Je, Kikwete ni Msafi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, Kikwete ni Msafi?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BAK, Mar 10, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Mar 10, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,587
  Likes Received: 82,207
  Trophy Points: 280
  Ni zamu ya Kikwete
  Baada ya Lowassa, Rostam...

  na Irene Mark
  Tanzania Daima~Sauti ya Watu

  BAADA ya wanamtandao wawili maarufu, Edward Lowassa na swahiba wake kisiasa, Rostam Aziz kutikiswa kisiasa, dalili za awali zimeanza kuonyesha kwamba, jina la Rais Jakaya Kikwete nalo limeanza kuwekwa chini ya mstari mwekundu.

  Matukio ya hivi karibuni yanaonyesha kuwa, wiki hii imeanza kuchukua mkondo mbaya kwa Rais Kikwete ambaye kwa mara ya kwanza jina lake limeanza kuingizwa katika maeneo mabaya, ambayo rekodi zinaonyesha ndiyo waliyopita marafiki zake wawili, Lowassa na Rostam ambao hivi karibuni walikumbwa na gharika ya kisiasa wanayoendelea kukabiliana na athari zake.

  Kwa mara ya kwanza, jina la Rais lilitajwa katika gazeti la kila wiki la MwanaHalisi ambalo katika habari yake kubwa lilionyesha dalili za kumhusisha Kikwete na ajira yenye mwelekeo wa kutia shaka ya mtoto wake mkubwa Ridhiwani ambaye anafanya kazi katika kampuni binafsi ya uwakili kama mwanasheria.

  Siku chache tu baada ya kutajwa huko kwa rais waziwazi na kwa mara ya kwanza tangu aingie madarakani Desemba 21, mwaka 2005, katika sakata linalomhusisha mtoto wake huyo, dalili za mara moja zilianza kuonyesha kutikisika kwa mamlaka za dola.

  Katika hali isiyotarajiwa, suala hilo la kutajwa kwa Rais Kikwete lilianza kuchukua mwelekeo unaoonyesha kuwa wenye lengo mahususi la kumpaka matope katika mwenendo unaokwenda sambamba na kuwapo kwa madai mengine ya kuwapo kwa jitihada mahususi za kumsafisha Lowassa ambaye hivi karibuni alilazimika kujiuzulu uwaziri mkuu baada ya jina lake kutajwa katika kashfa ya Richmond.

  Hali hiyo ilisababisha kuitishwa mara moja kwa mkutano wa pamoja kati ya Jukwaa la Wahariri na Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari (MOAT) uliofanyika katika Hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam na kutoa tamko kuhusu masuala hayo makubwa mawili; kuchafuliwa kwa Rais Kikwete na kusafishwa kwa Lowassa.

  Habari kutoka ndani ya mkutano huo zinaeleza kuwa, wamiliki na wahariri hao waliafikiana kimsingi kuwa, kazi ya wanahabari si kuchafua au kusafisha viongozi, bali kuandika habari za kweli, zilizotafitiwa na ambazo zinazitendea haki pande zote zinazotajwa katika habari husika.

  Katika tamko lililotolewa kwa pamoja na Mwenyekiti wa MOAT, Reginald Mengi na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Sakina Datoo, vyombo vya habari vilikubaliana kimsingi kudumisha misingi na kanuni za uandishi wa habari wakati wanapotimiza wajibu wao.

  Mkutano huo kwa namna ya pekee ulionyesha kupanda kwa joto la kisiasa hapa nchini, tangu jina la Rais Kikwete lilipoanza kutajwa katika masuala ambayo yanaonyesha mwelekeo wa wazi wa kuendelea na mashambulizi ya waziwazi ya kuchafuana miongoni mwa viongozi wakitumia baadhi ya vyombo vya habari ‘lynch mob.’

  Siku moja tu baada ya angalizo hilo kutolewa na MOAT na Jukwaa la Wahariri, Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe jana alivurumisha tuhuma nzito dhidi ya Rais Kikwete akieleza kushangazwa kwake na namna anavyoshughulikia wizi wa fedha katika akaunti ya malipo ya madeni ya nje (EPA) maarufu kwa jina la Kashfa ya EPA.

  Mbowe aliyekuwa akihutubia kongamano la wanawake wa CHADEMA lililofanyika katika Ukumbi wa Urafiki jijini Dar es Salaam, jana, alisema kushindwa kwa rais kuyatumia ipasavayo madaraka yake ya kikatiba dhidi ya wezi hao ambao sasa inadaiwa kuwa wameanza kuzirejesha fedha hizo, kunamfanya yeye mwenyewe aonekane akiingia katika kashfa hiyo.

  Alisema Rais Kikwete anahusika katika kashfa ya ufisadi kwa sababu ameshindwa kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wa ufisadi licha ya kuelezwa mara kadhaa kwamba anayo mamlaka ya kuwakamata na kuwachukulia hatua za kisheria mafisadi waliotajwa kwenye taarifa ya kampuni ya ukaguzi ya Ernst & Young.

  Alisema zipo juhudi za makusudi zinazofanywa na serikali ya awamu ya nne chini ya utawala wa Rais Kikwete za kuwalinda na kuwatetea watuhumiwa wa ufisadi, hasa waliodhulumu fedha za EPA.

  “Zipo juhudi za makusudi za kuwalinda na kuwatetea mafisadi wa EPA… tunalaani kauli ya Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustapha Mkulo, kwamba fedha zilizoibwa EPA zimeanza kurudi huku kukiwa na siri katika kuwataja hadharani waliorudisha.

  “Huu ni uhuni, kwa wezi kurudisha fedha halafu wanaendelea kutamba mitaani. Hii inatulazimu kuamini kuwa Rais Kikwete anahusika. Tunataka hiyo timu ya rais iliyotumwa kuwachunguza hao mafisadi itutajie majina ya walioanza kurudisha fedha zetu na hatua gani za kisheria zilizochukuliwa dhidi yao.

  “Sheria inaruhusu kukamatwa kwa watu hao na kufunguliwa mashitaka ya uhujumu uchumi, tunasema ngoma hii ni nyepesi, najua tutakutana na serikali bungeni katika mkutano wa Aprili, wakitukwamisha tunaileta hoja yetu ya kutaka majina ya wanaorudisha fedha kwa wananchi,” alisema Mbowe.

  Katika hilo, alibainisha kwamba wabunge wa chama chake wamejizatiti katika kupigania maji safi na salama kwa kuwa fedha nyingi za wananchi zinaliwa na wachache kwa manufaa binafsi.

  Alitoa mfano kuwa zaidi ya sh bilioni 133 za EPA zilizoibwa na watu wachache zingetosha kusambaza huduma za mabomba ya maji safi na salama kwa kila kijiji nchini.

  “Laiti hao mafisadi wangejua ni kiasi gani wanawatesa wanawake na watoto katika suala zima la maji safi na salama, Watanzania tungepiga hatua kubwa kimaendeleo,” alisema Mbowe na kuongeza kuwa ni lazima serikali ieleze ukweli kuhusu ufisadi na kuwachukulia hatua stahiki watuhumiwa wote.

  Akizungumza kuhusu umoja na mshikamo wa kitaifa, Mbowe aliwata wanawake wa CHADEMA kutowabagua wala kuwatenga wanawake wenye itikadi nyingine, badala yake washirikiane nao katika kuwabadili kiitikadi. Pia aliwashauri kutoingiza uzalendo wa kijinsia katika kutetea haki zao na kutokuwa tayari kufaidi matunda ya ufisadi.

  “Msiingize uzalendo wa kijinsia katika kutetea haki zenu hasa kwenye suala la ufisadi… msiwe tayari hata kidogo kufaidi matunda ya ufisadi, taifa linaangamia kwa ajili ya wachache. Nawaomba tuichukue vita hii tuipeleke katika familia zetu.

  “Lazima tujue tu wasafi kwa kiwango gani kabla ya kuwahukumu wenzetu… tukianzia kwenye familia tutaweza kupambana katika ngazi ya taifa,” alisisitiza Mbowe.

  Alisema, nyuma ya kila mwanaume aliyefanikiwa, kuna mwanamke aliyeteseka. Aidha, kaulimbiu ya maadhimisho hayo ilikuwa ni ‘Tuelekeze rasilimali fedha katika usawa wa kijinsia’.
   
 2. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #2
  Mar 10, 2008
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Mambo mengine hata hayana kichwa wala miguu.
   
 3. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #3
  Mar 10, 2008
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Kichwa ni Kikwete na miguu ni ufisadi
   
 4. BabaH

  BabaH JF-Expert Member

  #4
  Mar 10, 2008
  Joined: Jan 25, 2008
  Messages: 703
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Wewe utakuwa na matatizo, au ni ma mluki na umekuja hapa kwa sababu zako maalumu tu,
  Kwani wewe huoni umuhimu wa habari hii kabisa??
  Kwani ni uongo kuwa Kikwete ni muhusika mkubwa wa Ufisadi? Na si ndichokinaelezwa hapa.
   
 5. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #5
  Mar 10, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,587
  Likes Received: 82,207
  Trophy Points: 280
  Watu kama nyie ndio mnanifanya niwe mmoja waliokuwa addicted na ukumbi huu na kujua kwamba kuna Watanzania wengi ambao bado wanajali sana mwelekeo wa nchi yetu. Watu wanaiba mabilioni ya shilingi na bado wako huru na mali zao hazijafilisiwa, na Mkuu wa SK haoni kama kuna walakini wowote! tukianza kuhoji juu ya hili inakuwaje vibaka wadogo wadogo wanasweka lupango kila kukicha wakati wezi wanaoiangamiza Tanzania wanaachwa huru, tunaambiwa hakuna kichwa wala miguu! Mwe! ukistaajabu ya hayawani utaona ya .......
  Ahsante sana.
   
 6. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #6
  Mar 10, 2008
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Napenda kukufahamisha kuwa mimi si mamluki, wala sina tatizo wala matatizo, sioni umuhimu wa kumuunganisha JK na mwanae, jee ukifumaniwa wewe ndio kafumaniwa mwanao?

  Ni uongo usio na mfano kumhusisha mfichuwa ufisadi na mwajibishaji wa mifisadi kuwa yeye ndie "muhusika mkubwa fisadi", huoni haya, basi hata vibaya?
   
 7. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #7
  Mar 10, 2008
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Yaani unataka kutuaminisha kwamba JK hafahamu kuhusu ajira ya mwanawe?Hivi hujasikia mzazi anaisaidia polisi when mwanae ame-disappear baada ya ku-commit crime.
  Inawezekana kwa mtazamo wako habari hii haina kichwa wala miguu,ndio demokrasia hiyo.Pengine hata Nicolaus Mkapa anapohusishwa na ufisadi wa baba yake huko Kiwira ni habari isiyo na kichwa wa la miguu.Didnt somebody say like father like son?
   
 8. BabaH

  BabaH JF-Expert Member

  #8
  Mar 10, 2008
  Joined: Jan 25, 2008
  Messages: 703
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kama ulifuatilia mjada uliomuhusisha Ridhiwani kupata kazi IMMA, kuna mchangia alieleza sifa za huyo Ridhiwani, kwa kutumia Vigezo vya Masha, inaonyesha kuwa Rodhiwani hastaili kupata kazi IMMA, ok, na kazi iliyoifanya IMMA kwa kuifungua Deep Green na hapo Badae kuifirisi, ni kitu ambacho hakipo katika sheria,Kwa namna hii kuna logic association katika haya mambo, lazima uwe na upeo wa kufikilia sana hapa

  pili

  Kwa taarifa yako, Kikwete ajafichua Ufisadi wowote na mwanzo alipoambiwa mambo ya Ufisadi alitoa kauli za kejeli, na pia hajashughulikia Mafisadi wowote zaidi ya kuwakumbatia ili nae wasimfichulie Maovu yake, huo ndo ukweli Kikwete smart hata kidogo
   
 9. S

  Siao Member

  #9
  Mar 10, 2008
  Joined: Jan 4, 2008
  Messages: 96
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hakuna cha kikwete wala sijui ridhiwani..!

  Sisi sio watoto...!

  Wote wawili ni kundi moja tu ...!
  Tena waangalie sana maana majina yao yanaanza kuwa KERO kabisa masikioni mwa watu...!
   
 10. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #10
  Mar 10, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  Kwa kawaida huwa ninaliheshimu sana gazeti la Tanzania Daima, lakini kama limefikia hivi, kuandika kichwa cha habari ambacho hakifanani na the heart of the article, basi no hope na media zetu, yaaani na wao pia hawaelewi kuwa kuajiriwa ka Ridhiwani huko IMMA ni uamuzi wa IMMA period?

  I mean kama kuna ishu ya Deep Green, au Tangold, zisizungumziwe kwa kuchaganya ishu ya ajira ya kijana IMMA, ni ishu mbili tofauti na kwa wanaolilia kuwa ni lazima ziende pamoja hawaelewi kuwa wanatoa mwanya wa Deep Green na Tangold, kukwepa lawama kama ipo, mimi tatizo langu ni kwamba IMMA wanayo haki ya kumuajiri m-Tanzania yoyote kwa faida ya biashara zao, nashangaa media nayo haielewi hilo, basi kaazi! kweli! kweli!
   
 11. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #11
  Mar 10, 2008
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 3,749
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  unashangaa nini wakati makala imeandikwa na gazeti la mbowe aka chadema ! ndio maana sisomi magazeti yao, kila leo wamekazania ccm, ccm, ccm, ccm, jk, el, uvccm, nchimbi, utadhani hakuna mambo muhimu zaidi ! that shows wapinzania bila ya chama tawala will never exist !
   
 12. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #12
  Mar 10, 2008
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Mazingira haya yanatisha kweli kweli.

  Watu wawili kutoka kampuni iliyomwajiri mtoto wa rais wamepewa madaraka makubwa sana serikalini na rasi huyo huyo huku kampuni hiyo hiyo ikihusishwa moja kwa moja na uundwaji wa makampuni hewa yaliyoshiriki katika wizi mkubwa wa fedha za umma.

  Ngoma nzito sana kucheza na akili timamu.
   
 13. K

  Kithuku JF-Expert Member

  #13
  Mar 10, 2008
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Mkuu naona hata wewe "the heart of the article" kama ulivyoiita hujaiona, au umeamua tu kumtetea Ridhiwani. "Heart of the article" sio Ridhiwani, nadhani hata ukiondoa heading ya story hii ukawapa watoto wa sekondari waisome wapendekeze heading, hawatamtaja Ridhiwani, maana siye wazo kuu la article hii. Kikubwa anachosema mwandishi ni kuwa baada ya watuhumiwa kadhaa waliokwisha kutajwa, sasa hivi tuhuma za waziwazi zinaelekezwa kwa rais, na akataja wanaomsema waziwazi hadharani ni vyombo vya habari (Mwanahalisi) na Kiongozi wa Upinzani (Mbowe). Ndicho anachosema huyu dada mwandishi, kuwa sasa hivi watu wana guts za kusema "hata JK yumo". Sasa kama JK yumo kweli humo kwenye ufisadi ama hayumo, ni jambo analoweza kuthibitisha ama kukanusha mwenyewe kwa vitendo vyake. Waandishi wataandika watakayoandika, lakini wasomaji wa habari tutaamini tutakayoelewa kwa mujibu wa tafsiri zetu. Na hizi tafsiri ndizo zinazojenga public opinion juu ya uongozi mzima akiwemo Rais mwenyewe. Hata kama waandishi wa habari wasipotamka waziwazi kuwa "JK yumo miongoni mwa mafisadi", iwapo maandishi yao yatatuwezesha kutafsiri hiyo (constructed meaning), basi ndio opinion tutakayokuwa nayo juu ya JK na timu yake. Na hata wakizuiwa kuandika hicho kitendo cha kuzuiwa pia kitapewa tafsiri, pengine mbaya kuliko ile ambayo ingekuwapo wanapoandika.

  Kifupi kabisa ni kuwa sasa wapo wengi wenye mashaka kuwa huenda hata JK si msafi katika suala hili la ufisadi, naye JK hajawaondolea watu mashaka hayo hadi sasa.
   
 14. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #14
  Mar 10, 2008
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Ndo FMES anatetea eti Masha ni safi!

  Kuna shaka kama hata JK nae ni safi! Mwenye macho haambiwi tazama!
   
 15. K

  Kalamu JF-Expert Member

  #15
  Mar 10, 2008
  Joined: Nov 26, 2006
  Messages: 874
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hapana.
  Inabidi tuanze kuamini kuwa Kikwete sio safi.
  Dalili zimeanza kuwa wazi kuwa Kikwete sio safi hata kidogo.

  Kufunikafunika mambo yanayohusu kashfa kunachukuliwa kuwa ni mbinu za kuwasahaulisha watu.

  Kuchelewesha mkondo wa sheria katika mambo yaliyothibitika kuwa ya uhalifu kunawafanya watu wahitimishe kivyao - Kikwete si safi.

  Pengine anasita kuchukua hatua kwa maslahi yake mwenyewe na si kwa maslahi ya nchi.
   
 16. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #16
  Mar 10, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,587
  Likes Received: 82,207
  Trophy Points: 280
  Mkuu kichwa cha habari kilikuwa ni "Zamu ya Kikwete" baada ya Lowassa na Rostam Aziz. Tunawajua hawa wote wawili si safi ndio maana mmoja kamwaga unga na mwingine bado anajikanyakanyaga kutetea ulaji wake, sijui kama atafanikiwa. Hivyo hilo swali la "Je, Kikwete ni Msafi" ni mimi ambaye nimeliweka sidhani kama lina tofauti kubwa na "Baada ya Lowassa na Rostam Aziz ni zamu ya Kikwete"

  Kama kichwa cha habari hicho kimekuchanganya, basi niwie radhi mkuu.
   
 17. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #17
  Mar 10, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Hoja nyingine bwana, sasa kama baba anamtumia mtoto kufanya uhuni, mtoto asitajwe? Hivi kweli wewe na utimamu wote wa mawazo unaamini kuwa kampuni ya anayofanya kazi mtoto wa Rais na ambayo imehusishwa na ufisadi wa chama tawala inatoa Jaji ni jambo dogo?

  Yaani huyo mfichua ufisad na mwajibishaji ndio nani? Aliwafichua lini hao mafisadi na aliwawajibisha lini? Aangalie tu akinyosha kidogo asije kuwa anaonesha kwenye kioo ambacho kinaoonyesha sura yake!
   
 18. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #18
  Mar 10, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,587
  Likes Received: 82,207
  Trophy Points: 280
  Hata magazeti ya chama na siri kali yanaandika habari mbali mbali kuhusiana na ufisadi wa viongozi wetu. Magazeti ya uhuru, mzalendo, daily news na sunday news yameandika kuhusiana na kashfa za EPA, Richmond, Fisadi Mkapa na wengineo . Cha ajabu ni kipi kwa Tanzania daima kuhoji kama sasa ni zamu ya Kikwete? Huwezi kuendelea kuwakingia kifua mafisadi kama wewe mwenyewe unajijua huna doa! Upoonyesha woga wa kuwafukuza kazi kwa kutumia madaraka uliyonayo kama Rais wa nchi basi kuna walakini mkubwa hapo!
   
 19. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #19
  Mar 10, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,587
  Likes Received: 82,207
  Trophy Points: 280
   
 20. a.9784

  a.9784 Senior Member

  #20
  Mar 10, 2008
  Joined: Feb 19, 2008
  Messages: 146
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  BABA H wewe ni mtu mzima,au na wewe ni fisadi?Ajira ya Ridhiwani unaijua?Waanzilishi wa IMMMA unawajua?Kwanini unamtetea JK na mwanae ktk kuhusika na ufisadi.JK naamini sio msafi.Kwanini anawakumbatia akina Balali mpaka leo?
   
Loading...