Je Mtangazaji wa BBC Swahili Mariam Dodo Abdallah hana Kalenda nyumbani Kwake hadi anakengeuka hivi?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,544
108,878
Nashindwa sana kumuelewa huyu Mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC Mariam Dodo Abdallah kwa vitendo vyake vya kuwa anakosea / anakengeuka / anavapa kila mara anapokuwa akitangaza iwe ni asubuhi ( amka na BBC ) au jioni ( dira ya dunia ).

Huko nyuma nilidhani labda ni Ugeni au matatizo mengine ya Kiufundi ndiyo yamekuwa yakipelekea Yeye ' kuvapa ' kila anapokuwa hewani ila alichokifanya leo asubuhi Saa 12 katika Kipindi changu pendwa cha ' amka na BBC ' kimenifanya nianze kuamini kwamba huyu Mtangazaji labda ana matatizo yanayohitaji ' counseling ' ya haraka.

Wakati akifungua Kipindi leo asubuhi alisema kuwa leo ni siku ya Jumanne tarehe 2 kisha baadae akasema tena kwamba leo ni Jumatano tarehe 2 na hapo hapo tena haraka haraka akasema kwa ' bashasha ' zote kuwa leo ni siku ya Jumanne tarehe 2 mwezi August 2017 kisha akaendelea na matangazo ya BBC kama ilivyo kawaida na hata huko mbele ya Kipindi alisema tena leo ni Siku ya Jumanne.

Mshangao wangu uko sehemu moja tu kwamba Je huyu Mtangazaji Nyumbani Kwake hana hata Kalenda? Je hapo Studioni BBC hawana Kalenda? Je ni kwanini kati ya Watangazaji wote wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC ni Yeye tu ndiyo ambaye huwa anakosea kosea hasa akiwa hewani?

Mwisho nichukue tu nafasi huu kutoa pongezi zangu za dhati kabisa kwa Uongozi wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC kwa kuweza kutuletea Mtangazaji ambaye kiukweli anatuvutia sana Sisi wasikilizaji ' tuliotukuka ' kwa Utangazaji wake mzuri na ulio ' romantic ' kabisa aitwae Ambia Hirsi. Huyu Binti ama hakika ananifanya ' nisibanduke ' BBC Idhaa ya Kiswahili.

Nawasilisha.
 
Hata mi Leo asubuhi kanishangaza sana. Ambia ni binti wa kisomali mkuu, jipange upeleke mahari kama upo single. Somalia sio mbali ila nadhani wana ndugu Kenya pia.
 
Maisha yanaenda kasi sana yaani nina siku nyingi sijasikiliza BBC kiswahili!!!
 
Back
Top Bottom