Hatua za kupata mirathi

Free Again

Senior Member
Dec 20, 2015
114
93
Nawasalimu !

Mwaka 2013 nilimpoteza kaka yangu kwa ajali ya pikpiki. Yeye alikuwa mwalimu wa shule ya msingi na mimi kipindi hicho nilikuwa chuo mwaka wa Kwanza.

Baada ya mazishi na msiba kuisha, kikao kilikaa kwa ajili ya mirathi na mimi ndiye niliteuliwa kuwa msimamizi wa mirathi, lakini sikuweza kusimamia kwa sababu nilikuwa bize na chuo.

Kwa hiyo nilishauriwa ni deligate hilo jukumu kwa mtu mwingine aliye free kidogo ambaye alikuwa shemeji yaani mke wa marehemu. Nikaandika barua ya kubadilisha msimamizi wa mirathi.

Sasa tangu mwaka huo anafuatilia, lakini wanampiga kalenda tu. Kuna wakati wanasema walioandikwa kwenye mirathi wafungue akaunti Maana pesa iko karibu kutoka lakini ukweli hakuna kinachoingizwa.

Sasa, nasikia kuna watu wanapata mirathi. Je wanafuata HATUA zipi? Vitu gani vinasababisha kupata au kukosa kwa mirathi hata kama umefuata HATUA zote?

Je miaka yote hii (karib 10) mirathi haija expire?

Watalaam/wajuzi/wanasheria nisaidieni!
 
Nawasalimu !

Mwaka 2013 nilimpoteza kaka yangu kwa ajali ya pikpik.Yeye alikuwa mwalimu wa shule ya msingi na mimi kipindi hicho nilikuwa chuo mwaka wa Kwanza.

Baada ya mazishi na msiba kuisha,kikao kilikaa kwa ajili ya mirathi na mimi ndiye niliteuliwa kuwa msimamizi wa mirathi, lakini sikuweza kusimamia kwa sababu nilikuwa bize na chuo.

Kwa hiyo nilishauriwa ni deligate hilo jukumu kwa mtu mwingine aliye free kidogo,ambaye alikuwa shemeji yaan mke wa marehemu. Nikaandika barua ya kubadilisha msimamizi wa mirathi.

Sasa tangu mwaka huo anafuatilia,lakini wanampiga kalenda tu. Kuna wakati wanasema walioandikwa kwenye mirathi wafungue akaunti Maana pesa iko karib kutoka lakini ukweli hakuna kinachoingizwa.

Sasa, nasikia kuna watu wanapata mirathi. Je wanafuata HATUA zip? Vitu gan vinasababisha kupata au kukosa kwa mirathi hata kama umefuata HATUA zote?

Je miaka yote hii ( karib 10) mirathi haija expire?

Watalaam/wajuzi / wanasheria nisaidien!
Fafanua unafuatilia mirathi gani au mafao gani? Mirathi haina expire mpaka ufunge mirathi mahakamani.
 
Fafanuwa unafuatilia mirathi gani au mafao gani? Mirathi haina expire mpaka ufunge mirathi mahakamani.
Mwanzoni pale nimeanza kuelezea kuwa, kaka yangu alifariki alipata ajali ya pikipiki na alikuwa mwalimu.
 
Nawasalimu !

Mwaka 2013 nilimpoteza kaka yangu kwa ajali ya pikpik.Yeye alikuwa mwalimu wa shule ya msingi na mimi kipindi hicho nilikuwa chuo mwaka wa Kwanza.

Baada ya mazishi na msiba kuisha,kikao kilikaa kwa ajili ya mirathi na mimi ndiye niliteuliwa kuwa msimamizi wa mirathi, lakini sikuweza kusimamia kwa sababu nilikuwa bize na chuo.

Kwa hiyo nilishauriwa ni deligate hilo jukumu kwa mtu mwingine aliye free kidogo,ambaye alikuwa shemeji yaan mke wa marehemu. Nikaandika barua ya kubadilisha msimamizi wa mirathi.

Sasa tangu mwaka huo anafuatilia,lakini wanampiga kalenda tu. Kuna wakati wanasema walioandikwa kwenye mirathi wafungue akaunti Maana pesa iko karib kutoka lakini ukweli hakuna kinachoingizwa.

Sasa, nasikia kuna watu wanapata mirathi. Je wanafuata HATUA zip? Vitu gan vinasababisha kupata au kukosa kwa mirathi hata kama umefuata HATUA zote?

Je miaka yote hii ( karib 10) mirathi haija expire?

Watalaam/wajuzi / wanasheria nisaidien!
Pole kwa madhila.

Nitajibu kwa kifupi kwa kuwa kuna somo nitalipost wiki hii inayoanza lihusulo mirathi tu, huko nitaeleza kwa kina.

Awali, wewe uliposhindwa kusimamia mirathi, hukutakiwa kuandika barua ya kubadilisha mrithi na kumpa huyo shemeji yako. Ulichotakiwa kufanya ilikuwa ni wewe kujitoa kusimamia mirathi na familia iteue mtu mwingine tena.

Kuhusu hatua za kufuata ni hizi:
1. Mteuliwa kuomba uteuzi rasmi mahakamani (mliyemteua anaomba mahakamani kupewa barua za usimamizi wa mirathi) - hapa warithi wataitwa nahakamani kuthibitisha uteuzi na idadi ya mali nk;

2. Msimamizi kufuatilia mali na madeni ya marehemu (mali halisi au mafao kwenye mifuko ya jamii nk)

3. Msimamizi kulipa madeni ya marehemu (kama yapo);

4. Msimamizi kugawa mali kwa warithi wa marehemu (hapa mifuko ya jamii hujipa mamlaka kwa kugawa mafao yenyewe kwa warithi kwa akaunti za benki)

5. Msimamizi kuwasilisha orodha ya mali

6.Msimamizi kuonesha namna alivyogawa mali na kufunga mirathi
 
Pole kwa madhira.

Nakushukuru sana ndugu, ngoja nisubiri somo hilo, pengine nitajua na kujifunza mengi. Hapa umenipa mwanga lakini haunitoshi kuona
 
Mkuu tiririka nalo
 
Jaman naomba msaada eti file la mirathi likifika mahakama kuu linachukua miezi mingapi kwa makadilio??
 
Back
Top Bottom