Epuka hawa matapeli (Your mobile # has won 1,000,000 Dollars! )

God'sBeliever

JF-Expert Member
Sep 1, 2015
5,790
3,020
Za leo ndugu.
Mwanzoni mwa mwaka 2013 nilipata message kwenye namba yangu ya voda kwamba your mobile number won 2000Pounds from NOKIA UK ANNIVESARY PROMO. Nilitumiwa hiyo message na +44... ambayo hiyo ni country code ya UK kweli wakanipa na email yao wakaniambia ni contact nao kwa hiyo email kwa maongezi zaidi na namna ya kupokea mkwanja wangu.
Ni kweli nilishakuta sehemu fulani kuna kuingiza namba ili uingie kwenye shindano so sikujiuliza sana maana nilihisi ni kweli nimeshinda.\
Basi nikaendelea kuwasiliana nao tuu huku wakitaka niwape details zangu kama birthday, phone numbers, job etc.
Baada ya process kuisha ilibakia tuu kupokea pesa, kwa sababu mimi niko africa na wao wako uingereza nkawaambia watumie western union ili wanitumie pesa zangu wakagoma wakasema mpaka niende huko mwenyewe au nimtume mtu afike hapo physically kwa ajili ya ku apply some fees na deduction ya kodi ili nipokee pesa yangu. Nikawaambia kama ndo hivyo kateni tax na hayo malipo mengine yanayohitajika halafu itakayobaki mnitumie kwa western union.
Wakagoma kabisa, nika kaa kama mwana nikawatext tena, hapa walichelewa ku reply ila walinijibu, huyu bwana bado aliendelea na msimamo wake.
Basi nikakatab shauri kabisa ila zile conversation ninazo hadi leo.



Leo nimepata nyingine hii imesema +1.... your mobile # has won 1,000,000 Dollars in T.MOBILE PROMO USA, to claim send your... hapo walitaka niweke details zangu kama kawaida.
Ni kweli niliwahi shiriki kwenye mtandao flan ivi unaitwa lottery... nishasahau ila hapa niliweka namba zangu na kujibu maswali yao ili nikishinda wawasiliane nami, kwa kweli ni mda kama mwaka uliopita hivi.
Chakushangaza nimepokea hiyo message kutoka namba ya tanzania ya voda +255.. sasa hapa najiuliza kwa nini wasinitumie hio message wenyewe?? naona huyu ni mwizi tuu baadae ntawasiliana nae.

Katika uchunguzi wangu nikaingia google na ku google promotion za hayo makampuni. Daa nlichokikuta ni balaa, nimekuta malalamiko kibao, ni mitandao inayohusika na hizo biashara imepinga. Message zote ni scam, wazungu kibao wameshaliwa humu! na wame contact wahusika wakuu na hao wahusika wamepinga na kusema hawahusiki wala hawaja fanya hizo promotion.



Kumbe siko peke yangu bwana. Kuna mtanzania nae kaliwa na T.MOBILE wenyewe wamejibu malalamiko yake vizuri, waweza fungua hii linkhttps ucheki hiyo conversation.
Hali ni ngumu sana hapa duniani.
Tuwe makini watanzania wenzangu, hakuna kitu cha bure, vya bure vinauwa wala haviji kwa njia hizo.
Please wataarifu na wengine kwani matapeli wamezidi sasa na wanatumia trick kali sana za kisayansi, wamejiandaa kukujibu, pia wakati wanaogea na wewe wanasoma saikolojia na udhaifu wako wanaingiza changa la mawe machoni.
 
Fanya kazi Mkuu hakuna maisha ya shortcut hizo details unazowatumia wenzako wanazifanyia kazi usishangae ipo siku utakuja kukamatwa kwa kutaka kujilipua au ukawa unatafutwa kama gaidi
 
Hao wanakuwaga ivyo sijui wanajuaje SIM mtu anayotumia, juzi nliingia google, naperuzi yakaja matangazo wananambia congratulations kampuni ya SIM hii nayotumia wanazawadi kwa users na SIM yako aina ya (wakataja aina ya SIM yangu) imefanikiwa kuingia kwenye droo mshindi anapewa iPhone 6 or Samsung TV ili kushiriki jibu maswali yafuatayo.
Naona watu wanacomment hapo how happy they are baada ya kupokea zawadi zao sijui wanajicommentia wenyewe!! nikacheck iyo kampuni iko USA
Nikajibu baada ya kujibu naletewa umefanikiwa kujiunga weka Namba yako ya SIM nkaweka... napewa terms and conditions nikazisoma ndo nkajua utapel wao, ntakuwa nakatwa 600 daily. Watu wengi hawasomi terms and conditions wao kila kitu wanabonyeza accept ndo inawacost
 
Wadau kuna hii sijui taasisi ya kukopesha pesa kupitia tigo inaitwa L-Pesa sio matapeli kweli.
Kwa sababu wanalazimisha uingize namba ya simu, tarehe ya kuzaliwa na profile picha eti ndio upate mkopo.
Kibaya zaidi na password wanakupa wenyewe.
Ninachoshangaa tigo hawajalizungumzia hili kabisa.
 
Back
Top Bottom