Je, mwaka huu kutakuwa na sherehe za uhuru?

Je, mwaka huu kutakuwa na sherehe za uhuru?

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2013
Posts
40,823
Reaction score
46,943
Kama tutaahirisha tena, naomba hizo pesa ziende kuweka lami mchepuko wa kutokea Tabata kimanga hadi jeshini, jana wapitisha greda lakini bado hali ya tope sio nzuri kwa kweli. Tutashukuru sana kama tutawekewa lami maana magari yote yanayoelekea kimanga na hata mengine yanayoelekea segerea nayo hutumia mchepuko huu ili kukwepa foleni ya kuzimu ya kuanzia Tabata relini hadi bima, ni foleni ya hatari sana! Pia hii itatupa mwanya wa kuomba ruti ya daladala Sumatra ya kutokea mawasiliano hadi Tabata Kimanga, hii itapunguza muda wa kusafiri na foleni kutoka masaa mawili na dakika zake hadi kufikia muda wa dakika 25 tu kutoka mawasiliano hadi Kimanga. Mbunge wetu sijui anaitwa nani lakini kama anasikia afanyie kazi.
 
Mbunge wenu ni Bonna Kalua,ila kipaumbele cha sasa ni kuzuia siasa siyo barabara, tumeshahamisha masafa huko
 
Hii sera ya kubana matumizi soon watoto watasahau kumbukumbu ya siku ya kupata uhuru kwa taifa letu
 
Sherehe mwaka huu zitakuwepo kama kawaida.Kuhusu hiyo barabara yenu wasiliana na mbunge wenu au amueni kujichangisha kwa ajili ya maendeleo yenu.
 
Kuwepo au kutokuwepo kwa sherehe anajua Ngosha pekee yake hakuna mwingine anayejua hadi muda huu.
 
Sherehe mwaka huu zitakuwepo kama kawaida.Kuhusu hiyo barabara yenu wasiliana na mbunge wenu au amueni kujichangisha kwa ajili ya maendeleo yenu.
Serikali itoe 80% kama ilivyo ada, sisi tutachangia 20%
 
Tukirejea ya mwaka, 2015 je ? Ndio itavokuws sasa 2016 ? Hakuna fununu ya msandalizi ya shamrsshsmra ama gwaride?Hskuna tamko?
 
Sherehe itakuwepo, na mgeni rasmi ni mtukufu rais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania, mh, Dr. John Joseph pombe magufuli
 
km hazitakuwepo miundo mbinu ya mjini hapa mibovu sana, mvua ikishesha kidogo tu balaa, nashauri hizo pesa watengeneze mitaro ya kupitia maji wakati wa mvua, tafadhalini sana
 
Iwepo ili iweje, unataka kutukosesha barabara wewe. Safari hii zamu ya Gairo kupata barabara.
 
Ingependeza tukafagia kufanya usafi majumbani ili tuokoe mamilioni
 
Katika hali ya kawaida media ingalishaanza kutoa makala zinazohusu siku hiyo mfano hotuba zenye historian hiyo makini kimya na hakuna kinachozungumziwa.Kweli Luna mabadiliko
 
Saizi tungalijua michezo maalum ,Mgeni maalum, Halaiki nk
Nitashangaa kama tutatumis fomeshini ya mwaka Jana its unfair
 
CywBa9nWIAAWgMK.jpg:large
 
Back
Top Bottom