Je, kwanini unadhani watu bado wanagoma kuchanja chanjo hii?

Swahili_Patriot

JF-Expert Member
Aug 22, 2018
231
413
Swala la chanjo ya kinga dhidi ya ugonjwa wa uviko unaosababishwa na kirusi hatari zaidi kwa sasa, bado halijakuwa na mwamko kama ilivyo kwa chanjo nyingine kama polio, bcg.

Je, kwanini unadhani watu bado wanagoma kuchanja chanjo hii?

Kama mwezi ulopita nilikutana n rafiki yangu wa muda, aliyenipa habari za msiba wa mtu niliyekuwa ninamfamu, dada flani alikuwa mlinzi wa kanisa nadhani ni PCEA makongo.

Kwa mtazamo wake, aliniambia wanaamini marehemu alifariki kutokana n chanjo ya corona.

Aliniambia kuwa, baada ya siku chache baada ya marehemu kuchanjwa, alianza kuugua hadi umauti kumkuta.

Hilo ni wazo lake. Kwa mlioichukua fursa ya kupata chanjo hii, ninaomba mtupe ufafanuzi kama hio chanjo ikekuwa na athari zozote kwenu.

Mliobaki wenzangu na mie ambao bado hatujachanjwa, mnalichukuliaje hili swala la kupata kinga n kwanini hadi sasa hamjaenda kupata chanjo?
 
Wengi mnasusia kisa vile vioja vya mwenda zake, aliwaamnisha vitu vya ajabu ajabu, mara corona imetoeka kwa maombi, mara ipo kwenye mapaipai mara mataputapu ya Madagascar, mara kujifukiza, mara ni ya mabeberu n.k.

Kiongozi wa nchi akiyumba yumba haeleweki msimamo wake, na wananchi pia wanayumba na kukosa muelekeo.

Ifahamike hii dunia hauwezi ukawa kila kitu wewe, mengine waachie wataalam husika washauri ipasavyo, wasklize wataalam wako na kuheshimu taaluma za watu. Unapoingia kwwenye mghahawa na kuagiza msosi, unaka mkao wa kutulia wafanye mapishi yao na kukupakulia, usiingie jikoni na kuanza kubishia kila wanachokifanya huko.

Hii chanjo ni kweli imeharakishwa na haikufuata hatua zote za kisayansi, ila inaeleweka corona ni gonjwa lililoshtukiza dunia na hapakua na muda wa kufuata taratibu zote hizo, ili kunusuru watu ilibidi chanjo ibuniwe upesi, na kawaida kitu kama hcho lazima kitakua na kasoro zake. Mimi hapa nimechanjwa Moderna, na yenyewe ina awamu mbili, ya mwanzo sikua na matatizo, nilichanjwa na maisha yakaendelea freshi tu, ila ya pili ilinipelekesha balaa, hata hivyo sikulaumu wala kujutia, niliendelea kupambana mpaka hali ikawa shwari na kuendelea na shughuli zangu.

Kwa kifupi, ni kweli inawezekana kunao wanachanjwa na kukumbana na athari zingine na ndio maana muhimu ukaeleza kuhusu afya yako ueleweke kabla kuchanjwa. Kwa mfano mke wangu hajachanjwa maana muda huu anaumwa, hivyo ni busara kusubiri kwanza apone.

Kingine mnapaswa kuelewa, chanjo haimanishi ndio sasa umepata kinga dhidi ya corona kwa asilimia 100%, bado kuna uwezekano unaweza ukaathirika ila inapunguza makali ya corona, ndio maana licha ya kuchanjwa, bado ninachukua tahadhari zote husika.
 
Weka ushahidi tafadhali, neno "wengi" unamaanisha nini?
Nina mtu namfahamu alipata dozi ya pfizer majuzi tuu walipolazimisha, ghafla amekuwa anapata matatizo ya moyo yasiyoeleweka. Hospitali wameshindwa kujua nini kinasababisha. Baada ya kumfanyia vipimo wakamuuliza kama amepata chanjo, alipowaambia, haraka ma dokta wakawasiliana na CDC.
 
Mimi nitakimbilia kwenda kuchanja iwapo wataalam wataniambia yafuatayo:

1. Sitalazimika kutumia barakoa.
2. Sitalazimika kukaa mbali na umati.
3. Sitalazimika kunawa kila wakati mpaka mikono inapauka.
4. Sitalazimika kuchanja kila inapokuja aina mpya ya kirusi.
Kwa ujumla nataka nione tofauti ya mtindo wa maisha, kati ya aliyechanja na ambaye hajachanja.
 
Nina mtu namfahamu alipata dozi ya pfizer majuzi tuu walipolazimisha, ghafla amekuwa anapata matatizo ya moyo yasiyoeleweka. Hospitali wameshindwa kujua nini kinasababisha. Baada ya kumfanyia vipimo wakamuuliza kama amepata chanjo, alipowaambia, haraka ma dokta wakawasiliana na CDC.
Huyo ni mtu mmoja tu au wawili ambao wanepata athari", Kuna mamilioni ya watu nyuma ya huyo unayemjua ambao wamefaidika na chanjo.

Ni sawa na kuhesabu jamaa au ndugu yako aliyekufa akiwa anatibiwa Hospitali, bado tunazidi kwenda Hospitali kwasababu wengi Kati ya wanaokwenda Hospitali wanapona, wachache Sana wanakufa.
 
Mimi nitakimbia kwenda kuchanja iwapo wataalam wataniambia yafuatayo:

1. Sitalazimika kutumia barakoa.
2. Sitalazimika kukaa mbali na umati.
3. Sitalazimika kunawa kila wakati mpaka mikono inapauka.
4. Sitalazimika kuchanja kila inapokuja aina mpya ya kirusi.
Kwa ujumla nataka nione tofauti ya mtindo wa maisha, kati ya aliyechanja na ambaye hajachanja.
 
Tumtangulize Mungu Mbele Tutashinda Hili Pepo
TUNATISHANA Sana Ndugu Zangu, Mara Vigogo Wafa, Vigogo Wapukutika Ni Uzushi Mtupu
By Mzilankende Mnyago
 
Nina mtu namfahamu alipata dozi ya pfizer majuzi tuu walipolazimisha, ghafla amekuwa anapata matatizo ya moyo yasiyoeleweka. Hospitali wameshindwa kujua nini kinasababisha. Baada ya kumfanyia vipimo wakamuuliza kama amepata chanjo, alipowaambia, haraka ma dokta wakawasiliana na CDC.
Haha Mambo bhana..... Ni hatari sana
 
Hivi yule Gwajima mzee wa porno na mauno yake, bado yupo, aliacha yale mabomu yake kila Jumapili alikua anahubiri dhidi ya chanjo.
Nakumbuka aliwahi kuwaahidi Watz atawapeleka Marekani sijui ilikua alipie gharama....hehehe hiyo nchi bana mnapenda masinema sana.
 
Endeleeni kupiga nyungu majirani. Acheni usaliti na unafiki, chanjo imetengenezwa kwa matumizi ya 'mabeberu' na vibaraka vyao. Kulikuwa na haja gani ya kumtukuza na kumsifia sana mtakatifu wenu? Hadi safari yake ilipoishia kuzimu, alafu eti baadaye ndio mnaanza kusita sita. Sio freshi hata kidogo.
 
Nonsense
 
Mkuu, fungua link hapo juu post #11, hili ni Jambo la kitaalamu Sana, unahitaji kuuliza wataalamu wa Afya katika eneo la chanjo wakupe majibu ya kitaalamu.

Kwa ufupi mkuu ni kwamba, hii chanjo imethibitishwa na wataalamu duniani kote Kama zilivyothibitishwa dawa na chanjo zote duniani, hata chanjo za Surua, Polio na zinginezo pia Zina madhara, lakini ni chini ya 2%, waliobaki yaani zaidi ya 95% wanafaidika
 
Endeleeni kupiga nyungu majirani. Acheni usaliti na unafiki, chanjo imetengenezwa kwa matumizi ya 'mabeberu' na vibaraka vyao. Kulikuwa na haja gani ya kumtukuza na kumsifia sana mtakatifu wenu? Hadi safari yake ilipoishia kuzimu, alafu eti baadaye ndio mnaanza kusita sita. Sio freshi hata kidogo.

Hivi unakumbuka hili dubwana pale Muhimbili, sijui kama bado wanalitumia na vioja vyao

_117381410_4d6cae7c-62e8-439f-a607-e45d1661603d.jpg
 
Back
Top Bottom