Je Natapeliwa?

Likasu

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2011
Posts
857
Reaction score
441
leo asubuhi nimepokea ujumbe unaosema kwamba number yangu imeshinda 200,000 pounds katika shindano la nokia anniversary promo, kwa maelezo zaidi nimeekelezwa nitume mail kwenda nokia-uk@live.com au nipige number +447012950083. Je wadau hii kitu ipo au nataka kutapeliwa ?
 

Watakutapeli bureeee.... Iyo email tu haielekei kama inatoka kwa nokia!!
 

Hii kitu mbona kila siku tunasema kuwa ni UTAPELI!!! Kama hauamini piga hiyo simu uongee nao, wakikuomba bank details tuma ili uone maumivu!
 
Ni utapeli, usithubutu hata kujibu simu/email.
 
Mbona huu ni utapeli wa kizamani sana
 
Bora wewe paundi 200,000. Mwenzio paundi 650,000. Wife acha anipigie kelele nizifuatilie,kila nikimsomesha huu ni utapeli somo lilikuwa gumu kwake. Nikamwambia hebu google hiyo mesej... akagundua kuwa ni mchezo mchafu.
 
Yaani wewe ilale nyumbani kwako, uamke na kunywa chai afu ushinde mapaundibyote hayo? Kwani wewe ni nani jamani? Kijukuu cha mtume eeh?
 
jamani hizo ni pesa fuatilia uone mwisho wake lakini ukifika mahali wakikuambia utoe pesa ndipo uwatupe tena umbali wa kilometa kumi
 
Kwa akili ndogo tu, unadhani Nokia wanaweza kutumia email ya live.com?
 
Last edited by a moderator:
hivi unashindaje shindano ambalo hujashiriki?
 



ulishiriki shindano lolote kuhusiana na huo ujumbe?? Kama hukushiriki kuwa macho. Huwez vuna bila kupanda.
 
Wandugu jioni hii nimetumiwa msg kutoka namba +2347068891452 ikiniambia kuwa nimeshinda pound 200,000/= na ili kuzipata nitume email kwa Nokiauk-win@live.com au nipige +4470129500083.

Kiukweli haya mambo yameshanikosakosa mara kibao my principle ya "if it's too good to be true then maybe it is!" has always prevailed (recently) miaka ya nyuma nisha tapeliwa kama mara 2 hivi.
Nime google hii kitu nikakuta kumbe ni scam kubwa tu na ishawala watu kibao.

Hivyo chukueni tahadhari bandugu.
Link: The Nokia Lottery isn't real, don't fall for it – Nokia Conversations : the official Nokia blog

Niko apa apa bongo by the way!
 
Ebana kampuni ya nokia haiwez kutumia email ya live ya hotmail,mi walishantumia nimeshinda paund mil 80 kutoka yahoo uk wakataka account detail zangu.nkafikiria nkajua ni uongo coz huwez pewa hela bila kucheza kamal au kufanya kaz ."ther is no free lunch in economics.
 

Mkuu unajua paundi mil 80 ni sh ngapi za bongo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…