Je, Kuna watu wana experience haya mambo? Cognitive dreams

Je, Kuna watu wana experience haya mambo? Cognitive dreams

Sijawahi kumwambia mtu kuhusu hii hali ambayo imekuwa inanitokea kwa miaka zaidi ya 10 sasa hasa toka nimpoteze Kaka yangu.

Tulicheza pamoja, Soma pamoja alikuwa kama best friend japo alinizidi miaka 3.

Kwanza japo amefariki zaidi ya miaka 10 sasa lakini karibu kila siku lazima niote tupo wote.

Pili, naota matukio ambayo yanatokea baadae. Nikiota jambo usiku mchana litatokea. Hii haitokei kila siku ila nikiota jambo litatokea.

Nilipokuwa nasoma kuna kipindi niliota maswali ya UE na nilikuwa sijajiandaa na mtihani. Siku hiyo niliamka nikawaambia wana nimeota maswali haya na haya yapo kwenye mtihani hawakuamini tulipoingia kwenye mtihani wakadhani nilikuwa na paper.

Kuna jamaa tuna-hang naye mtaani nikawaambia wana huyu jamaa nimeota kafuta kazi. Week 4 sio nyingi jamaa alisimamishwa kazi kwa kuiba pesa ya ofisi. Iliniuma saana kwasababu ningemsanua asingepoteza kazi.

Jana usiku jambo lililonifanya niandike uzi niliota ninapigana na mtu. Kabla hata siku haijaisha naendesha kidogo nikagusa gari la mama mmoja akatoka akaanza kunitukana lakini sikumsemesha neno.

Mfano mdogo kama nina jambo natafuta solutions nikilala basi nitaota namna ya kulitatua.

Siamini katika ulimwengu usioshikika.... I'm too realistic...sipo hapa kutafuta waganga wa kienyeji au msaada wa kiroho...I'm 100% perfect and I don't need another human being to tell me how imperfect I am.

Swali ni je Kuna watu wengine wana experience haya mambo?

Hii ni mifano michache tu....
Haahaaaa....!
Huo msaada ambao huutaki, utautafuta tu wewe mwenyewe.....!

Ni Wachache wapo hivyo, Mimi ni mmojawapo.

Life is Spiritual.....!
 
Hii pia mimi unitokea nikiota ndoto inaweza chukua mda nilishasahau ndo tukio linatokea naanza kuvuta kumbukumbu Nakumbuka kwamba ili jambo nimeshawahi kuliota
 
Swali ni je Kuna watu wengine wana experience haya mambo?
Ndio nipo Mimi mwenye experience ya hayo mambo... At least wewe unaota ukiwa umelala lakini Mimi huwa naota kwa hisia mchana kweupeeeeee.

Naweza nikatembea njiani, nikapata hisia kwamba kuna jambo fulani linaenda kunitokea hapo mbele na litaleta madhara haya na kweli lazima litokee kwa namna ile ile.

Na matatizo yangu yote binafsi ambayo yamewahi kunikuta huwa nayajua siku kadhaa nyuma kabla hayajanitokea, iwe kwa hisia au kwa ndoto za usiku ila kitu ambacho kinanitatiza hadi sasa ni kwamba nikishaona hayo maono huwa ni lazima yatokee hata ufanyeje kwa maana hakunaga solution juu yake.

Kwahiyo nipo hapa ndugu yako katika ndoto 😅😅😅
 
Huu uwezo binadamu anazaliwa nao Ila ukianza kupiga punyeto , ngono iwe kwa KE au ME uwezo hupotea Mara moja.
 
Ndio nipo Mimi mwenye experience ya hayo mambo... At least wewe unaota ukiwa umelala lakini Mimi huwa naota kwa hisia mchana kweupeeeeee.

Naweza nikatembea njiani, nikapata hisia kwamba kuna jambo fulani linaenda kunitokea hapo mbele na litaleta madhara haya na kweli lazima litokee kwa namna ile ile.

Na matatizo yangu yote binafsi ambayo yamewahi kunikuta huwa nayajua siku kadhaa nyuma kabla hayajanitokea, iwe kwa hisia au kwa ndoto za usiku ila kitu ambacho kinanitatiza hadi sasa ni kwamba nikishaona hayo maono huwa ni lazima yatokee hata ufanyeje kwa maana hakunaga solution juu yake.

Kwahiyo nipo hapa ndugu yako katika ndoto 😅😅😅
Je kwanini yawe mambo negative tu waht about positivity?.
 
Je kwanini yawe mambo negative tu waht about positivity?.
Katika experience yangu ya maisha ya namna hiyo, mambo mengi ambayo yamenijia kihisia ni negative kwamfano naweza nikawa natembea njiani ghafla kuna picha ya kihisia inanijia kwamba mbele nitakutana na jiwe au something nitakanyaga nitateleza nitaanguka nitatumia sehemu fulani then nitaenda home/hospital watanipa huduma fulani ya kwanza na kweli inatokea kama ilivyo😂😂... na jambo la ajabu zaidi hisia hizo zikinijia nakua sina alternative ya kukwepa jambo hilo.

Kwenye ndoto za usiku ndio kuna mchanganyiko na yale ya positive kwa kiasi chake.

Bado nipo napekua hapa na pale ili nione kama naweza kupata ufumbuzi juu ya mambo hayo yote.
 
Naona hiyo ni Law of attraction +subconscious Mind .

Unatumia muda mwingi kuwaza na kuzalisha negative thoughts

Kwahiyo Auto suggestion yako huwa inachukua negative na inakurudia negative in physical realm

Jaribu Ku-practice meditation uondoe huo uchafu .

Kufikiria jambo baya na likakutokea ni issue ya subconscious zaidi .

Tumia muda mwingi kuwa na productive and healthy thought.
 
Hii mimi pia unitokea hapa nilipo sasa nilishawai ota miaka miwili nyuma ila niliibishia nafsi kuwa siwezi kufika pale but nipo na kuna mazingira nayaonaga sana yanatokea ila nishawai yaota
 
Back
Top Bottom