Je, Marais/Ikulu zina walinzi wenye vipawa vya spiritual intelligence?

heko kwenu wadau wa hili jukwaa la wachache,

Mimi binafsi huwa natumia spiritual intelligence kuweza kutambua kama niko salama, nitakuwa salama kesho au kuna jambo baya laweza nitokea baadae ama likamtokea ndugu yangu wa karibu au rafiki pia. Hata hivyo kuna mengine huwa siwezi yaona katika ulimwengu wa kiroho maana Mola hunionyesha anachotaka nijue, asichotaka hunishitukiza tu na kutokea ghafla.

Ninaposema spiritual intelligence namaanisha 'UJUZI WA MAMBO YA KIROHO' yaani mambo yasiyoonekana kwa macho ya kawaida ila yapo na huenda yakakutokea hata leo au kesho.

jambo hili limekaa kiimani lakini bado linabaki lenye maana na umuhimu mkubwa sana kwa ulinzi wa mtu yeyote yule.

wale wasomaji wa biblia na wanaoamini katika biblia au imani nyingine watakuwa wanaelewa ninachozungumza hapa, kwasababu kwenye biblia kuna mifano kadhaa inaelezea jambo hili kwa ufasaha zaidi,

mfano wa kwanza ni Yusufu wa kitabu cha mwanzo yaani mwana wa yakobo alionyeshwa ndoto iliyoonesha baba yake na wakubwa zake wanamuinamia, alipoisema ndoto hii wakubwa zake walimchukia na kumkebehi lakini baada ya miaka kadhaa baadae walikuja kumsujudia yusufu kule nchini misri wakati alipokuwa waziri wa chakula na baadaye waziri mkuu.

mfano wa pili ni ikulu ya farao katika kitabu cha mwanzo inaonyesha kuwa ilikuwa na wataalamu wa mambo ya kiroho kwa imani ya farao au ya kimisri, kwa mfano ikulu ilikuwa na waganga, wasihiri na wengineo ambao walitumika kumlinda farao dhidi ya adui zake wa kipindi hicho.

lakini mbali na hilo kuna watu kadhaa katika dunia hii wamewahi kuota au kuona kuwa kama siku fulani wangesafiri bhasi wangepata ajali na kufa au kuumia, walipoahirisha kusafiri ajali ilitokea na ikaua watu kama alivyoota au kuona katika maono.

wengine hawaoti wala kuona maono lakini nafsi zao huwazuia kabisa kufanya kitu fulani iwapo tu kitawaletea hatari fulani katika maisha.

Najiuliza tu hivi ikulu kuna wataalamu wa haya mambo ya kiroho ili kuipambanua kesho ya nchi fulani/mtawala au kiongozi fulani katika ulinzi na mengineyo?

karibuni wajuzi.
Akili hizi ni moja ya sababu Waafrika hatuwezi kutawala Dunia.
 
Walinzi wengi wanapata training za kijeshi kwanza ili waive, halafu baadaye "wanapikwa kiroho".

Hapo ndipo kuna michezo yote michafu ya kiroho ikiwemo wizi wa nyota, kivuli, kumchomoa mtu na kuweka kitu ingine ndani ili "aive kiroho"

Kwa hiyo si lazima awe na spiritual intelligence tangu kuzaliwa ila anaweza kupewa spiritual intelligence na wabobezi wa sarakasi za rohoni...

Ni kana ilivyo kwa utajiri, sio lazima uwe uwe na kipawa cha kuumbwa tajiri ili uwe tajiri, ila unaweza kujifunza maarifa ya kuwa tajiri halafu ukawafuata wazee wa sarakasi za rohoni "wakakusafishia njia zaidi"

Huko kwenye kitengo, kuna kitengo maalumu cha Kiroho.
 
Salute mkuu Sokoro..
Umeeleza vizuri sana lakini hapo kwenye watu wa farao umeharibu kidogo. Unajua kunatofauti kati ya Uchawi/Uganga na matumizi ya Nguvu za kiroho/Power within. Kiukweli wale wa misri walikua ni waganga,wanajimu na wapiga ramli. Walichokua wanakifanya kilikua kinyume na Mungu. Mkuu unajua pia matumizi ya hayo mnayoita kua ni Mambo ya kiroho pia ni kinyume na Mungu..? Waliotufundisha taaluma hiyo ni wale malaika waaasi 200. Wewe destiny yako anayeijua ni Mungu wako (If u believe ni God) kwanini usumbuke kutaka kujua kesho itakuaje? Kula kwako, usalama wako,kuishi kwako n.k kupo mikononi mwa Mungu acha kuisumbukia kesho Anaijua Mungu.
lkn pia Mungu aliwatumia manabii katika kuwapa muongozo wafalme wa enzi za kale japo sio wote waliokuwa wanafanya na kufata maneno ya unabii, rejea kwa Eli/Samuel kwa mfalme wa kwanza wa waIsrael "Sauli" hadi anguko lake na kuinuliwa mfalme "Daudi".

kwa dunia ya sasa tunaona hawa watu "spiritual intelligence" kama alivyowaita mleta mada hawapo au wapo lkn sio kwa mapenzi ya Mungu bali kwa mapenzi ya viongozi na hawa ndio tunaweza kuwaita "waganga/wachawi"

na hawa wanaojiita manabii wanajidhihirisha uFake wao kutokana na unabii wao kutotimia...

mimi upande wangu naweza kusema inawezekana Mungu ameacha kuambatana na hawa viongozi wa sasa kwa maana wamejichagulia njia zao wenyewe...

(tukizungumza mambo ya kiroho lazima kuwe na pande mbili either upande wa MUNGU ambae ndio mkuu, au upande wa Shetani.)
 
Ushauri wa kiroho kutoka kwa Mungu wa kweli Rais anatakiwa kusugua goti na kuomba Mungu ataupata tu, uko mwingi. Maandiko yanasema, "Tafuteni mtapata, bisheni mtafunguliwa." Hata humu jF washauri tupo wengi tu.

ni kweli, je kuna raisi ambaye yupo tayari kusugua goti kwaajili ya MUNGU ktk karne hii?
 
ni kweli, je kuna raisi ambaye yupo tayari kusugua goti kwaajili ya MUNGU ktk karne hii?

Mh JPM kila siku si anatuhimiza kumuweka Mungu kwanza kabla ya vitu vyote. Mungu kwanza maana yake ni pamoja na yeye kusugua goti. Na nimeshaona picha kadhaa akiwa kanisani kapiga magoti. Lakini sisi wengine tuna muombea kila uchao kuwa aiongoze nchi hii akiwa na hofu ya Mungu na kutafuta muongozo wa hekima, busara na maarafi kutoka kwa Mungu mwenyewe.

Tunafanya hivi maana tunajua maamuzi yake yatatugusa tu kwa njia moja ama nyingine.
 
Amen to that
 
mkuu kuwa wa kiroho ni tofauti na kwenda kanisani, being spiritual is totally different from being a church goer.
 
Unaweza Kujua Kinachotokea Kesho? Kwako Au Kwa Ndugu Yako?

Kupitia Kuzama Rohoni?

Unajua Kesho? Kweli Mleta Mada?

Cc Da'Vinci

umesoma vizuri nilichoandika kweli, acha kukariri mambo, kwangu mimi kuna mambo MOLA hunionyesha kuhusu kesho yangu na kuna mengine hanionyeshi maana yeye anafanya hivyo kama apendavyo, hicho ndicho nilichoandika mwanzoni mwa thread yangu.

halafu nikwambie mkuu, siyo kila mtu anaelewa haya mambo ya kiroho, kama hujui kitu unapita kimya.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom