Al-Watan
JF-Expert Member
- Apr 16, 2009
- 11,891
- 14,601
Sasa tunaposema Marekani tuna maana gani?Marekani ni taifa kama yalivyo mataifa mengine, ila tofauti yake na haya mataifa mengine ni kwamba Marekani ni nchi ambayo raia wake wengi si watu wa asili wa eneo lile, wengi wa wamarekani asili yao ni UINGEREZA, AFRICA AND LATIN AMERICA NA WENGINE NI WAYAHUDI. Asili ya watu wa eneo lile ni RED INDIS. Halfu Marekani ndiyo super power wa hii dunia kwa saiv.
Tushaona Marekani sikitu kimoja.
Wao wenyewe wanapingana.
Sasa sisi tunaposema "Marekani hivi, Marekani vile" wakati Marekani yenyewe inajipinga vibaya sana, maana yetu ni nini?
Hata ukichukulia uongozi wa juu wa serikali.
Ukiangalia tu safari ya Donald Trump Saudi Arabia unaweza kuona msimamo wa nchi hii ulivyobadilika katika muda mfupi tu kutokautawala wa Obama mpaka sasa kuhusu Saudi Arabia na siasa nzima za Mashariki ya kati.
Sasa nchi ambayo inaweza kubadilika badilika hivi unawezaje kusema ikohivi au vile?