Je mafunzo ya 'kitchen party' yanasaidia?

Kimbori

JF-Expert Member
Feb 21, 2012
5,458
3,206
Naomba tujadiliane juu ya haya mafunzo dada zetu wanayopewa siku kadhaa kabla ya ndoa, hususani huku mijini.
Je mafunzo hayo yanayotolewa kwa masaa kadhaa yanakidhi changamoto za ndoa? Kama kuna mama au dada au mtu yeyote yule aliyefanikiwa kupata mafunzo haya au mwenye uelewa hususani maeneo ya mijini naomba atujuze faida zake, na nini kifanyike ili yawe chachu ya kuimarisha ndoa.
MTAZAMO WANGU: mafunzo hayo (yanayotolewa mijini) yapo chini ya kiwango kwa kuwa yanatolewa kibiashara, yafafuati maadili ya Kitasnzania, mchango wake hauonekani n.k. Naomba kuwakilisha
 
mafunzo ya nyumbani kwao mwanamke ndio yanasaidia haya mengine makelele tu
 
Mimi sina imani kabisa ya hayo mafunzo. Mafunzo yanayotolewa na wananwake mashangingi walioshindwa kulea ndoa zao, wanaofundisha huku wamelewa; wakidhalilisha utu wao, wanafundisha ngono tu, n.k. kuna jamaa yangu anaingia kupiga chabo kwa 'mwavuli' wa DJ alinisimulia na kunionyesha rekodi mmmm ni aibu tupu, hao wakufunzi hata hawajitambui, wanafundisha ngono tu, kwani kwenye ndoa ni ngono tu?
 
kitchen party ni sherehe ya kukusanya vyombo n not otherwise! me binafs hta si-support hili. . .
 
mi niko tofauti kidogo jamani kwanza kabisa mafunzo ya kitchen party sio kwamba eti ndio yatamsaidia huyo mwanamke moja kwa moja kwenda kuishi na mwanaume kwa tabia nzuri atakayoipata pale la hasha ila kitchen party ni kama kukumbusha tu majukumu yako kama mwanamke unaenda kuolewa kwa mafunzo mengi utakuwa umeyapata kupitia kwa mzazi wako au mlezi wako ulipokuwa unaishi pale ni kama final exam tu sasa basi tukija kwenye kitchen party za mjini kuna za aina mbili kuna zile za mashangingi na zile za kikirsto, kweli zile za mashangingi ukweli mtupu hazifundishi kabisa kwanza kwenye hizo sherehe huwezi amini baadhi yao wanaotoa mafunzo au mamc ni wanaume mashoga na wanawake wanaosasambua ni wahuni sana pia ni kama wako kibiashara ila kuna hizi za kidini ukweli hapo wanakukumbusha shangazi yangu huwa ni mtoa somo kwenye kitchen party sijui huwa wanaitwaje kitalaam ila ukweli kuanzia pale wanapoingia mpka mwisho ni mambo ya kwenye bible tu huwa yanatumika na mistari kwa kwenda mbele ndio inasomwa nilishawahi kucheki video yake ya hiyo sherehe ukweli unakumbushwa nini wajibu wako kama familia uliokulia katika malezi ya kidini. so wengi wao siku hizi wanafanya kitchen party kama njia ya kujipatia zawadi ila haina maana hiyo watu walishachange taste yake.
 
wote mmejibu vizuri na ni bora mkatuonyesh aasura ya pili ya hizi kitchen party. Ukweli ni kwamba mwali mdogo hufundwa kwa sehemu kubwa sana na makuzi ama malezi ya nyumbani kwao na jamii inayomzunguka. na tabia hizi binti akizipata humfanya akue akiziishi na wala hatutegemei aende kinyume nazo kwani ndivyo alivyozoea.

mwali huyu yapo maswala ya ndani kabisa(chumbani) ambayo mama yake hawez kumweleza wazi wazi kwa mila zetu za kiafrika so siku kama a week before mama humtafutia mwali kungwi wa kuja kumfunda ndani. Kungwi huyu huingia chumbani pamoja na somoye mwali na humo huongelewa yote ya chumabani na penine mwali hupewa majaribioa humo humo. baada ya mama mwali kuridhika basi yeye anakuwa amesa maliza kazi yake ya kumfunda mwali husika.

sharehe za kitchen party hizi huwa na lengo la kumjengea binti confidence na ni kama njia ya akina mam kumkaribisha mwali kwenye maisha ya umama na ya kuwa mke so hapa hakuna kubwa sana zaid ya akina mama kumpa experience ya maisha ya ndoa na kumpatia zawadi hasa vyombo kama sehemu ya kumfanya kuwa mama manake ni aibu sana bnti akaenda kwa mumewe pasi hata shuka na kikombe na ni kweli anaweza kujinunulia lakin zawadi inapendeza zaid manake inaonyesha ushirikiano wako na wenzio na pia inakufanya mwali kujifunza ushirika na akina mama wenzio.
 
kitchen pati ni kwa ajili ya kukusanya vyombo, halafu siku hizi wanafanya kibao kata kwa ajili ya kufunza kukatika.......
 
kama muolewaji hakuelewa dhana ya ndoa kwa mafunzo aliyopata katika malezi yake kwa miaka yote hakika hizo saa chache hazitamsaidia kuielewa ndoa.
 
yote tisa last saturday kuna mdada alifanyiwa kp wakat keshaish na hyo mwanaume over 3 years na wana mtoto et naye kenda fanyiwa kp. makubwa!

ndo ilivyo bi dada hapo anataka jiko la umeme, zulia na vyombo vya ndani tu tena vya udongo, kama kufundwa wala haitaji maana kashakomaa huyo
 
Back
Top Bottom