Je, Lissu anajijenga ili kugombea Urais 2020?

Je, Lissu anajijenga ili kugombea Urais 2020?

Kwani yeye haoni wivu kuzidiwa akili na lissu?
 
Kwani yeye haoni wivu kuzidiwa akili nA lissu?
Hapana, rais wala hahitaji kuonea wivu wananchi wake, bali kazi ya rais ni kutambua vipawa vya wananchi wake na kuvitumia vema kwa manufaa ya nchi yetu. Lissu anavipawa vya pekee. Rais Magufuli ampatie fursa issu ya kuisaidia nchi hii.
 
Lissu ni msomi kuliko Mtikila ila Mtikila alikuwa na Kipaji kuliko Lissu.
Mtikila alikuwa hana kundi leo anakuunga mkono kwa hili na kesho atakuponda kwa lile. Independent Person, Mtikila ana kundi na akizungumza anazungumza kama kundi
 
Lissu ni mwiba wa fisiem, hawawezi kumkubali hata siku moja
 
Ni matumaini yangu kuwa Mh. Rais au wasaidizi wake wataona uzi huu na kumfikishia ujumbe na kuufanyia kazi ili nchi isonge mbele.
 
Lissu ni mwiba wa fisiem, hawawezi kumkubali hata siku moja
Ni suala la kubadili fikra kuwa kila mwananchi bila kujali itikadi yake ya siasa, anaweza kutumika vizuri kuleta maendeleo nchini.
 
Nawaomba sana mjitathimini upya na muone kama bado Jamii ya kitanzania I inahitaji aina ya siasa mnazozifanya.

1. Mmekuwa mkihubiri kuhusu ufisadi kwa mila mingi na kuwataja kwa Majina. Cha ajabu mkageuka na kutueleza si mafisadi ni watu Safi.

2. Mmekuwa mkisema CCM hakipambani na ufisadi. Sasa Mhe Rais ameonyesha dhamira Safi ya kupambana na mafisadi. Sasa mmegeuka mnasema ni dikteta.

3. Mmekuwa mnasema nchi inaibiwa kwenye mikataba ya madini na wawekezaji. Mhe Rais ameamua kuivunja kwa kuikiuka. Bado mnasema hapana anakosea.

Bado sijawaelewa aina ya siasa mnazozifanya kama ni siasa Safi au Chafu.

Kama ni Safi basi mnipe mfano ni nchi ipi Duniani imefanikiwa kimaendeleo kwa aina hii ya siasa?

Kama haipo basi mjitafakari na muache siasa Chafu.

Magufuli kanyaga Twende mwendo mdundo.
 
Wanasiasa wa mtindo huu wametukadiria sisi watanzania na kutugeuza mazuzu. Ombi kwa watanzania wenzangu ni kwamba, tuachane na siasa za kikanjanja badala yake tuutetee uhalisia wa mambo. Rais Magufuli anaweza kutufikisha mahala pazuri kabisa ambapo hata sisi hatukutarajia. Kila mtanzania kwa nafasi yake afanye kazi kwa bidii na maarifa yake yote. Pia tuwe wavumilivu kidogo katika kipindi hiki cha mpito, kwani ukitaka kufanikiwa katika jambo lolote lile ni lazima kwanza uvuje jasho. Hatuwezi kuendelea kwa kupiga kelele zisizo na manufaa kwetu na kwa wananchi. MUNGU IBARIKI TANZANIA, MBARIKI RAIS WA JAMHURI YA
 
Huyo Malaika wenu ni kweli amefanya mazuri mengi tu hadi sasa, ila ana mapungufu vilevile. Cha ajabu amekuwa hataki kuambiwa wala kusikia mapungufu aliyonayo, yaani hataki kukosolewa. Hivi ni kiumbe gani ambaye atasifiwa tu pasi kukosolewa? Inafika mahali hata ameamua kuzuia mikutano ya hadhara ya vyama vya upinzani kwa hofu ya kumkosoa. Sasa unafikiri Lissu anafanya vibaya kumsema na kumkosoa kila mara? Watanzania wazalendo tunataka Lissu aendelee na utamaduni huo dhidi ya mkuu wa kaya ili pawe na uwezekano wa mkuu huyo wa kaya kubadili mwenendo. Go, go, Lissu watanzania tuko nyuma yako hadi madikt*t@ uchwara watakapokoma.
 
Wenzako wanagaiwa Magwangala bule we unahangaika na buku 7
 
Unaandikaa uzi mrefu unajaza server ya jf tu
 
Hivi nyie mnao mtete rais naomba leo mnifahamishe kitu !kwani huyo rais kuna uhusiano gani kati ya juhudi zake za kupambana na ufisadi na dhamira yake ya kukandamiza demokrasi?msijitoe ufahamu hapa hakuna mtu anayempinga rais kupambana na ufisadi ubadhirifu ukwepaji kodinrushwa na kadhalika ila ukweli nia na dhamira yake hiyo haimpi uhalali wa yeye kuwa ndio mdomo pekee macho pekee ,masikio pekee na akili pekee katika nchi hii!hana mamlaka hayo nchi inaend3shwa kwa sheria tulizokubaliana sio kwa hisia za mtu!
 
hakuna jambo baya kwa kiongozi kama kuvunja katiba aliyoapa kuilinda....
 
  • Thanks
Reactions: JGG
Kukamatwa kwa Lissu kunahusiana vipi na ufisadi?
 
Back
Top Bottom