Zuhra Yunus wa Dira ya Dunia

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,910
30,253
ZUHRA YUNUS, BBC, NA MAGOMENI MAPIPA

Ilikuwa Zuhra Yunus anaondoka BBC sasa ishakuwa Zuhra kaondoka.

Labda nianze kwa kusema kuwa nina ''sentiments,'' mapenzi na BBC Idhaa ya Kiswahili toka udogoni katika miaka ya 1960 na hadi leo naweza nikakuimbia ''signature tune,'' iliyokuwa inafungua kipindi.

Miaka hiyo si kama nilikuwa msikilizaji bali nikisikia hiyo ''signature tune,'' najua hiyo BBC.

Baadae tena ukubwani nikawa nasikiiza BBC London kipindi nilichokuwa nakipenda ni ''Magic Mystery Tour,'' kipindi cha muziki wa zamani na maelezo yake.

Baadae zaidi akili zimejaza kichwani nikawa nikitaka habari za uhakika nafungua BBC.

Mtu aliyeniingiza Bush House London alikuwa Ahmed Rajab mwaka wa 1991 na kule kuisikia BBC radioni kukageuka kuiona BBC yenyewe ikitangaza mubashara na mimi nikapata fursa ya kufanya kipindi cha ''majaribio'' kutoka studio za BBC Glasgow, Scotland.

Hiki ni kisa kirefu Insha Allah iko siku nitakieleza lakini muhimu ni kuwa magwiji wa utanganzaji kama Aisha Yahya na Chama Omari Mtata waliponisikia wakaniambia kuwa ninacho kipaji cha kuwa mtangazaji.

Zuhra Yunus nilimfahamu siku moja mwaka wa 2014 alinipigia simu kutoka London akinitaka nishiriki katika kipindi cha BBC kuhusu Vita Vya Kwanza Vya Dunia (1914 - 1918) ambacho kitarekodiwa British Council, Dar es Salaam.

Sijui alijuaje kuwa nilikuwa na Shajara za Vita (War Diaries) za Lance Koplo Kleist Sykes wakati akipigana katika jeshi la Wajerumani katika vita hivyo.

Hivi ndivyo nilivyojuana na Zuhra Yunus lakini kwa bahati mbaya sikuweza kushiriki katika kipindi kile.

Alipokuja Dar es Salaam alinitembelea nyumbani kwangu Magomeni Mapipa na katika watu waliofurahi sana kukutana na Zuhra ni mabinti zangu na ikiwa vurugu ya kupiga picha na yeye,

Kipindi chake Dira ya Dunia kilikuwa hakitupiti kwa hiyo alishafika ndani mwetu kabla ya yeye mwenyewe kuvuka kizingiti cha mlango wetu kwa miguu yake.

Nyumba yetu inatazamana na kibla cha msikiti na nje ya nyumba kuna duka la vyakula, fundi wa radio, na vyombo vya elektroniki na yupo kinyozi kwa hiyo muda wote panakuwa na watu.

Nakumbuka nilipokuwa namsikindikiza Zuhra kuingia kwenye gari yake bwana mmoja alinyanyuka kutoka barza ya msikiti na kupiga kelele huku akitujia, ''Huyu si Bi Zuhra huyu wa BBC?''

Na Mashaallah Zuhra kama unavyomuona katika runinga na kwenye maisha yake ya kawaida haiba yake hivyo hivyo mtu wa bashasha na mchangamfu.

Ikawa sasa pale nje nyumbani kwangu mazungumzo ni Zuhra, Zuhra, Zuhra.

Kwa hakika ni mimi nikawa jina langu Zuhra kalipandisha juu kuwa nimetembelewa na Zuhra Yunus wa BBC, London.

Ikawa nimepata dada na Zuhra kila akija Dar es Salaam lazima aje kutusalimia nyumbani.

Kiasi cha kama miaka miwili, mitatu hivi siku hiyo katoka London kaja nyumbani akaniambia kuwa anakusudia kuandika kitabu.

Nikamtia moyo sana aandike hicho kitabu hasa pale nilipojua kuwa anaandika kitabu cha maisha ya mtu mashuhuri sana lakini alikataa kata kata kunitajia jina.

Kajiponza.

Ikawa kila akinipigia simu au akija nyumbani mimi ninae na kitabu.
Akiniandikia ujumbe mfupi kwenye simu nitauliza kitabu.

Kitabu kinakwendaje na lini kitabu kitakamilika.
Hayawi, hayawi, mwishowe yakawa.

Siku hiyo niko nyumbani nimeletewa nakala ya kitabu chake ambacho sasa ni kitabu maarufu, ''Biubwa Amour Zahor Mwanamke Mwanamapinduzi.''

Sikukiweka chini hadi nilipokimaliza.

Tokea asubuhi Zuhra aliponieleza kuwa anakusudia kuandika kitabu nilijua kitakuwa kitabu kizuri.

Utabiri wangu ulikuwa tawire.
Zuhra akanialika katika uzinduzi wa kitabu Zanzibar na Dar es Salaam.

Shughuli zote mbili nilihudhuria.

Katika uzinduzi wa kitabu iliwekwa video fupi ya watangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC wakimpongeza Zuhra Yunus kwa kitabu chake.

Nilimuona Chama Omari Matata na imepita miaka mingi sijakutananae.
Nilimuona pia Salim Kikeke ambae keshapata kunihoji Dira ya Dunia.

Nimeweka picha hapo chini ya Chama tukiwa BBC Club, Bush House na myingine nikihojiwa na Salim Kikeke.

Chama ni huyo picha ya mwisho wa kwanza, aliyesimama nyuma yake ni Mohamed Maharage Juma sasa Balozi Maharage, Mwandishi na Ali Saleh.

Hakika miaka imekwenda.
Ukweli nimetaabika sana kusikia Zuhra Yunus anaondoka BBC na naamini tuko wengi.

Zuhra hajatuambia kuhusu Zoom na Zu.
Nilikuwa sipungui ukumbini kwake.

Tunamngojea huko.

Picha ya pili Zuhra Yunus akiwa Magomeni Mapipa, picha ya tatu akimsainia Mama Getrude Mongela nakala ya kitabu chake.

Namtakia dada yangu huyu kila la kheri.

Screenshot_20220119-094738_Facebook.jpg
 
View attachment 2087631
Samuel L. Jackson ni ndugu yako?
 
Mtu aliyeniingiza Bush House London alikuwa Ahmed Rajab mwaka wa 1991 na kule kuisikia BBC radioni kukageuka kuiona BBC yenyewe ikitangaza mubashara na mimi nikapata fursa ya kufanya kipindi cha ''majaribio'' kutoka studio za BBC Glasgow, Scotland.

Hiki ni kisa kirefu Insha Allah iko siku nitakieleza lakini muhimu ni kuwa magwiji wa utanganzaji kama Aisha Yahya na Chama Omari Mtata waliponisikia wakaniambia kuwa ninacho kipaji cha kuwa mtangazaji.
Ahsante kwa uzi maridhawa kabisa mzee wetu Mo.

Fanya hima kutuletea hiko kisa tafadhali.
 
Zuhura si tu miongoni mwa wanawake wanaonivutia kwa haiba na silka yake
Bali ni mwanamke anaenivutia zaidi kwenye tasnia ya habari kuliko mwingineyo
Huyu si tu mwanamke bali ni mwanamke na nusu.
 
Aaaa Mzee Said...
Ulikuwa unajua yajayo na kutupa wasifu wa mteule kabla hayawi hayawi ..
Haya wasije kukupopoa mawe kuwa list yote ya Wa BBC tokea enzi na enzi ni dini fulani....
 
Tek...
Nilisoma mtandaoni kuwa Bi. Zuhra anaondoka BBC nikahisi kuna kazi kubwa kapata.

Sasa kwa kuwa ni dada yangu mdogo nikaona hebu nimwandike.
 
Back
Top Bottom