WISTON MWINUKA
Member
- Apr 29, 2012
- 81
- 4
Ndugu zangu wakati ulipofanyika mkutano wa CDM pale Jangwani wiki kadhaa zilizopita,niliandika maelezo yaliyohusu kichwa habari hapo juu,sababu ilikuwa ni kubwa tu kwani ITV walirusha Live mkutano wa CDM, na TBC hawakufanya hivyo!Leo eti TBC wanarusha Live mkutano wa CCM pale jangwani,na kwa siku kadhaa wamekuwa wakitangaza matangazo yanayohusiana na mkutano wa CCM pale jangwani.Swali,Je!ni haki kwa TBC ambacho ni chombo cha habari cha uma kupendelea katika urushaji matangazo ya mikutano ya kisiasa ya vyama?