Je, mtandao wa Smile umefunga virago Tanzania?

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,028
Network haipatikani.

Website yao haifunguki.

Simu hawapokei.

Page zao za facebook na insta zipo kimya tangu october.

Kuna waliolipia vifurushi vya mwezi, siku zinaenda tu na hua hawafidii vifurushi network ikikata.
 
Uzungu unawacost sana smile. Kuna style flani wanalazimisha waonekane ni premier wakati soko la sasa watu wanapenda ofa na bwerere.

Nawaza kama tigo isingepambana kipindi kile cha longa longa, chombeza, etc kiasi kwamba mtu anaongea bure masaa 12 kuanzia sa12 jioni hakika wasingetoboa. Walijitoa ufahamu wakachoma pesa nyingi sana tigo kupata nafasi waliyopo sasa.

Kama isingekuwa vile mobitel ingekuwa historia kwasasa. Smile nao walipaswa wapambane upande wa data wangepiga ofa za uhakika miezi sita ama mwaka hakika kwa watu wanavyopenda kuwa mitandaoni kila mtu angekuwa na simcard ya smile.
 
Uzungu unawacost sana smile. Kuna style flani wanalazimisha waonekane ni premier wakati soko la sasa watu wanapenda ofa na bwerere....
Umeongea bro.

Nakumbuka mwaka 2017 nilinunua laini yao kwa elf 24 yani basi tu sikuwa na namna, siku hizi naskia wanauza elf 6, yani wanafanya biashara kwa kujiona wao ni premium flan hivi wakati wenzao usajili ni buku tu.

Kitengo cha masoko naona kimelala sana, yani hakuna walichofanya kuonesha juhudi ya kusaka wateja wapya, yani sijawahi kuona hata gari ya matangazo inazunguka inatangaza mtandao wao, hata sijawai kuona wakifanya hizi events za burudani ili watu wakusanyike wajue uwepo wao.

Yani wapo wapo tu wanasubiri wafatwe.
 
Umeongea bro.

Nakumbuka mwaka 2017 nilinunua laini yao kwa elf 24 yani basi tu sikuwa na namna, siku hizi naskia wanauza elf 6, yani wanafanya biashara kwa kujiona wao ni premium flan hivi...
Sales persons wao wanapitaga maofisini na wanatafuta managers wa kampuni na wahasibu na mabosi wengine. Wao wateja wanataka kuanzia level ya supervisor kwenda juu sio chini ya hapo.

Bahati mbaya sana wamekuja na sera za voda na airtel za miaka ya 2000. Sera ambazo voda alizikacha airtel wakakomaa kidogo nao zikawashinda.

Saivi voda, tigo na airtel ndio wanaoshika tatu bora na wana ofa kibao ikitoka hii inakuja hii. I think smile hawakuwa na mtaji wa kutosha wa kuteketeza sokoni.
 
Sales persons wao wanapitaga maofisini na wanatafuta managers wa kampuni na wahasibu na mabosi wengine. Wao wateja wanataka kuanzia level ya supervisor kwenda juu sio chini ya hapo....
Ukishindwa kujiandaa jiandae kushindwa, hao jamaa naona strategically walikuwa sifuri, maana mtandoa huu naskia ulianza huko nigeria saizi wana matawi congo, uganda na tz...Yani hapo uganda kupata kifurushi cha siku ni gb 4 na ni elf 10 ya huku.

Naona wanalazimisha sera za huko nigeria wazitumie huku bongo na wamefeli, Mtandao kama halotel umeanza juzi juzi tu wakaenda na flow ya wabongo yani saizi mambo yao yako vizuri tu, watu wenye uchumi mdogo ni wengi na wanapendelea sana kutumia halotel kwa unafuu wa bei.

Hawa smile kiukweli internet yao ina kasi, wangecheza karata zao vizuri kwa flow ya kibongo saizi huu ungekuwa mtandao unaotumika sana na makampuni, vyuo, mashirika ya serikali, yani ungekuwa ni kama mtandao premium hivi
 
Uzungu unawacost sana smile. Kuna style flani wanalazimisha waonekane ni premier wakati soko la sasa watu wanapenda ofa na bwerere...
Ukishindwa kujiandaa jiandae kushindwa, hao jamaa naona strategically walikuwa sifuri, maana mtandoa huu naskia ulianza huko nigeria saizi wana matawi congo, uganda na tz...Yani hapo uganda kupata kifurushi cha siku ni gb 4 na ni elf 10 ya huku...
Nyie jamaa mnaona biashara ni mchezo mchezo tu?

-Vodacom part ya Vodafone kampuni papa Duniani lina MA asset mengi, matrilioni ya Hela, pato LA mwaka tu ni budget ya Nchi nzima ya miaka kadhaa

-Tigo nao Hivyo Hivyo kampuni kubwa stock kibao nje ya nchi, makumi ya trilioni wanaingiza,

-Halotel nayo ni Ttcl ya Vietnam, Wana serikali nzima ina wa backup

-then una smile kakampuni kadogo ambacho kameanzishwa kwa mikopo na ku raise funds mbalimbali.

Hao mapapa wanaweza ku afford kukupa ofa za kupiga Bure hadi kuche, Wana cash za kutosha hata ku operate miaka kadhaa kwa loss ilimradi tu baadae waje wapate faida

Smile Hana luxury hio ndio maana akatafuta niche yake, yeye ndio wa kwanza kuileta 4g Tanzania na pia wao Wana Vo-lte Hali ya kuwa mitandao mikubwa Hawana, walibase na maofisi na makampuni makubwa kuwapa hio service.

Sijui kilichowapata ni nini ila makampuni yanapofunga biashara automatic na wao biashara Yao ina anguka.
 
Nyie jamaa mnaona biashara ni mchezo mchezo tu?

-Vodacom part ya Vodafone kampuni papa Duniani lina MA asset mengi, matrilioni ya Hela, pato LA mwaka tu ni budget ya Nchi nzima ya miaka kadhaa...
Umenena kweli.

Ila wangeamua kubadili market strategy yao wangefuata watu wa hali ya chini huku wawateke.... Mtandao ukiamua kudeal na coorperate tu haya ndio matokeo.
 
Nyie jamaa mnaona biashara ni mchezo mchezo tu?

-Vodacom part ya Vodafone kampuni papa Duniani lina MA asset mengi, matrilioni ya Hela, pato LA mwaka tu ni budget ya Nchi nzima ya miaka kadhaa...
umenena vizuri mkuu

kiukweli tangu mwaka 2016 kampuni nyingi na biashara kibao zimefungwa, mifano ni kama fast jet na hotel kubwa ambazo zilikuwa zinatumia smile.

ila ilibidi wabadili strategy kuliko kudeal na strategy ile ile ambayo imepata pigo kubwa kulingana na macro environment ya soko
 
Nyie jamaa mnaona biashara ni mchezo mchezo tu?

-Vodacom part ya Vodafone kampuni papa Duniani lina MA asset mengi, matrilioni ya Hela, pato LA mwaka tu ni budget ya Nchi nzima ya miaka kadhaa....

Your last sentence ndipo walipochemsha. Ktk FMCG kuna masoko mawili lazima uyashike ipasavyo (Mass Market na Corporates Market).

Walikuwa wanauza bidhaa yenye sifa za FMCG wakatumia kanuni za kuuza magari. Wamechuma walichopanda.
 
Umenena kweli.
Ila wangeamua kubadili market strategy yao wangefuata watu wa hali ya chini huku wawateke.... Mtandao ukiamua kudeal na coorperate tu haya ndio matokeo.
better late than never, wangeanza mapema sana kubadili strategy kile kipindi na hata sasa tunavyoona biashara nyingi zinafungwa

ila smile wana speed aisee, yani nikitumiaga facebook kwenye laptop yani inafunguka fasta sana kuzidi mtandao wowote hapa tz
 
umenena vizuri mkuu

kiukweli tangu mwaka 2016 kampuni nyingi na biashara kibao zimefungwa, mifano ni kama fast jet na hotel kubwa ambazo zilikuwa zinatumia smile.

ila ilibidi wabadili strategy kuliko kudeal na strategy ile ile ambayo imepata pigo kubwa kulingana na macro environment ya soko
Hao jamaa msiwatetee huwezi uza Fast Moving Consumer Goods halafu ukabase tu kwenye corporate customers ukadharau mass market.

Unajua kwanini baresa hafilisiki? Mass market inamlinda na itamlinda milele. Mass market ndio mpango mzima.
 
better late than never, wangeanza mapema sana kubadili strategy kile kipindi na hata sasa tunavyoona biashara nyingi zinafungwa

ila smile wana speed aisee, yani nikitumiaga facebook kwenye laptop yani inafunguka fasta sana kuzidi mtandao wowote hapa tz
Kwa minara ipi? Ili waweze kuhudumia mass market wa nahitaji kueneza minara nchi nzima,

Kampuni kama Voda kwenye 4g tu 2011/12 Wali spend zaidi $100m kwa mwaka kujenga hizo base,

Smile Hawana huo mtaji, hela walizoraise ni kama $300m na wapo nchi kibao, Hawana uwezo wa ku cover nchi nzima na minara.
 
Hao jamaa msiwatetee huwezi uza Fast Moving Consumer Goods halafu ukabase tu kwenye corporate customers ukadharau mass market.

Unajua kwanini baresa hafilisiki? Mass market inamlinda na itamlinda milele. Mass market ndio mpango mzima.
Kuna kampuni ni b2b muda wote na zina nguvu sana, Japan wao makampuni Yao mengi yapo Hivyo yaliondoka consumer markets siku nyingi na yapo vizuri kupitia kiasi.

Bakhresa na Rostam Nani Ana hela Nyingi? Rostam anahangaika na mass Market?

Kama biashara unajua basi unajua tu bila kujali eneo.
 
Kuna kampuni ni b2b muda wote na zina nguvu sana, Japan wao makampuni Yao mengi yapo Hivyo yaliondoka consumer markets siku nyingi na yapo vizuri kupitia kiasi....
Rostam hayupo mass market? Acha kutuangusha mwamba.

Rostam anamiliki voda kwa over 15% na voda imejikita kwenye massmarket.

Pia ukiacha keyword ya FMCG basi umeikosa point yangu.

Anaefanya biashara ya FMCG halafu aka ignore mass market huyo kwishnei.

So nitajie biashara ya rostam inayodili na FMCG ambayo ime ignore mass market.
 
Umeongea bro.

Nakumbuka mwaka 2017 nilinunua laini yao kwa elf 24 yani basi tu sikuwa na namna, siku hizi naskia wanauza elf 6, yani wanafanya biashara kwa kujiona wao ni premium flan hivi wakati wenzao usajili ni buku tu...
Network coverage yao inafika nje mji kweli?
 
Nyie jamaa mnaona biashara ni mchezo mchezo tu?

-Vodacom part ya Vodafone kampuni papa Duniani lina MA asset mengi, matrilioni ya Hela, pato LA mwaka tu ni budget ya Nchi nzima ya miaka kadhaa...
Shida hao mapapa wezi wa data,voda kifurushi chao cha gb 10 kwa wiki kwa elfu 10 kinaisha ndani ya siku 2!
 
Back
Top Bottom