"Mwanzo 1:26
Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi."
"Yohana 4:24
Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli."
Kwa sisi Wakristo.
Tunatambua kuwa Mungu hana Mwili kama wa Binadamu.
Kwa maana hiyo hana viungo vya mwili kama Masikio, Mkono, Macho, nk. ya Nyama.
Mungu ana uweza wote, uweza ambao mfano wake ni kazi za viungo vya Binadamu.
Yaani anaona, anatembea, anasikia,nk
Zaidi ya hapo Mungu ana Hekima Akili, Busara nk.
Mambo ambaye wanyama wengine hawana.
Hata hivyo Mungu yeye ni Muweza wa yote hivyo kutofananishwana kiumbe chochote.
Hivyo basi Binadamu tumekuwa mfano wa Mungu sio tu kwakuwa tunasikia kama yeye anavyoweza kusikia.
Bali tuna Hekima na Busara na Akili, ambazo Wanyama hawana.
Kuhusu Umbo la Mwili, sio kama Mungu ana umbo kama la Binadamu bali
Umbo la Binadamu ndio umbo ambalo Mungu analipenda zaidi ya maumbo ya wananyama wengine.
Ngoja ninukuu hapa.
"Mwanzo 18:1
Bwana akamtokea Ibrahimu karibu na mialoni ya Mamre, alipokuwa ameketi mlangoni pa hema yake mchana wakati wa hari."
"Mwanzo 18:2
Akainua macho yake akaona, na tazama, watu watatu wamesimama mbele yake. Naye alipowaona alipiga mbio kuwalaki kutoka mlangoni pa hema, akainama mpaka nchi,"
Hapa tunaona Mungu katika Agano la Kale, akimtembelea Nabii wake katika Umbo la Kibinadamu.
"Yohana 1:1
Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.
Yohana 1:14
Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli."
Hapo tunaona Katika Agano Jipya Mungu anakuja kutuhubiria Habari Njema ya Ukombozi wa Mwanadamu ( Injiri) kwa kuuvaa Mwili wa Binadamu Yesu Kristo wa Nazareti.
Nukuu za hapo juu zinatuambia kuwa Mungu analipenda umbile la Binadamu, umbo ambalo amelibuni mwenyewe.
Na huwa analitumia anapotaka kukutana na Binadamu kama alivyolitumia kwa Nabii Ibrahimu na kwa Vizazi vya Agano Jipya ambalo Manabii walilitabiri huko zamani.
"Yeremia 31:31
Angalia, siku zinakuja, asema Bwana, nitakapofanya agano jipya na nyumba ya Israeli, na nyumba ya Yuda.
Yeremia 31:32
Si kwa mfano wa agano lile nililolifanya na baba zao, katika siku ile nilipowashika mkono, ili kuwatoa katika nchi ya Misri; ambalo agano langu hilo walilivunja, ingawa nalikuwa mume kwao, asema Bwana.
Yeremia 31:33
Bali agano hili ndilo nitakalofanya na nyumba ya Israeli, baada ya siku zile, asema Bwana; Nitatia sheria yangu ndani yao, na katika mioyo yao nitaiandika; nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.
Yeremia 31:34
Wala hawatamfundisha kila mtu jirani yake, na kila mtu ndugu yake, wakisema, Mjue Bwana; kwa maana watanijua wote, tangu mtu aliye mdogo miongoni mwao hata aliye mkubwa miongoni mwao, asema Bwana; maana nitausamehe uovu wao, wala dhambi yao sitaikumbuka tena."
Hivyo basi Umbo la Sisi Binadamu ndio Umbo linalotiliwa Kipaumbele na Mwenyezi Mungu.
Ndilo umbo pekee alilowahi kulitumia.
Ndilo Umbo lake, linalo akisi Sura yake, na mfano wake.