Je, Mungu aliumba dunia kwa miaka Elfu 6?

Je, Mungu aliumba dunia kwa miaka Elfu 6?

Hakuna sehemu kwenye Biblia iliyosema dhahiri kuwa mwaka mmoja mbinguni ni sawa na miaka buku bali inasema 'ni kama'
 
Kwa mujibu wa Biblia takatifu Mungu aliumba Dunia kwa siku sita na kumpumzika siku ya saba kulingana na kitabu cha Mwanzo.

Lakini kuna dhana ya kwamba siku moja mbinguni ni sawa na miaka elfu moja duniani pia nikinyume na kwamba miaka elfu duniani ni sawa na siku moja mbinguni.

Pia kulingana na dhana hiyo tunaweza pata kitu hiki, kwamba Mungu alipumzika siku ya saba hii inaweza toa taafsiri kuwa Mungu alipumzika miaka elfu moja baada ya kuumba dunia.

Swali muhimu la kujiuliza ni kwamba siku ambazo dunia iliumbwa na Mungu zinahesabiwa katika hali ipi ya kuhesabu siku kidunia au kimbinguni?

Wajuzi wa mambo naomba ufafanuzi katika hilo.

El perdode
Swali fikirishi kwa kweli....
 
Ukichukulia uumbaji kwa muktadha huu wa "cycle" za billions of years, basi dhana hii ya uumbaji inakubalina na dhana ya "Big Bang" na evolution zinazotetewa sayansi!

Hizo "siku" sita ni nyakati sita.

Nyakati ni "cycles", umri wa dunia ni mabilions ya miaka, sasa ukigawanya hayo mabilions ya miaka utapa kila nyakati una umri wa bilions kadhaa za miaka.

Katika kila nyakati umbo la dunia lilikuwa likibadilika hadi nyakati ya mwisho (ya 6) dunia ilipochukua sura kamq hii t unayoiona leo, sura ambayo ina mito, maziwa, bahari, Ozone layer, atmosphere, viumbe hai nk,.

Mungu kupumzika katika siku ya 7, maana yake (yawezekana) ni kwamba katika nyakati ya 7 duniani hakukutokea au hakutatokea mabadiliko yoyote yaani Mungu hakufanya commandment yoyote kubadilisha umbo la dunia, Mungu kupumzika haina maana kwamba Mungu alichoshwa na shughuli za uumbaji na akaamua kupumzika, lazima tukumbuke kuwa Mungu ni mkamilifu katika kila hali, hasinzii, halali, hali, hanywi, hachoki nk, tukisema kwamba Mungu alipumzika jinsi tunavyopumzika sisi viumbe vyake basi ipo siku (apishe mbali) wstu watasema Mungu atakufa kama jinsi viumbe wake tunavyokufa. Mungu apishe mbali na atuepushe na fikra mbovu za kumdhalilisha.
 
Sasa mkuu biblia inaposema Mungu alipumzika siku ya saba ina maana gani? Maana kulingana na maelezo yako umekataa
Kwenye biblia nilizosoma sikumbuki inayosema Mungu alipumzika siku ya Saba. La hasha.

Maneno yaliyotumika Ni; Mungu alistarehe siku ya Saba. Akaacha kuifanya kazi aliyo kua akiifanya.

Maana yake kwa maneno hayo ni kwamba hakuchoka, ila aliridhika na alichokifanya akaacha kuumba. Maana aliona vimetosha.

Kuacha kufanya kazi haimaanishi umechoka.

Hata sisi binadamu. Unaweza ukafanya kazi yako ikakamilika ikakuridhisha. Ukaona imetosha. Hapo unaacha. Hata mjenzi akikamilisha ujenzi wake anaacha. Aendelee ili iweje?

Siku ya Saba Mungu hakupumzika.

Aliacha kufanya kazi ya Uumbaji. Na biblia nilizosoma zinaongezea Akastarehe.
 
Mkuu sasa utakuwa vipi na imani juu ya jambo fulani wakati hujui msingi wake?
Basi unaruhusiwa kuchunguza, na ndo utajua hata alie andika amekuficha mengi sana mfani Adamu aliumbwa na lilithi na sio Hawa, hawa aliumwa baada ya makosa ya lilithi.
 
Ukichukulia uumbaji kwa muktadha huu wa "cycle" za billions of years, basi dhana hii ya uumbaji inakubalina na dhana ya "Big Bang" na evolution zinazotetewa sayansi!


" the Big bang" ni kwa ajili ya uumbaji wa ulimwengu wote na evolution (cycles) ni katika dunia tu. Hizo cycles kwa maana ya mabadiliko makubwa yametokea katika nyakati 6.

"The big bang, Expanding universe na Black hole" ni concepts zinaungwa mkono na Quur'an tukufu, kitabu pekee cha dini kilichozungumzia hizo concepts tangu miaka 1400 kabla ya Wanasayansi.
 
Kiujumla swala la Uumbaji, yakiwemo na maswali Mengi ya dini, ni maswali ya kifalsafa.

Kwa uelewa wangu, Muda sio tu relative, bali binadamu tumeweka na kujiwekea hesabu ya Muda ili tuishi kimpangilio.

Ila kiuhalisia hakunaga mwanzo na mwisho, ila upo mwanzo wa Jambo na mwisho wa japo, mwanzo na mwisho wa tukio, nk.

Mwanzo wa Maisha na mwisho wa Maisha, ya kiumbe au tukio.

Kuna dhana ya Mungu Hana mwanzo Wala mwisho. Mimi ni Muumini wa hiyo dhana.
Kama ana mwanzo na mwisho hiyo hawezi kuwa Mungu. Labda mmoja wa miungu" demigod/ or Idols"

Ila Mungu aliye mmoja hapaswi kuwa na mwanzo wala kuwa na mwisho wa existence yake.

Vinginevyo ni Bora kusema hakuna Mungu.

Biblia ilivyoandikwa imeandikwa na mwanadamu. Kuanzia ikiwa ni kitabu kimoja kimoja, kabla havija kusanywa na kuwa kitabu kimoja.
Enzi za Musa akiwa na vitabu vya Sheria/torati. Huo ndio ulikua mwanzo wa biblia.

Simulizi za Uumbaji zilianza kwenye vitabu vya Musa, kwenye kitabu cha Mwanzo. Fikiria kwa teknolojia, Maendeleo,Elimu, na Uelewa wa watu wa kipindi Cha Musa, Miaka mingi kabla ya Yesu, maana yake Zaidi ya Miaka elfu mbili iliyopita. Kungekuwa na namna gani Bora ya kuwaelezea watu wa kipindi hicho juu ya Uumbaji zaidi ya jinsi Musa alivyowaelezea kwenye kitabu cha Mwanzo.

Bila shaka namba rahisi kwa uelewa wa watu wa kipindi kile, ilikua lazima Musa avunje Zama za Uumbaji kwa kusema siku ili aweze kueleweka.

Ila siamini Kama kweli Uumbaji ulifanyika ndani ya siku sita, yaani masaa 24×6. Kama tunavyoelewa Sasa. Au Kama ambavyo yamekuwepo siku zote.

Nakubaliana na aliyesema hizo siku sita zilikua nyakati ambazo pengine ni Miaka Bilioni Moja, kwa kila wakati.

Sasa fikiria kwa kipindi Cha Musa hata neno Bilioni lilikuwepo?

Maana hata ukiangalia msamiati ulioo yesha namba kubwa iliotumika kwenye biblia ni elfu.
Sana sana wakitakuonyesha ni zaidi ya elfu litatumika neno maelfu kwa maelfu. Na lilitumika kwenye kuonyesha idadi ya vitu au watu.

Sasa achana na Hesabu hiyo rahisi.

Embu, fikiria Musa angepewa ufunuo wa Uumbaji kwa namna ambayo Leo hii sayansi inauelewa. Yaani Ile process yoote ya Evolution Kama sayansi inavyozidi kugundua Leo hii, ndio Musa angelielewa Hilo kipindi hicho.

Angemuelezea Nani ambaye angemuelewa. Na ingefaa nini kwenye kuwafanya watu aliokua akiwaongoza( waizraeli) waweze kumcha Mungu?

Hivyo naamini Maelezo ya Uumbaji Kama yalivyo kwenye kitabu cha Mwanzo Ni Simple Version ya Uumbaji, ambayo lengo lake lilikua ni watu wa kipindi hicho waweze kuelewa Mungu yupo na ndio chanzo Cha vyote vilivyoumbwa, hivyo wanapaswa kumcha yeye.
 
Na wakati anaumba aulikuwa na glass ya juice ya tende pembeni
 
Back
Top Bottom