Je, Kinana ni mzalendo?

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,601
8,741
Nikiwa mdogo mwaka 1986 jirani yetu ambaye alikuwa anakaa kwenye nyumba za msajili njia ya Sanawari. Alikuwa mpole, mrefu na anaonekana tofauti sana kulinganisha na vijana wengine pale.

Mzee wangu ambaye alikuwa mmoja wa viongozi wakuu wa mkoa wa Arusha alialikwa kwenye harusi ya Kinana! Cha ajabu huyu kijana alikuwa kapata Ubunge na kuchaguliwa Naibu Waziri wa Ulinzi.

Mtaa mzima tulikula pilau karibu wiki nzima na Waziri wa Ulinzi wa wakati huo Salim Salim alikuja kwenye harusi ile ya mkeka na waligawa video tapes za harusi kila mahali. Kiukweli Kinana alikuwa anapedwa kama mfalme wa Arusha mjini miaka hiyo.

Baadae tukaanza kuona dry cleaners za wasomali na kuambiwa za Kinana!. Baadae Kinana akawa anajiona tofauti sana na wakazi wa kawaida nakumbuka vijiwe vya chai alikuwa hawezi kwenda tena.

Na ghafla Kinana akaanza kuwa mwongeaji zaidi🤔 sio yule mpole. Lakini Arusha ikaanza kubadilika kutoka kuwa mji wa Wamasai kuanza kuwa mji wa Wachagga. Miaka ya 90’s Arusha Mjini ukawa mji wa wafanyabiashara wahamiaji kutoka mji wa Moshi.

Wafanyabiashara wengi wa Kimasai ambao walikuwa wana support sana CCM na Kinana walihamia kwenye mashamba yao Arumeru, migodini na biashara nyingine baada ya wachagga kuleta ushindani mkubwa sana Arusha. Lakini wale wahindi wengi wa Arusha wenye pesa walibaki bila chama maana upepo ulikuwa unaenda upinzani.

Arusha walikuwa hawapendi serikali kwasababu ilikuwa haina mradi wowote pale mjini wa maana. Majengo yalikuwa na wauza mawe na wahindi na sio kampuni za Serikali au za pesa kama Dar.

Kinana naye akaja kama mfanyabiashara! Akafungua kampuni zake za utalii na uwindaji. Sawa kila majambazi wa kisomali wakishikwa kuna note inatoka juu zaidi Serikalini inasema waachiwe ni ndugu wa Kinana! Hii ni mpaka leo hii🤔. Gafla miaka ya 90’s Kinana akawa mfanyabiashara kuliko mwanasiasa na alipoteza watu wote waliokuwa wana msupport pale mjini.

Wakati huo kulikuwa na kikundi cha Wambulu wakiongozwa na tajiri wa magari Verani ambaye ndiye alikuwa mbebaji wa ngano za kampuni ya bia Tanzania nzima kutoka pale Karatu.

Wambulu wakakutana miaka hiyo na kumchagua kinara wao ambaye ndiye Sumaye awe mbunge ili nao wapate nguvu Arusha. Lakini baada ya kuona maji mazito sumaye alienda kugombea kwao na kubahatika kuwa Waziri! . Alivyokuja Mkapa na kumpa Sumaye Waziri Mkuu Sumaye akaja Arusha na kusema yeye ndiye king mpya wa Arusha na sio Kinana. Kitu cha kwanza sumaye alifanya kushindana ni kuwapa vitalu wambulu mbuguni baada ya miaka michache akatokea king of Tanzanite ambaye alikuwa na jina na Sunda! ambaye alikuwa kijana wa Sumaye.

Hili la Sumaye likamkimbiza kabisa Kinana na mpaka leo Kinana sio yule mzalendo ambaye alikuwa mbunge 1986.

Nasema haya na kumwonya Rais awe makini na Kinana ni mfanyabiashara hana mapenzi na mtu. Yeye anaona kama vile ana kazi na sio wito

Je, alisingiziwa hapa🤔?

The country's Natural Resources and Tourism Minister Khamis Kagasheki admitted to amaBhungane that politicians are involved in the ivory trade.

“This business involves rich people and politicians who have formed a very sophisticated network,” Kagasheki said.

His deputy, Lazaro Nyalandu, echoed this, saying that big names in the Cabinet and the army, as well as officials in wildlife conservation, the Tanzanian Port Authority, the immigration department and the police, are implicated.



“It is a hard fight because the network collaborates as a team, sharing information, money and positions,” Nyalandu said.

Shein
A report read by the main opposition party, Chadema, in Parliament in June pointed a finger at a member of the ruling Chama Cha Mapinduzi (CCM) party, wealthy businessperson Mohsin Abdallah Shein.

Shein was said to own 16 hunting blocks in game reserves. He allegedly uses these for poaching.

The hunting blocks are held by four companies – Royal Frontiers of Tanzania Limited, Game Frontiers of Tanzania Limited, Western Frontiers of Tanzania Limited and Northern Hunting and Enterprises Limited – which local media alleged belong either to him or his relatives.

This week, Shein described himself as “an innocent citizen of Tanzania” who is being targeted by business competitors.

“I've never been involved in illegal business, let alone elephant tusks,” he told the Mail & Guardian.

“I have a number of legal businesses and I don't see the point of it.”

Shein said that he owned Game Frontiers of Tanzania, but that the company operates “according to the law. These heavy allegations are full of lies.” He vehemently denied owning 16 hunting blocks.

Kinana
Another powerful figure under suspicion is the CCM secretary general, Abdulrahman Kinana.

In 2009, customs officers at the Vietnamese port of Haiphong found tusks weighing a massive 6.2 tonnes under bags of plastic waste on the freighter Sharaf.

The Sharaf Shipping Company, which owns the Sharaf, was registered in October 2003 in the name of Kinana and his wife.

Kinana insists he did not know about the hidden cargo. This week he said that both Interpol and the Convention on International Trade in Endangered Species had cleared him of any wrongdoing and that he was a victim of a politically motivated smear campaign.

Yaani eti huyu ndiye alikuwa awe next Salim salim. Hakunaga copy ya kipaji!

 
Akili za kimasikin zinakera sana so ukiwa mfanyabiashara ndio sio muadilifu sio?
Kuna vimaneno kwenye bandiko lake ama umeviruka Bahati mbaya ama umeviruka Bahati makusudi. Vinginevyo, usingeibuka na swali hili. Hata hivyo, Mimi naamini katika ushahidi usiotiliwa mashaka. Naamini, Makamu Mwenyekiti ni msafi mpaka hapo itakapodhibitika vinginevyo.
 
Nikiwa mdogo mwaka 1986 jirani yetu ambaye alikuwa ana kaa kwenye nyumba za msajili njia ya sanawari. Alikuwa mpole, mrefu na anaonekana tofauti sana kulinganisha na vijana wengine pale.

Mzee wangu ambaye alikuwa mmoja wa viongozi wakuu wa mkoa wa Arusha alialikwa kwenye harusi ya kinana! Cha ajabu huyu kijana alikuwa kapata ubunge na kuchaguliwa waziri mdogo wa ulinzi.

Mtaa mzima tulikuwa pilau karibu wiki nzima na waziri wa ulinzi wa wakati huu Salim Salim alikuja kwenye harusi ile ya mkeka na waligawa video tapes za harusi kila mahali. Kiukweli kinana alikuwa anapedwa kama mfalme wa Arusha mjini miaka hiyo.

Hili la Sumay likamkimbiza kabisa Kinana na mpaka leo kinana sio yule mzalendo ambaye alikuwa mbunge 1986.
Mkuu @kamindu, Kinana ni mmoja wa wazalendo wa kweli wa nchi hii!. Ni Kinana na Nape ndio wameiokoa CCM ile 2010 to 2015 kwa zile ziara zao za amsha amsha, baada ya kusoma bandiko hili CCM Imechokwa, CHADEMA Haijajipanga!, kwenye bandiko hili nilishauri
Wanabodi,
Nasisitiza CCM imechokwa, na ule ushindi wa kishindo wa Kikwete toka asilimia Zaidi ya 80% mwaka 2005 hadi asilimia 60% 2010, ni uthibitisho tosha, Watanzania sasa wameichoka CCM ila pia hawakuwachagua wapinzani kwa wingi zaidi, kwa sababu wapinzani bado hawajaonyesha kukomaa vya kutosha kuweza kukabidhiwa nchi kwa kushindwa kuonyesha utayari kukamata dola na kutawala.

Najua kwa dhati, japo CCM na JK wanafurahia ushindi huu kiduchu kwa furaha, ni furaha ya machoni tuu, lakini moyoni ni maumivu na vilio kwa huzuni ya kukataliwa toka ushindi wa kishindo wa asilimia 80% ya 2005 hadi ushindi kiduchu wa asilimia 60 za 2010, na hiyo asilimia 20% ya kukataliwa, kukataliwa ni kukataliwa tuu kunauma!.

Hivyo chama makini chochote lazima kikae chini na kujiuliza, hivyo CCM lazima watakaa chini na kujiuliza kulikoni, ni katika kujiuliza huko, huenda wakajipanga upya na kuja kwa mbinu mpya, kwa nguvu zaidi na kasi zaidi, ila kwa vile CCM imechokwa, hata ijipange upya vipi, kama Chadema itajipanga, then kwa CCM, safari ya kwaheri ndio imeanza, there is nothing to stop it from failing down unless ibadilike kwa revamping.

Dawa pekee ya kuitibu CCM chovu iliyochokwa, ni kuirevamp CCM completely, task nambari moja ni Makamba and his old guards pale Lumumba, should go, kupisha new blood. Tena CCM msisubiri mpaka uchaguzi mkuu wa chama chenu, miaka miwili ijayo (2012), itakuwa too little too late. If you are to do anything, just do it now and fast!. Leteni fresh blood kina January type, Kippi, Nape type and the like ambao wanaziweza siasa za kisasa za .dot com type.

Pasco..
Ushauri huo ulifuatwa immediately, CCM wakamtoa Makamba, wakamuingiza Kinana, Nape na January na hapa ndio survival ya CCM ilipoanzia maana ilikuwa almost dead! Chadema ilikuwa wachukue nchi Yametimia!, CCM Imechokwa!, CHADEMA Njia Nyeupe 2015!-Jipangeni! hapa ni Kinana ameiokoa CCM!.

Baada ya issue ya uraia wa Azim Premji kuibuka, Kinana alirekebisha uraia wake kwa official declaration kama Bashe na Jenerali Ulimwengu, ila kiukweli kabisa kuna watu kibao tuu ambao sio raia wa Tanzania lakini ni wazalendo kuliko Watanzania wenyewe!, watu kama Joan Wickens, Amiri Jamal, Dr. Leader Starring, Oscar Kambona, Michael Kamaliza, Chinyama Chiume etc, hivyo Kinana ni mzalendo wa kweli kabisa wa Taifa hili!.

Kitendo cha Kinana kutukanwa na yule kichaa ile 2015 na ule ukichaa wa voice notes ulimfedhehesha sana Kinana nami niliuzungumza hapa, Psychoanalysis ya Waomba Msamaha Kwa Rais, Makamba Snr is the Next, Membe Will Never for Pride, Kiburi na Jeuri, Kinana Will Never for Integrity humu nilisema
7. Comred Kinana.
Huyu is the man of principles and integrity, anakisimamia kile anachoamini, ule waraka ni wake, na yote alioongea ni yake na ni kweli tupu, men of principles and integrity they stand with what they believe, kama ni kuadhibiwa kwa kuusema ukweli, let it be!. Hapa naomba kutoa angalizo kuhusu Kinana, kwa mambo Kinana aliyoifanyia CCM, akija kuadhibiwa adhabu yoyote kwa kuonewa, kwa kuusema ukweli wake, kiukweli kabisa Mungu atampigania!, hiyo karma yake.... usipime!.
Imevuja sauti inayodaiwa ni Maongezi ya Simu ya Nape Nnauye na ...

9. My Take.

2.Udukuzi ni kosa la jinai, ili nchi yetu kuonyesha inaheshimu utawala wa sheria, baada ya zoezi la misamaha kukamilika, naomba serikali yetu iwachukulie hatua wadukuzi sio waliodukua, maana hawa tunawajua na tunajua udukuzi unaendelea kufanywa kila siku, tena usikute hata mimi ninadukuliwa, bali walio likisha sauti hizo zilizodukuliwa kinyume cha sheria, wafikishwe mbele ya vyombo vya sheria, tena kitu cha ajabu, unaweza kukuta hakuna hata mtu mmoja kati ya walidukuliwa amekwenda kushitaki au kulalamika rasmi mawasiliano yake binafsi kudukuliwa kinyume cha sheria, naijua sababu iliyofanya watu walio dukuliwa wasiende kuripoti popote, naomba kuwafariji kwa kuwaeleza kitu kinachoitwa karma kitawalipia, wadukuzi yatawawakuta ya kuwakuta na walio watuma, na waliodukuliwa na kuwa persecuted, watafidiwa na malipo ni hapa hapa duniani, mbinguni ni hesabu tuu!.

Paskali.
Natumaini wale mnao ijua karma by now you can connect the dots usikute karma ya Kinana imechangia kwenye ile issue na huku kuwa elevated ni karmic consolations kumfidia!.
Nasisitiza Kinana ni mzalendo, and also karma is real, mtu akiwa mzalendo wa type kama ya Comred Kinana, mtu uki doubts uzalendo wake, ukaandika au kumshitumu, watu wakianza kum doubts kutokana na andiko lako, chochote negative kitakacho sababishwa na andiko lako, kitakuwa na karmic consequences
P.
 
Walikuwa wanampenda Mungu, wanyenyekevu kwa mwenyezi mungu, ila machoni pa watesi wao ni watu wsbaya
IMG-20221210-WA0000.jpg
 
kijana alikuwa kapata ubunge na kuchaguliwa waziri mdogo wa ulinzi.
Unamaanisha naibu waziri ?

Nasema haya na kumwonya Raisi awe makini na kinana ni mfanyabiashara hana mapenzi na mtu. Yeye anaona kama vile ana kazi na sio wito
Viongozi wote wa Sasa ni wafanyabiashara hata Ccm ni chama cha wafanyabiashara na matajiri wenye ukwasi....acha kumlenga Kinana pekee.
 
Back
Top Bottom