Sokoro waito
JF-Expert Member
- Nov 21, 2014
- 2,201
- 2,587
heko kwenu wadau wa hili jukwaa la wachache,
Mimi binafsi huwa natumia spiritual intelligence kuweza kutambua kama niko salama, nitakuwa salama kesho au kuna jambo baya laweza nitokea baadae ama likamtokea ndugu yangu wa karibu au rafiki pia. Hata hivyo kuna mengine huwa siwezi yaona katika ulimwengu wa kiroho maana Mola hunionyesha anachotaka nijue, asichotaka hunishitukiza tu na kutokea ghafla.
Ninaposema spiritual intelligence namaanisha 'UJUZI WA MAMBO YA KIROHO' yaani mambo yasiyoonekana kwa macho ya kawaida ila yapo na huenda yakakutokea hata leo au kesho.
jambo hili limekaa kiimani lakini bado linabaki lenye maana na umuhimu mkubwa sana kwa ulinzi wa mtu yeyote yule.
wale wasomaji wa biblia na wanaoamini katika biblia au imani nyingine watakuwa wanaelewa ninachozungumza hapa, kwasababu kwenye biblia kuna mifano kadhaa inaelezea jambo hili kwa ufasaha zaidi,
mfano wa kwanza ni Yusufu wa kitabu cha mwanzo yaani mwana wa yakobo alionyeshwa ndoto iliyoonesha baba yake na wakubwa zake wanamuinamia, alipoisema ndoto hii wakubwa zake walimchukia na kumkebehi lakini baada ya miaka kadhaa baadae walikuja kumsujudia yusufu kule nchini misri wakati alipokuwa waziri wa chakula na baadaye waziri mkuu.
mfano wa pili ni ikulu ya farao katika kitabu cha mwanzo inaonyesha kuwa ilikuwa na wataalamu wa mambo ya kiroho kwa imani ya farao au ya kimisri, kwa mfano ikulu ilikuwa na waganga, wasihiri na wengineo ambao walitumika kumlinda farao dhidi ya adui zake wa kipindi hicho.
lakini mbali na hilo kuna watu kadhaa katika dunia hii wamewahi kuota au kuona kuwa kama siku fulani wangesafiri bhasi wangepata ajali na kufa au kuumia, walipoahirisha kusafiri ajali ilitokea na ikaua watu kama alivyoota au kuona katika maono.
wengine hawaoti wala kuona maono lakini nafsi zao huwazuia kabisa kufanya kitu fulani iwapo tu kitawaletea hatari fulani katika maisha.
Najiuliza tu hivi ikulu kuna wataalamu wa haya mambo ya kiroho ili kuipambanua kesho ya nchi fulani/mtawala au kiongozi fulani katika ulinzi na mengineyo?
UPDATES:
Angalizo: Uwezo wa kiroho niliouzungumzia hapa ni ule wa pande mbili tu, yaani uweza wa MUNGU MUUMBAJI na uwezo wa Ibilisi. Wapo watu wanalindwa na MUNGU MUUMBAJI kwa kuonyeshwa maono au kuota ndoto zenye kuwaelekeza namna ya kuepuka mambo yanayoweza kuwadhuru sasa au baadae.
huenda pia wakawepo watu wanaolindwa na Ibilisi kama alivyokuwa farao wa misri ya kipindi hicho.
chonde chonde kama hujui chochote kuhusu mada hii ya spiritual intelligence pita pembeni tu au usome kimya kimya bila kukomenti utoto.
karibuni wajuzi.