Kwa kipindi kirefu inaaminika kuwa mtu akipwata na kifafa/degedege anaweza akameza ulimi hivyo hutumia kijiko,kijiti au kumuweka kiganja cha mkono mdomoni kama njia ya kumsaidia.
je kunauwezekano wa mtu kumeza ulimi?
je kunauwezekano wa mtu kumeza ulimi?
- Tunachokijua
- Tunachokijua
Ulimi ni kiungo cha misuli ndani ya kinywa kinachosaidia kufanya kazi mbalimbali muhimu za mwili. Mfano, kuzungumza, kutambua ladha, kumeza, kutafuna na kusogeza chakula. Kimaumbile ulimi umeunganishwa na sakafu ya kinywa kupitia tishu inayojulikana kama lingual frenulum pamoja na misuli inayoushikilia.
Madai
Kuna madai kwamba mtu anaweza kumeza ulimi wake, hasa wakati wa degedege, kupoteza fahamu au akiwa amelala. Kutokana na madai hayo, baadhi ya watu huamini kwamba wakati wa degedege ni muhimu kuweka kijiko, kidole au kitu kingine ndani ya mdomo ili kuzuia ulimi kumezwa.
Uhalisia
Je, mtu anaweza kumeza ulimi wake?
Baada ya kufanya ufuatiliaji kwa kupitia makala na tafiti za afya ambapo inabinisha kuwa hakuna uwezekano wa mtu kumeza ulimi wake.
Madai haya kwamba mtu anaweza kumeza ulimi wake si sahihi. Kisayansi haiwezekani mtu kumeza ulimi wake. Kinachoweza kutokea wakati wa degedege au mtu anapopoteza fahamu ni misuli ya mwili ikiwemo ulimi kulegea.
Hivyo mtu akiwa amelala chali, ulimi unaweza kusogea kuelekea nyuma ya koo na kuziba njia ya hewa kwa sehemu au kabisa. Hali hii ndiyo mara nyingi huchanganywa na “kumeza ulimi.”
Hivyo madai kwamba mtu anaweza kumeza ulimi wake ni si ya kweli. Ulimi unaweza kurudi nyuma na kuathiri njia ya hewa au kuumia wakati wa degedege, lakini hauwezi kujitenga na kinywa na kumezwa.
Cha kufanya mtu akipatwa na degedege
Mtu akipatwa na degedege, usiweke kijiko, kidole au kitu chochote mdomoni na usijaribu kushikilia ulimi wake. Mtoe kwenye vitu vinavyoweza kumuumiza, mlaze sehemu salama na mweke kitu laini chini ya kichwa. Baada ya degedege kuisha, ikiwa hajitambui lakini anapumua, mgeuze katika mkao wa kupona (recovery position) ili kusaidia kuweka njia ya hewa wazi. Ikiwa hapumui kawaida au hali yake ni ya dharura, tafuta msaada wa kitabibu mara moja.