nzima na yule mwanamke na namna alivyojitoa kwa ajili yake. Nikamwambia kuwa mimi kufikia hapo sina mpango wa kuendelea na yule mwanamke tena, na yeye pia akawa hana mpango japo wote tuliendelea kuwasiliana na yule mwanamke.

Kiukweli nikawa nafikiri namna ambavyo nilikuwa naenda naye kavukavu huku tukifanya mambo mengine , huku kumbe ana mwanaume mwingine, nikakumbuka zile safari alizokuwa anakuja kwangu saa tano usiku huku akiwa anatoka kwa jamaa.

Mwisho tukaafiki tukio lifanyike eneo la public, tukachagua B9; jumapili moja jioni nikamwambia huyu binti kututane hapo.

Nikakaa kona upande wa mashariki, meza yenye viti viwili, nikawahi kukaa kiti kinachoangalia mlango wa kuingilia, binti alipofika akaupa mgongo mlango.

Nikiwa na Nokia 1100 nikamtumia jamaa meseji, kipindi hiko meseji moja shilingi 40 nadhani; kuwa tumeshafika nikimtaka aje na yule fundi kwa pamoja.

Baada ya dakika 20 hivi fundi na jamaa yake wakaingia na kuja moja kwa moja nilipokuwa nimekaa. Wakanisalimia na mimi nikamtambulisha jamaa kuwa huyu binti ni girlfriend wangu, na nikageuka kwa binti na kumwambia huyu jamaa ni classmate wangu.''

Binti alijiinamia; huku amekunja leso yake ameziba mdomo. Ni wazi kuwa lile jambo lilimchanganya. Jamaa wakaenda kukaa meza ya jirani, dakika mbili baadaye binti akaondoka bila kuaga.

Ukawa mwisho wa mahuasiano kwangu na kwa jamaa pia. Nikampitishia nguo zake alizokuwa ameacha kwangu.
Nimekutana naye mwaka jana akiwa na afya njema kabisa mkoani Dodoma japo bado ana aibu ya lile tukio; ameolewa na ni mama wa watoto wawili.
 
Mkuu Mimi ni yule fundi umeme, jamaa etu aliendelea na demu kimya kimya bila wewe kujua, demu alimwomba jamaa msamaha, alimwambia jamaa kuwa alimpenda sana yeye kuliko wewe, walikuja kuachana baadae kwa sababu nyengine kabisa.
 
Sharing is caring, you like it or not mmoja wenu Kati yako na yule jamaa bado anaendelea kumla huyo binti.
Watu hawaachanagi kirahisi namna hyo bana.Kiporo kinaendelea kupashwa na mmoja wenu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom