Je, makaa ya mawe yanafaa kupikia Katika majiko ya majumbani kama mkaa wa kawaida unavyotumika?

Rabbon

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2022
Posts
25,938
Reaction score
41,098
Salaam!

Nimepenyezewa taarifa tokea Dodoma kuwa,

Wapo baadhi ya wanakijiji yanapopita marori yaliyobeba makaa ya mawe, wananchi Hawa hukaa Pembeni mwa barabara na kusubiri baadhi ya makaa ya mawe yadondokke kutoka Katika haya malori ya kubebea makaa ya mawe na kwenda kuyatumia makaa haya kupikia Katika majiko ya mkaa ya kawaida na wanadai makaa haya ni Bora sana, unapikia hayaishi.

Swali no 1:
Je ni kweli makaa ya mawe yafaa kwa matumizi ya majumbani?

Swali no 2.

Yepi ni madhara ya kiafya kutumia makaa ya mawe kupikia kwa matumizi ya majumbani?

Swali No 3.

Upi uhusiano wa rostam kumiiliki mgodi wa makaa ya mawe akiyapeleka nje hapo hapo akiingiza gesi kuwauzia watanzania?
 
Toa sababu za kitaalamu.

Swali gumu lisipewe majibu mepesi.

Wananchi Dodoma baadhi wanapikia,

Na ikiwa yanafaa, kwanini rostam aende kuyahodhi,

Je ana mpango wa kuja kuyauza nchini baadae ?
Huo mkaa unawaka kama petroli
 
Inahitaji sufuria Zito sana. Mwaka 2021 niliwahi kupata nusu debe la huo mkaa, masufuria yalitobolewa sana. Moto ule una nguvu sana sana. Bonge Moja ukiliwasha unaweza kupika maharage hata mara Tano bado moto mkali.
Yana madhara yoyote kiafya?

Kama hakuna madhara, sufuria SI tatizo,

Tuyatumie kuepukana na Kuni na mazingira
 
Salaam!

Nimepenyezewa taarifa tokea Dodoma kuwa,

Wapo baadhi ya wanakijiji yanapopita marori yaliyobeba makaa ya mawe, wananchi Hawa hukaa Pembeni mwa barabara na kusubiri baadhi ya makaa ya mawe yadondokke kutoka Katika haya malori ya kubebea makaa ya mawe na kwenda kuyatumia makaa haya kupikia Katika majiko ya mkaa ya kawaida na wanadai makaa haya ni Bora sana, unapikia hayaishi.

Swali no 1:
Je ni kweli makaa ya mawe yafaa kwa matumizi ya majumbani?

Swali no 2.

Yepi ni madhara ya kiafya kutumia makaa ya mawe kupikia kwa matumizi ya majumbani?

Swali No 3.

Upi uhusiano wa rostam kumiiliki mgodi wa makaa ya mawe akiyapeleka nje hapo hapo akiingiza gesi kuwauzia watanzania?
Majibu:

1. Ndiyo yanafaa lakini ni vema yakasafishwa na maji kuondoa sulphur. Kinachotakiwa ni kuyaponda ponda yawe vipande vidogo, safisha na maji kuondoa sulphur, anika kukausha maji na kisha changanya na mkaa wa kawaida, washa moto na endelea kutumia.

2. Madhara ni yale yale ya kutumia mkaa wa kuni.

3. Hakuna uhusiano kwani Rostam Aziz ni mwekezaji kama wawekezaji wengine. Tofauti tu ni kuwa Rostam Aziz ni fisadi aliyekubuhu nchi hii na amekuwa akitumiwa na viongozi wa serikali na CCM kuhujumu uchumi wa nchi! Hata huo mgodi ameuziwa kwa bei ya chee hivyo kuikosesha serikali na nchi kwa ujumla mapato makubwa ambayo yangepatikana!

Kuhusu mradi wake wa gesi, hakuna uhusiano na mkaa wa mawe!
 
Je ni kweli makaa ya mawe yafaa kwa matumizi ya majumbani?
Kwa hisani ya Chatgpt

Ndiyo, makaa ya mawe yanaweza kutumika majumbani, lakini matumizi yake yana faida na changamoto zake. Hebu tuangalie kwa undani:

✅ Faida za makaa ya mawe kwa matumizi ya majumbani​

  1. Chanzo cha nishati chenye nguvu – yanatoa joto la muda mrefu zaidi ukilinganisha na kuni au mkaa wa miti.
  2. Yanapatikana kwa wingi – katika maeneo yenye migodi (kama Njombe, Mbeya – Tanzania), makaa ya mawe yanapatikana kwa urahisi.
  3. Hudumu muda mrefu – ukitumia kupikia au kupasha joto, hayaishe haraka kama kuni.
  4. Bei nafuu – katika baadhi ya maeneo, ni nafuu kuliko gesi au umeme.

❌ Changamoto na madhara ya makaa ya mawe majumbani​

  1. Moshi na gesi hatarishi – makaa ya mawe yakichomwa hutoa gesi kama kaboni monoksidi (CO) na dioksidi ya sulfuri (SO₂) ambazo ni hatari kwa afya, hasa yakitumika sehemu zisizo na hewa ya kutosha.
  2. Uchafuzi wa mazingira – gesi na vumbi vinavyotokana na makaa ya mawe vinaathiri hewa na kuchangia uharibifu wa mazingira.
  3. Hatari ya kiafya – matumizi ya muda mrefu majumbani yanaweza kusababisha matatizo ya mapafu, kikohozi sugu, na matatizo ya moyo.
  4. Kuchafua vyombo na nyumba – moshi wake unaacha masizi (vumbi jeusi) ambavyo huvutia uchafu.

🔑 Hitimisho​

  • Ndiyo, yanafaa kutumika majumbani hasa kwa kupikia au kupasha moto lakini ni salama zaidi yakitumiwa nje au sehemu yenye hewa ya kutosha (ventilation).
  • Kama kuna uwezekano, kutumia gesi, umeme au mkaa wa miti ni salama zaidi kiafya na kimazingira.
  • Serikali na wataalam wa nishati wanashauri kupunguza matumizi ya makaa ya mawe majumbani ili kulinda afya na mazingira.
 
Hii nchi kweli inahitaji reform kwanzia ngazi ya chekechea
 
Kumbe pakiwa na mazingira yenye hewa ,unapikia sio!

Watu wa kuchoma chips nadhani wameanza hii
 
Siyo kweli kwa sababu radioactivity ya material haitegemei moto, ipo tu kiasili (naturally). Kwa hiyo hayo madhara yangewakumba zaidi wanaochimba na siyo wanaotumia!
Kumbe yawezekana kutumika majumbani?

Ikiwa bibi zetu walipikia Kuni wakawa na red eyes, vipi madhara ya makaa ya mawe?

Mimi nashauri, wasomi wafanye utafiti hasa VETA, waje na njia Bora kuweza kuingia nishati hii Bora kwa matumizi ya majumbani.
 
Back
Top Bottom