SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 5,129
- 7,898
Wajuvi wa siasa na harakati za nje ya uwanja inapokuja mechi ya Simba na Yanga embu tuelimishane.
Wote tunakumbuka Clautus Chama alipotolewa katika mechi na Mbeya City alikwenda moja kwa moja vyumbani na baadae kurudi. Hii ikazua gumzo kubwa.
Siku kadhaa baadae mchezaji wa Yanga anayevaa jezi inayofanana na ya Chama, Farid Musa naye baada ya kutolewa katika mechi dhidi ya Ruvu Shooting naye alikwenda moja kwa moja vyumbani kabla ya baadae kurudi.
Kuna mdau mmoja nilisoma comment yake sehemu moja jana akasema "mchezo wa derby wa mwezi wa 4 umeshaanza kuchezwa". Ni kauli inayofikirisha sana. Tukumbuke kwenye game iliyopita ya Simba na Yanga, Chama na Aziz Ki walitegeana kuingia uwanjani na walikataa kupeana mikono, hali iliyopelekea timu zote mbili kutozwa fine na wachezaji hao kufungiwa mechi kadhaa.
Tueleweshane haya mambo yanafanyikaje. Tuelewashane pia, Yanga wanapokuwa wanakataa kutumia milango rasmi ya kuingilia uwanjani wanaepuka nini ambacho hakiwadhuru Simba. Hii technology inafanyaje kazi?