Je kwa mwanamke ndoa ndiyo kila kitu?

uzi umeenda sana lkn naomba niseme japo kidogo..............

binafsi naamin ndoa sio kitu cha muhimu kwenye maisha ya binadamu manke ukikosa bado unaweza kuish kwa maana ya ukapumua na kula na kunywa.

lakin ndoa ni kitu kinachokamilisha maisha yako kwa maana ya kuwajibika kijamii zaid. mwanaume/mwanamke kama hajaweka nadhir ya useja basi ndoa hukamilisha maisha yake.

binafsi naipenda na napenda kuona mtu yuko kwenye ndoa yake, furaha yangu huzidi zaidi pale majukumu yanapoongezek zaidi
 
uzi umeenda sana lkn naomba niseme japo kidogo..............

binafsi naamin ndoa sio kitu cha muhimu kwenye maisha ya binadamu manke ukikosa bado unaweza kuish kwa maana ya ukapumua na kula na kunywa.

lakin ndoa ni kitu kinachokamilisha maisha yako kwa maana ya kuwajibika kijamii zaid. mwanaume/mwanamke kama hajaweka nadhir ya useja basi ndoa hukamilisha maisha yake.

binafsi naipenda na napenda kuona mtu yuko kwenye ndoa yake, furaha yangu huzidi zaidi pale majukumu yanapoongezek zaidi

Hebu teacher tueleze, maisha yako bila ndoa yangekuwaje?

Binafsi sijui bila bibi ningeishije...ila nisingekufa!
 
mother-daughter-pf.jpg


Katika makuzi yangu kama binti wa Kiafrika nimefunzwa mambo mengi kuhusu maisha na wajibu wangu kama mtoto wa kike.

Baada ya kuvunja ungo nilianza kuandaliwa kuwa mke mtarajiwa wa mwanaume nisiyemfahamu.

Nimefunzwa kupika, nimefunzwa usafi wangu wa mwili, nimefunzwa usafi wa nyumba, nimefunzwa kuvumilia maisha ya ndoa na nikaaminishwa kwamba mwanaume ndiye kichwa cha nyumba na nikafunzwa wajibu wangu katika kumtumikia, lakini pia nikafunzwa kupanga bajeti na kuweka akiba ili huyu mume ambaye ni kichwa cha nyumba akikwama kupata mkate wa kila siku kwa ajili ya familia niweze kumsaidia.

Kwa kifupi ni kwamba nilifunzwa mambo mengi lakini yote hayo yakiniaminisha kwamba siku isiyo na jina lazima nitaolewa na kuwa chini ya mwanaume ambaye atakuwa ndiye kila kitu kwangu.

Nakumbuka wakati fulani baada ya mama kuona mabinti ambao nalingana nao umri na wengine nikiwa nimewazidi umri wakiolewa pale mtaani mama alianza kunidodosa kama sijapata mtu kama wenzangu.

Lakini pia alijaribu kutumia misamiati mbalimbali na mafumbo lakini nilielewa kwamba alikuwa anamaanisha nisiwe mgumu sana kwa wanaume kwani sijui aliyevutiwa na mimi na anayetaka kunioa.

Nadhani alikuwa anataka kufikisha ujumbe kuwa umri unasonga na wenzangu wanaolewambona miye sisomeki?

Naamini si mimi peke yangu, ninayekabiliana na changamoto hizi za wazazi na jamii kwa ujumla.

Ukweli ni kwamba malezi ya mtoto wa kike yanamuandaa kuwa mke wa mtu, yanamuandaa kuolewa na yanamuaminisha kwamba ndoa ndiyo kila kitu.
Kinachosababisha watu waone ndoa kwa mtoto wa kike ni muhimu ni tabia ya baadhi ya wanawake wasimbe kuwa malaya na mara nyingine hadi kuiba waume wa wenzao.
 
Wazazi wangu walitaka nisome weee (hasa baba); hata kama nitazeekea nyumbani...

Lakini ndoa ilikuwa katika list ya malengo yangu humu duniani....nadhani ni mafundisho ya dini yamenijenga niamini hivyo...

Naelewa kwa mzazi muelewa anataka bint asome ili hata akiolewa asivunjwe miguu kisa utegemezi; ila huyu baba yangu ningemsikiliza nadhani ningekuwa home mpaka leo hii....

Jamani ndoa tamu...hata kama kuna wanaoteseka kwa nini iwe wewe? Kwa nini usiingie uogope kwa kuambiwa?

Na kama ni kuogopa risk ndoa ndio risk pekee duniani? Usipande ndege, usipande gari, usile baadhi ya vyakula.... USIWE na boyfried...( kwani hakuna tofauti na kuolewa zaidi ya ndoa ina baraka za Mungu na wazazi)

Life ni full of risk and uncertainity...na ndio raha yenyewe ya maisha; yangekuwa mstari yange bore...
 
Ni kweli si kila mtu ni ndoa material...kuna ma feminist hao akyanani ukimuoa utajutraaaa.....na wenyewe wanajijua wanakuwaga single au wanatafuta wanawake wenzao...


Wanakuwaga wakali hao...kuna dada mmoja huyo (mghana) nilikuwa natia naye story uwa niko makini sana na ninachozungumza lakini siku hiyo sijuhi niliteleza vipi; nikamuuliza 'kwani xxx kaolewa?' baada ya yeye kunambia ana mtoto...wacha anijie juu...'kwani kuzaa mpaka uoelwe!' yani kafura kabisa kusema nimemtukana...nkamwambia sumimasendeshita (samahani)....hapo tulikuwa tunamuongelea mtu mwingine si yeye (na yeye ana mtoto lakini)

Again, I wouldn't judge a woman who decides to be single ili aepukane na kero za ndoa, I will support her decision regardless.
 
yawezekana ni kweli kila mtu anaitaji kuolewa na kuoa je waowaji wapo na waolewaji wapo?? ndoa kama za siku izi ni fasheni tu ili kila mtu aonekane anapete mkononi au kuwa mr an mrs fulani. jamani kwa twakimu iliopo wanawake ni wengi kuzidi wanaume so kama basi kila mtu anataka kuolewa wanaume waowe wanawake zaidi ya mmoja au wanne ili kila mtu apitie izo stage wananazo sema watu wengine kwamba Kuzaliwa, Ndoa, na kifo mh. ila ndoa nyingi ni majina watu wanataka, pia mali na heshima kwamba wewe ni mke au mume wa mtu. ila tumesahau kuwa heshima ni mtu mwenyewe ulivyo. tuwafunze watoto wetu na tubadilikeni ndoa sio kila kitu maana mtu atakuwa anannyanyasika kisa yupo kwenye ndoa. je ukiishi peeke yako bila ndoa maana ni bora kuishi mwenyewe kuliko kuwa na ndoa ndoanoo ya majozi na kilio kila siku kisa mume au mke wa fulani na huku uko sawa na yule alie msimbe.

Alie sema kuzaa ovyo kwani kuolewa au kuoa ndio kuzaa?? mbona watu wapo kwenye ndoa hawana watoto ama wengine wameolewa au kuoa na wamezaa lakini kutunza watoto inakuwa tabu. kama unaweza kuzaa na kuwa single zaa na maisha yaendelee. ilo usizae ukizani ndio tiketi ya kufunga ndoa. kumbe ndio safari ya majozi inaanza. wanawake muwafunze watoto wenu ndoa sio kila kitu na kuwaombea ukubahatika kuolewa au kuoa shukuru Mungu ila ndio ivyo ndoa sio kila kitu wapenzi
 
mmmhhhhh! babu, mimi msimamo wangu kwenye haya makitu huwa yanajulikana. Ingawa sikatai kuwa ndoa si kila kitu kwa mwanamke. Tena naweza kushawishika kusema kuwa ndoa ndiyo kila kitu kwa mwanaume, maana nyie bila sisi hamu-survive.

Sikuwezi wewe. Kwa kuhamisha magoli huna mpinzani.

Kwa nini isiwe kwa wote ?
 
Sikuwezi wewe. Kwa kuhamisha magoli huna mpinzani.

Kwa nini isiwe kwa wote ?
angalia kapo nyingi ambazo baba akitangulia mbele za haki, mama anaweza ku-survive miaka mingi iwezekanavyo bila kuolewa tena. Ila akitangulia mama, baba inabidi aoe faster ili aishi muda mrefu, asipooa tu hachukui miaka mingi ana-RIP.
 
angalia kapo nyingi ambazo baba akitangulia mbele za haki, mama anaweza ku-survive miaka mingi iwezekanavyo bila kuolewa tena. Ila akitangulia mama, baba inabidi aoe faster ili aishi muda mrefu, asipooa tu hachukui miaka mingi ana-RIP.


Hahahahahahahahha,

Wanaume tuna mambo yetu bwana, we tuache tulivyo.

Ila kuna ukweli kuhusu hilo...
 
Zinduna,

Ndoa siyo kila kitu kwa wote (mwanamume na mwanamke) ila ni kitu muhimu sana katika maisha ya kila mtu. Ukiacha watu ambao wameamua kuishi kiseja (matowashi), ndoa ni sehemu ya kukamilisha mzunguko wa maisha yetu hapa dunia.

Ni kwel mpendwa, ila baadhi hawajafahamu ndoa ni nn na kumbuka elim zaidi juu ya ndoa inatakiwa.
 
Last edited by a moderator:
Ni kwel mpendwa, ila baadhi hawajafahamu ndoa ni nn na kumbuka elim zaidi juu ya ndoa inatakiwa.


Na bahati mbaya tunakuwa kama "Mwamba ngoma...."

Bila kuchukua nafasi ya kati na kuielewa kila hali, tutabaki kutambiana na kutishana tu!
 
Ukiona mtu anakuwa mkali sana kuhusu kitu alichokifanya, jua deep down anajua ni wrong. Anajaribu kujihami ili asiulizwe na kujisikia vibaya. Mtu ambaye haoni shida, wala hajali ukimuuliza.

Ujue kuna baadhi wanaponda wanawake walioolewa lakini na wao wanatamani? Ni kwamba tu hajapata aina anayoitaka.
Kuna mdada nafanya naye kazi, alikuwa anamponda mate mwenzetu kaolewa na marioo, anasema sasa marioo huyo atampa nini? Lakini anasahau yule dada kifedha yuko vizuri, so kwenye mapenzi yeye hatafuti unafuu wa maisha, ana hausi yake, viusafiri vya kutosha na miradi kadhaa.

Akawa anasema, yeye anataka mwanamme anayeweza kumjengea nyumba, nikajisemea kichwani, utasubiri sana. Mwenyewe kapanga kiupande Kinondoni, socialisation yake uko ni ya watu wa aina hiyo hiyo, afu atake mwanamme mwenye fedha? Nikajisemea atazeeka peke yake, now she is 40.


Ni kweli si kila mtu ni ndoa material...kuna ma feminist hao akyanani ukimuoa utajutraaaa.....na wenyewe wanajijua wanakuwaga single au wanatafuta wanawake wenzao...


Wanakuwaga wakali hao
...kuna dada mmoja huyo (mghana) nilikuwa natia naye story uwa niko makini sana na ninachozungumza lakini siku hiyo sijuhi niliteleza vipi; nikamuuliza 'kwani xxx kaolewa?' baada ya yeye kunambia ana mtoto...wacha anijie juu...'kwani kuzaa mpaka uoelwe!' yani kafura kabisa kusema nimemtukana...nkamwambia sumimasendeshita (samahani)....hapo tulikuwa tunamuongelea mtu mwingine si yeye (na yeye ana mtoto lakini)
 
Naungana na miss chaga bora uishi mwenyewe kuliko kuolewa cku hizi hakuna waoaji ila Kama unataka waje wakuvue Pichu na kukuacha solemba wapo kibao so c kwamba kuolewa ndo kila ki2 kwa mwanamke miye nilipoona umri unakwenda na waoaji hawapo nilijizalia katoto kangu nakalea kwa raha zangu so usihuzunike Sana mama maisha bila kuolewa yanaenda sana
 
Back
Top Bottom