Je kuna haja ya wanawake waajiriwa kupewa mapumziko wakiwa kwenye siku zao?

Yale maumivu achana nayo,ila mie nikilala huwa naona kama yanazidi bora niwe active.
Nakerwa tu na kubadili pads mara kwa mara kwenye public toilets na hasa nikiwa na kazi za nje ya ofisi!!
Hicho kisirani huwa si kila mwezi ila nikimu attend mtu wakati ninacho ataona rangi zote!!!
Unaingia ofcn umekunja uso hata salamu unaitolea kwenye meno kama hutaki,nikwaze kwa bahti mbaya nikutangaze makusudi!!!!!
Uanamke kweli kazi!!!!

Hahahaha ....mbavu zangu tafadhali...eti nikwaze kwa bahati mbaya nikutangaze makusudi...mweeh
 
period.jpg

Naamini mwanamke awaye yeyote ambaye bado anaziona siku zake anajua maumivu ya tumbo, hisia na msongo wa mawazo anaopitia wakati anapokuwa kwenye siku zake. wako wengine hulazimika kulala kitandani wakiwa hoi bin taaban wakati wanapozitumikia siku zao achilia mbali kisirani wanachokuwa nacho na mambo mengine yanayofanana na hayo.

Je kuna haja sasa ya sheria za kazi kuweka kipengele kitakachowapa nafasi wanawake waajiriwa ya kupumzika japo kwa siku mbili tu wakati wanapokuwa kwenye siku zao?

Naamini wengi mnajua ni kiasi gani hata ufanisi wa kazi kwa mwanamke aliye katika siku zake unavyopungua achilia mbali kisirani kinachoweza kujitokeza na kusababisha kutoelewana na aidha wafanyakazi wenzie au wateja pindi mwanamke aliye katika siku zake anapokuwa kazini.

Kwa mfano kule Japan hapo mnamo mwaka 1947 baada ya vita kuu ya pili ya dunia walipitisha sheria mpya ya kazi inayoitwa Menstrual Leave Policy. Sheria hiyo inawapa wanawake wanaoingia katika siku zao mapumziko ya siku mbili kutokana na maumivu wanayoyapata wakiwa katika siku zao ambapo kwa Kijapana wanaita Seirikyuuka (Physiological Leave). Mara baada ya sheria hiyo kutungwa na kupitishwa, ilisababisha wimbi kubwa la wanawake nchini Japan kuingia katika mfumo wa ajira nchini humo na hivyo kuongeza nguvu kazi na pato la taifa hilo kuongezeka mara dufu.

Najua wapo baadhi ya wanawake wenzangu wanaweza wasiunge mkono hoja yangu kwa hofu kwamba jambo hili linaweza kusababisha kuongezeka kwa unyanyasaji wa kijinsi kwa wanawake na pia kuwafanya waajiri kukwepa kuwaajiri wanawake kwa kuwaona kama ni mizigo na ni dhaifu.

Tukumbuke tu kwamba swala la kubeba mimba na likizo ya uzazi bado ni mtihani mkubwa sana kwa wanawake waajiriwa, ingawa swala la uzazi ni muhimu kwa ustawi wa taifa lolote duniani kwa sababu ni kitendo cha kuzalisha nguvu kazi mpya lakini bado mpaka sasa kuna baadhi ya waajiri wanakwazwa na swala la wanafanyakazi wa kike kubeba mimba.

Sasa je swala la likizo japo ya siku mbili kwa wanawake wanapokuwa kwenye siku zao watalipokeaje?

Mchango wenu tafadhali

snowhite, King'asti, BADILI TABIA, AshaDii, Lady doctor, ladyfurahia, Preta, Fixed Point, Kongosho, Nivea, Neylu, Lisa, miss neddy, miss chagga, Mamndenyi, Tina, Ennie, charminglady, Asnam, MankaM, Munkari, lara 1, Heaven on Earth, cacico, miss strong, a.rahabu, gfsonwin, afrodenzi, Husninyo, Karucee

Je kwa wale ambao mvujo wao hauna siku maalumu??? na pia wale amabo wakianza kutiririsha mvujo wanakuwa wanapitiliza siku 2 unawaweka kundi lipi??
 
Kuna kabinti machepere sana chuo....nilikishtukia kipo katika siku zake sababu uso ulimvimba kubita kawaida.....nikakaita nikakiambia "leo ukibugy step mimba unayo" kikaniuliza kwa nini? Nikamwambia si upo ktk siku zako!.....toka siku hiyo...kinanionea aibu asee
 
Kwa hiyo mtu akiwa kwenye siku zake ndo anapata mimba?
 
Hahahaha ....mbavu zangu tafadhali...eti nikwaze kwa bahati mbaya nikutangaze makusudi...mweeh
Hahaaaaa!!!!
Ndio inavyokuwa best,salamu ya kawaida tu unasikia kama mtu anakupigia kelele na akijifanya king'ang'anizi kuirudia mara tatu wakati hujisikii kuitika humuachi salama!!!
 
Kwa hiyo mtu akiwa kwenye siku zake ndo anapata mimba?

Ajabu hiyo hapo!!!
Ila walimu wa Biology wachache best,kuna wanaofundishwa na form 6 leavers ambao wanafundisha vile walivyoelewa wao!
 
Kwa hiyo mtu akiwa kwenye siku zake ndo anapata mimba?
Good question...
Naona amechanganya siku za hatari na siku za period.....
Siku za hatari mwanamke hawi katika period bali anabadilika ngozi na kuwa mrembo na mwororo kwa ajili ya kuwavutia wanaume kama vile wanyama majike wanavyowavutia wanyama madume ili wapandwe.
 
Hahaaaaa!!!!
Ndio inavyokuwa best,salamu ya kawaida tu unasikia kama mtu anakupigia kelele na akijifanya king'ang'anizi kuirudia mara tatu wakati hujisikii kuitika humuachi salama!!!
Nitakuwa makini sasa..
Ahsante kwa kunitahadharisha
 
Ajabu hiyo hapo!!!
Ila walimu wa Biology wachache best,kuna wanaofundishwa na form 6 leavers ambao wanafundisha vile walivyoelewa wao!
Lakini labda mabadiliko ya tabia nchi yamewafanya baadhi ya wanawake kubeba mimba wakiwa kwenye siku zao.
Tusimbishie sana, labda yuko sahihi.
 
Zinduna najifikisha hapa, nilivyokuwa mwalimu, ofisini kulikuwa watumishi 42 wakiume 6 waliobakia 36 ni wakike, hivi itakuwaje....?
 
Last edited by a moderator:
Lakini labda mabadiliko ya tabia nchi yamewafanya baadhi ya wanawake kubeba mimba wakiwa kwenye siku zao.
Tusimbishie sana, labda yuko sahihi.
Itabidi tuliosoma enzi za mtume Nuhu turudi darasani haraka sana!!!
 
hili ni tatizo kubwa kwa baadhi ya watu, kuna siku binamu yangu alikuwa anaumwa nilipo rudi home niliita sana sikupata jibu nilipoenda rum kwake nikamkuta ameanguka toka kitandan na amepoteza fahamu nkampatia huduma ya kwanza nkampeleka hospital akachomwa sindano ya kupunguza maumivu,nilipo muuliza akaniambia akiwa katika period anakuwa katika hali hiyo na anatapika sana
 
dah poleni dada zangu kungekuwa na uwezekano wa kusaidia hilo tungesaidia mbona tunachunwa sana tunapiga kimya?
 
Hahaaaaa!!!!
Ndio inavyokuwa best,salamu ya kawaida tu unasikia kama mtu anakupigia kelele na akijifanya king'ang'anizi kuirudia mara tatu wakati hujisikii kuitika humuachi salama!!!

Hahaaa kuna wale anakusalimia za asubuhi unamjibu nzuri...anaanza shwari....mzima...kabisa...khaaa huwa natamani kumeza mtu..
 
Back
Top Bottom