Je kwa mwanamke ndoa ndiyo kila kitu?

Zinduna

JF-Expert Member
Nov 6, 2011
2,379
1,500

Katika makuzi yangu kama binti wa Kiafrika nimefunzwa mambo mengi kuhusu maisha na wajibu wangu kama mtoto wa kike.

Baada ya kuvunja ungo nilianza kuandaliwa kuwa mke mtarajiwa wa mwanaume nisiyemfahamu.

Nimefunzwa kupika, nimefunzwa usafi wangu wa mwili, nimefunzwa usafi wa nyumba, nimefunzwa kuvumilia maisha ya ndoa na nikaaminishwa kwamba mwanaume ndiye kichwa cha nyumba na nikafunzwa wajibu wangu katika kumtumikia, lakini pia nikafunzwa kupanga bajeti na kuweka akiba ili huyu mume ambaye ni kichwa cha nyumba akikwama kupata mkate wa kila siku kwa ajili ya familia niweze kumsaidia.

Kwa kifupi ni kwamba nilifunzwa mambo mengi lakini yote hayo yakiniaminisha kwamba siku isiyo na jina lazima nitaolewa na kuwa chini ya mwanaume ambaye atakuwa ndiye kila kitu kwangu.

Nakumbuka wakati fulani baada ya mama kuona mabinti ambao nalingana nao umri na wengine nikiwa nimewazidi umri wakiolewa pale mtaani mama alianza kunidodosa kama sijapata mtu kama wenzangu.

Lakini pia alijaribu kutumia misamiati mbalimbali na mafumbo lakini nilielewa kwamba alikuwa anamaanisha nisiwe mgumu sana kwa wanaume kwani sijui aliyevutiwa na mimi na anayetaka kunioa.

Nadhani alikuwa anataka kufikisha ujumbe kuwa umri unasonga na wenzangu wanaolewambona miye sisomeki?

Naamini si mimi peke yangu, ninayekabiliana na changamoto hizi za wazazi na jamii kwa ujumla.

Ukweli ni kwamba malezi ya mtoto wa kike yanamuandaa kuwa mke wa mtu, yanamuandaa kuolewa na yanamuaminisha kwamba ndoa ndiyo kila kitu.Kwa nini nasema hivyo?

Ni kwa sababu kuna baadhi ya watu wanawaona wanawake wasioolewa kama vile wana kasoro au hawana thamani ukilinganisha na wale walioolewa na hii imetokana na jamii kuwapa heshima zaidi wanawake walioolewa na kuwadharau wanawake wasioolewa.

Si hivyo tu, lakini pia ndugu, marafiki na jamii huweza kumsakama mwanamke ambaye hajaolewa kwa maswali lukuki na hivyo kumjengea picha kuwa kutoolewa ni tatizo na hivyo kumfanya ajitilie mashaka na kushusha kiwango chake cha kujiamini. Jambo hili linawakwaza wanawake wengi amboa hawajapata waume wa kuolewa nao na kuyaona maisha bila kuolewa kama vile ni nuksi na wana kasoro. Hata hivyo pamoja na mtoto wa kike kufunzwa namna ya kuishi na mume na mafundisho mengine ya ndoa katika makuzi yake lakini hiyo haimhakikishii kwamba ni lazima atakapofikisha umri wa kuolewa, ataolewa.

Hivi wazazi wanapomuandaa mtoto wa kike kwa mafundisho ya ndoa unatarajia binti ambaye amefikisha umri wa kuolewa kwa mujibu wa jamii halafu akawa hajaolewa ataishi akiwa na furaha na amani moyoni?

Nadhani kuna haja ya ndugu, marafiki na jamii kwa ujumla kubadili mfumo wa malezi kwa watoto wa kike kuhusiana na swala zima la ndoa kwamba hata wasipoolewa haimaanishi kwamba wana kasoro ili ikitokea hawajapata wanaume wa kuwaoa waendelee kuyafurahia maisha wakiwa single na siyo kujuta na kuumia moyoni kwa kujihisi kama wana kasoro. Naamini wengi tunajua ni jinsi gani wanaume siku hizi walivyo wagumu kuoa na mazoea yametufundisha kwamba mwanamke ni wa kusubiri hadi atakapojitokeza mwanaume wa kumposa.

Nini kifanyike?

Kwanza jamii inapaswa kuzungumzia maisha ya kutoolewa au kuolewa kwa namna ambayo haitaathiri mitizamo ya watoto wa kike kwamba kuolewa ni ukamilifu kwa mtoto wa kike na kutoolewa ni nuksi na dalili kwamba mwanamke huyo ana kasoro au hana thamani. Tatizo ni kwamba wapo baadhi ya wanawake huzungumzia swala la kuolewa kwa namna ambayo inamfanya mtoto wa kike aone kama vile kutoolewa ni nuksi kabisa jambo ambalo si kweli.

Wanajenga dhana kwa mtoto wa kike kwamba haweza kuwa na furaha na amani kama hataolewa. Iwapo wanawake watajifunza na kuona kuna furaha na amani katika maisha ya aina yoyote, yaani maisha ya kuwa single na maisha ya ndoa naamini hakutakuwa na presha kwa wasichana wasioolewa kulazimisha kuolewa kwa namna yoyote hata kama hawajawapata wanaume wa ndoto zao.

Pili bibi zetu wanapaswa kubadilika na kuwafunza watoto wa kike watambue kwamba hata kama wasipoolewa thamani yao iko pale pale kama mwanamke na wanapaswa kuishi kwa furaha na amani na kujiamini kwa sababu hawana kasoro na furaha iko ndani mwao na si lazima ipateikane kwa kuolewa.

Mwisho wanawake wasioolewa wanapaswa wawe mfano kwa kuishi kwa kujiamini na kuyafurahia maisha na waache kulalamika kwa sababu wako single. Najua jambo hilo litakuwa gumu kwao kulikubali kwa sababu katika makuzi yao hawakupata kufundishwa kukubaliana na hali hiyo ya kuwa single na kuishi maisha ya furana na amani.
 
Zinduna

JF-Expert Member
Nov 6, 2011
2,379
1,500

Kwa nini nasema hivyo?

1,500Nini kifanyike?

Kaunga, Husninyo, MwanajamiiOne, Lisa, Neylu, Chocs, Nivea, Preta, Zion Daughter, charminglady, Elizabeth Dominic, snowhite, gfsonwin, Fixed Point, miss neddy, miss wa kinyaru, MankaM, Munkari, Heaven on Earth, Kongosho, AshaDii, King'asti, Tina, Ennie, sister, Sista, afrodenzi, Angel Msoffe, amu
 
miss chagga

JF-Expert Member
Jun 7, 2013
57,917
2,000
ni kweli kwa familia zetu za kiafrika wanaamini ndoa ndio kila kitu kwa binti na niheshima pia kwako na kwa familia nzima....... ila kwa upande wangu sioni kama ndoa ndo kila kitu zaidi naona kama ndoa ni zigo lisilobebeka likiwa na kila aina ya karaha ambazo hizo karaha unzikubali na kuzikaribisha mwenyewe kwa kukubali kuolewa kama ninakosea aisee akili yangu ipo kama imeathirika kidogo kuamini ndoa kama ni sehemu yenye furaha na amani
 
isha

Member
Dec 29, 2010
37
0
Thankfully i was not raised that way, instead my mum raised me to be a stable independent woman who would live her life happily whether married or not. Ila ulichokisema ni kweli kabisa haswaa kwenye jamii zetu za Kiafrika, watu wengi sana wamelelewa wakiamini kwamba ndoa ni moja wapo ya vitu vya ulazima vya maisha (i meant to say part & parcel of life). Ila kwangu mimi naamini kwamba "Marriage is not a rite of passage", you don't have to be married for your life to be complete. And this goes both ways, kwa wanawake na wanaume. Tatizo wanawake ndo wanakua more pressurized to get married and settle down tofauti na wanaume. Na nimeshaona cases nyingi sana ambapo mtu anaolewa kisa anaona mda unamtupa mkono ama her biological clock is ticking off and she needs to settle down and have babies, matokeo yake anajiingiza kwenye ndoa isiyokua na misingi bora which mostly leads to a broken marriage 5yrs down the line. Tunatakiwa tujifunze kwamba "our own happiness doesn't lie in being with someone else", learn to be your own best friend, love yourself and stop looking at life through rosy glasses, life is what you make of it. And if you find that special someone that you would like to settle down with and share the "forever after" with, then well and good! If you don't, well and good, bottom line here is, live your life to the fullest!!!
 
Ndeke afwege

Senior Member
May 20, 2014
154
0
ni kweli kwa familia zetu za kiafrika wanaamini ndoa ndio kila kitu kwa binti na niheshima pia kwako na kwa familia nzima....... ila kwa upande wangu sioni kama ndoa ndo kila kitu zaidi naona kama ndoa ni zigo lisilobebeka likiwa na kila aina ya karaha ambazo hizo karaha unzikubali na kuzikaribisha mwenyewe kwa kukubali kuolewa kama ninakosea aisee akili yangu ipo kama imeathirika kidogo kuamini ndoa kama ni sehemu yenye furaha na amani

umewahi kuolewa ukaona ni zigo? Usisikie wanayolalamika wenzako... Tambua ndoa ni sawa na choo:
kuna aliye ndani ya ndoa anataman kutoka kuna aliye ndani ya ndoa hataman hata kutoka wakat yule amabaye yupo nje ya ndoa anataman kuingi. Sawa na choo aliyemaliza haja zake anataka kutoka na yule anaeyendelea kutoa haja hana mpango wa kutoka na aliye na haja anataman kuingia
 
Heaven on Earth

JF-Expert Member
Mar 21, 2013
37,145

Aiseeeeeeeeee

I think my mom has a different perception towards marriage.........
 
miss chagga

JF-Expert Member
Jun 7, 2013
57,917
2,000
umewahi kuolewa ukaona ni zigo? Usisikie wanayolalamika wenzako... Tambua ndoa ni sawa na choo:
kuna aliye ndani ya ndoa anataman kutoka kuna aliye ndani ya ndoa hataman hata kutoka wakat yule amabaye yupo nje ya ndoa anataman kuingi. Sawa na choo aliyemaliza haja zake anataka kutoka na yule anaeyendelea kutoa haja hana mpango wa kutoka na aliye na haja anataman kuingia
mimi sijakuelewa kabisa yani ndo umanichefua zaidi... ndoa ni sawa na choo?
 
Ndibalema

JF-Expert Member
Apr 26, 2008
10,969
2,000
ni kweli kwa familia zetu za kiafrika wanaamini ndoa ndio kila kitu kwa binti na niheshima pia kwako na kwa familia nzima....... ila kwa upande wangu sioni kama ndoa ndo kila kitu zaidi naona kama ndoa ni zigo lisilobebeka likiwa na kila aina ya karaha ambazo hizo karaha unzikubali na kuzikaribisha mwenyewe kwa kukubali kuolewa kama ninakosea aisee akili yangu ipo kama imeathirika kidogo kuamini ndoa kama ni sehemu yenye furaha na amani
Thread hii itasaidia sana kufahamu wanawake waliotendwa, waliosota na umri kwend bila kuolewa na wanawake ambao sio wife material.
 
mito

JF-Expert Member
Jun 20, 2011
9,263
2,000
Wasichana wengi walioenda shule wanajitahidi kutokuzaa hovyo, shida kubwa ni kwa hawa shule-less, usipokuwa nao macho utaishia kurundikiwa tu wajukuu hapo home, na hiki ndo kikubwa wazee wetu wanajaribu kukikwepa
 
Kijana leo

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
2,863
1,225
ndoa ni heshima kubwa sana kwa familia, ndio maaana wazazi hufurahi pindi bitni/kijana akifunga ndoa, lakini ukichukuliwa take away wazazi wanaona umewakosea heshima na adabu au kujazwa mimba.
 
Eiyer

JF-Expert Member
Apr 17, 2011
28,268
2,000
Naweza kusema hivi;

Kimsingi ndoa ina umuhimu sana kwenye maisha ya binadamu isipokuwa wale wenye kazi maalum ambazo zinaweza kuwafarakanisha na wandani wao

Kimsingi kwa maisha haya ya sasa mwanamke kama hajaolewa kuna mawili,tabia yake sio nzuri au huenda hataki kuolewa

Hapo kwenye kutotaka kuolewa kunaweza kwa na sababu nyingi sana lakini ni vigumu sana kumkuta mwanamke ambae ni mzima kabisa halafu hana mtoto,hilo nalo ni tatizo lingine

Unaweza kujiuliza kama huyu ambae leo anasema hataki kuolewa na kwanini ana mtoto,bado na hapa napo kunaweza kuwa na sababu pia

Lakini kwa ujumla karibia wengi ni kuwa ni vigumu kumkuta anadai kuwa hataki kuolewa halafu awe hajishughulishi na masuala ya ngono,labda awe na tatizo

Kwa mtazamo huu ukitizama suala hili ni wazi tu kuwa inaweza kuwa hakuna ambae hataki mahusiano ya ndoa bali wapo ambao wameamua kuikana kwa hofu ya kutendwa tu lakini ndani mwao wanaitamani sana!
 
Eiyer

JF-Expert Member
Apr 17, 2011
28,268
2,000
Thankfully i was not raised that way, instead my mum raised me to be a stable independent woman who would live her life happily whether married or not. Ila ulichokisema ni kweli kabisa haswaa kwenye jamii zetu za Kiafrika, watu wengi sana wamelelewa wakiamini kwamba ndoa ni moja wapo ya vitu vya ulazima vya maisha (i meant to say part & parcel of life). Ila kwangu mimi naamini kwamba "Marriage is not a rite of passage", you don't have to be married for your life to be complete. And this goes both ways, kwa wanawake na wanaume. Tatizo wanawake ndo wanakua more pressurized to get married and settle down tofauti na wanaume. Na nimeshaona cases nyingi sana ambapo mtu anaolewa kisa anaona mda unamtupa mkono ama her biological clock is ticking off and she needs to settle down and have babies, matokeo yake anajiingiza kwenye ndoa isiyokua na misingi bora which mostly leads to a broken marriage 5yrs down the line. Tunatakiwa tujifunze kwamba "our own happiness doesn't lie in being with someone else", learn to be your own best friend, love yourself and stop looking at life through rosy glasses, life is what you make of it. And if you find that special someone that you would like to settle down with and share the "forever after" with, then well and good! If you don't, well and good, bottom line here is, live your life to the fullest!!!
Tunaweza kutengeneza hadithi nyingi sana za kujiliwaza lakini zinaweza kuwa kinyume na hali halisi

Unaweza kuwa hujalelewa kuitambua ndoa na umuhimu wake lakini ukiendelea kuishi utakuja kugundua kuna kitu hakiko sawa na kama hujafikiri vizuri hutajua ni kitu gani

Ndoa ni sehemu ya ukamilifu wa binadamu hasa mwanamke [nasema hivi kwa mtazamo wa Kikristo]

Lakini hata kibinadamu ndoa ni muhimu sana kwa binadamu yoyote ile

Kinachowafanya watu watafute njia ya kuiona ndoa sio ya muhimu ni kuumizwa na hili limetokana na binadamu kuiacha njia yake ya asili ya maisha na hapo ndipo maumivu yanapoanzia!
 
nemic4u

JF-Expert Member
Apr 4, 2011
438
500
umewahi kuolewa ukaona ni zigo? Usisikie wanayolalamika wenzako... Tambua ndoa ni sawa na choo:
kuna aliye ndani ya ndoa anataman kutoka kuna aliye ndani ya ndoa hataman hata kutoka wakat yule amabaye yupo nje ya ndoa anataman kuingi. Sawa na choo aliyemaliza haja zake anataka kutoka na yule anaeyendelea kutoa haja hana mpango wa kutoka na aliye na haja anataman kuingiaNa ingekuwa mzigo kweli watu wasingekuwa wanangangania kuingia huko...............na pia wangekuwa wameachika wengi kama kweli ni mzigo..............
 
Ennie

JF-Expert Member
Jan 15, 2011
7,140
2,000
Ni jamii tu inatuaminisha hivyo mamy lakini ndoa si kila kitu hasa kwa sasa ambapo hata thamani na maana ya ndoa zenyewe imeshuka sana.
Kama ulivyosema Zinduna ulifunzwa pamoja na mambo mengine kuweka akiba ili mume akikwama umsaidie,wanaume pia walifunzwa kuwa vichwa vya familia na waliona fahari kutimiza majukumu yao. Siku hizi wanaume wengi wanaona fahari kukuta chakula mezani na ada imelipwa bila yeye kutoa mfukoni mwake.
Nyakati zimebadilika na wazazi hasa kina mama tubadilike katika ulezi wa bint zetu. Nimempenda mama yake isha aliyemfunza mwanae kuwa independent. Mfunze bint kusimama kwa miguu yake na ajue yeye ana thamani akiwa au asipokuwa na mume.
Muonye kuhusu ngono zembe ila ikitokea ame conceive usianze kuuliza posa italetwa lini bali amejipanga vipi kulea mtoto ajaye yeye kama mama wa huyo mtoto.
 
Last edited by a moderator:

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom