Ipo wilaya ya Liwale mkoa wa Lindi, kuna mjomba angu mmoja alinisimulia aliwahi kwenda kwa shida zake sasa ikawa njianj akikutana na watu wakumuuliza unaenda wapi? Anajibu "tunaenda kusikiliza uongo wao kwa hawa jamaa"(anamaanisha huko Ngende kwa waganga yaani ni waongo hawaamini ila anakwenda kujaribu) Sasa alipofika akaulizwa umekuja kufanya nini huku na wakati sisi ni waongo? Ikabidi awe mpole na kuomba radhi akaambiwa usiniombe mimi kamuombe yule pale anaoneshwa chatu mmoja mkubwa sana kama Anaconda akawekewa unga kiganjani akamlambishe ndio msamaha. Sasa Anko akifikiria maneno aliyoyasema njiani na huyo jamaa wakuombwa radhi jinsi alivyo ule unga wa kiganjani atashiba kweli au ndio atakuwa yeye mwenyewe ni msosi?



.
Ila ni sehemu maarufu kwa kusini inasadikia kwa kutoa utajiri na mambo mengine mengi ya kishirikina.
Sent using
Jamii Forums mobile app