Je Kikwete arudishe fedha za nguo anazonunuliwa na nchi yake "maskini'? atumie mshahara wake?

Awo umeeleza vyema ila ukumbuke kuwa vimishahara hapa bongo vipo chini sana hasa kwa watumishi wa serikali ila wangeweza kuanzisha mfumo ambao hizo posho zingehesabiwa kwenye mshahara (au zilipwe pamoja na mshahara) kama za likizo, incentives, perdiems, nk kama wanavyofanya nchi nyingi za Ulaya na hata Japan

Tuwalipe vizuri sana tu ila wajihudumie wenyewe. They have to be responsible.
 
Si kwamba hana uwezo na fursa, tumejikuta tunarithi utamaduni mbaya, walala hoi "kumnunulia Rais wao soksi na nguo za ndani na nje? Mavazi". Sharti wachangia maendeleo watulipue na kutudharau. Hata kama Salva atakataa ofa ya MWARABU, haiswihi mkulima wa matombo kusikia kuwa kuna fungu la kumvika mzee wa kaya. Nadhani Tume ya Jairo iangalie na kanuni hizi mbovu na kupendekeza maboresho. Sidhani kama Obama naye anafanya madudu kama haya, na kamwe TUSIJIFICHE nyuma ya kanuni zinazotungwa na wachache kufurahisha watawala. "The practice may be legally right but morally and ethically wrong".
 
Si kwamba hana uwezo na fursa, tumejikuta tunarithi utamaduni mbaya, walala hoi "kumnunulia Rais wao soksi na nguo za ndani na nje? Mavazi". Sharti wachangia maendeleo watulipue na kutudharau. Hata kama Salva atakataa ofa ya MWARABU, haiswihi mkulima wa matombo kusikia kuwa kuna fungu la kumvika mzee wa kaya. Nadhani Tume ya Jairo iangalie na kanuni hizi mbovu na kupendekeza maboresho. Sidhani kama Obama naye anafanya madudu kama haya, na kamwe TUSIJIFICHE nyuma ya kanuni zinazotungwa na wachache kufurahisha watawala. "The practice may be legally right but morally and ethically wrong".

Dunia nzima ikulu zote wakuu wake wanahudumiwa na Serikali zao mpaka naniii zote,kuna watoa huduma hizo,na ni wajibu wa ikulu kama taasisi ya URAIS kuwajibika kutoa huduma zote hizo mpaka mashuka,kama tunavyohudumiwa vitanda vyetu hospitalini na labour za kina mama,Huduma hiyo ni kwa faida muonekanao wa kiongozi kama alama ya Taifa.Watoa huduma hizo wakisha toa wanaleta invoice zao wanakunja chao,ilo liko wazi dunia nzima.Ila kwa hili la Rais wetu kupewa suti ni aibu kwake na kwetu sisi kama Taifa.

Kulipwa mshahara ni wajibu wetu kumlipa haki yake kama,binadamu yoyote anapofanya kazi ana haki ya kupokea malipo kama ujira wake.Wapo MACEO na Wakulugenzi wa Mashirika wanafaidika na privilege za kiongozi nje ya mshahara wake yeye.na kutoa muonekano wa kiongozi huyo kwa mujibu wa dhamana yake kwenye sekata au taasisi husika.

Na mshahara wake utatumika kwa faida zake yeye binafsi kama kuwasomesha kuwahudumia ndugu zake na kuwasaidia watoto wake kama masomo nk.
 
Katika majibu yao Ikulu imesema kuwa Rais Kikwete haitaji kununuliwa nguo na mfadhili yeyote au kupelekwa shopping. Kwamba, "toka akiwa Waziri wa Mambo ya Nje alikuwa anapokea posho ya mavazi. Na sasa kama Rais jukumu lote la mavazi yake ni la serikali"! Najiuliza hivi hadi Rais ananunuliwa nguo na wananchi wake maskini huku akipokea mshahara mnono. Kwanini asitakiwe arudishe fedha zote za kununulia nguo alizopewa na taifa lake maskini juu ya mshahara wake?


Ni wazo tu ambalo limenijia. Au kumtaka arudishe tutakuwa tunamnyima "haki" yake kwa sababu "sheria haimkatazi". Je kitu kikiwa kisheria maana yake ni kiko kimaadili? when a thing is legal does it me it is also moral and ethical? In other countries for example abortion is legal but is it moral?


Je tukijua kiasi kilichotumika kumnunulia nguo tangu akiwa FM hadi sasa kama Rais haziwezi kutosha kunaksisha madarasa kadhaa ya shule za kata?

kama anagharimiwa na kukirimiwa vitu hivi vyote na nchi yake.. gari, afya, mavazi, chakula hata kuhudumia wageni.. analipwa mshahara kwa ajili gani.. maana wengine wanalipwa mishahara kwa ajili ya kazi wanazofanya ili waendeshe maisha yao.. sasa yeye maisha yake yote yanaendeshwa na fedha za Watanzania hadi tai na viatu.. aidha mshahara wake upunguzwe au arudishe hizo fedha... nawaza tu


Mkjj saa nyingine unabore na maandiko yako. Huwa unakosa vya kuandika au ndio chuki binafsi kwa Kikwete? Unanchekesha!
 
Mkuu wangu hata mimi nilipoyasoma majibu ya Rweyemamu niliijiwa na maswali zaidi hasa pale aliposema matumizi ya rais kama suit zinanunuliwa na Ikulu!..hii kusema kweli haikukaa vizuri kabisa ikiwa rais wetu matumizi yake yote yanalipwa na Ikulu wakati na mshahara wake hauna matumizi..
Mkuu Mkandara, alichokisema Salva ni ku white wash posibility ya rais wetu kununuliwa suti, ili kuwaambia Watanzania, kazi ya kuvisha rais wetu ni kazi ya ikulu na sio kazi ya mwarabu yule.

Tukirudi kwenye ukweli, kununuliwa mavazi ni stahili za rais kwa mujibu wa Government Standing Orders na sio kwa rais tuu, na watumishi wengine wote wa numma. Kama hizi ni stahili, unategemea afanya nini?. Tena afadhali hizo za rais, kingine ambacho hamjui, sio tuu kununuliwa mavazi, bali hata kula yake na familia yake, tunawalisha sisi kwa kodi zetu.

Msisahau, yeye ndie amiri jeshi wa majeshi yetu ya ulinzi na usalama, hivyo licha ya kupata stahili zote utumishi wa umma, pia anapata stahili zote za wanajeshi wetu, tena sio kama prilage bali ni rights.

Jee wengi humu mnazijua privilages za wajeshi wetu?, wanakula bure, wanapewa mavazi yote ya kazini mpaka nguo za ndani!, wanalala bure, wanasafiri bure, ot top of that, hawakatwi kodi na hawalipi kodi ndio maana wana maduka yao, sasa bado utajiuliza mishahara ya wanajeshi wanaifanyia nini?.

Stahili sio uamuzi wa JK ndio utaratibu, hata kama binafsi angependa kupanda beatle, Custom made, Bullet Proof M-Benzi ndio stahili iliyokuwa approved kwa hadhi yake. He has no choice lazima afuate. JK ni mpenzi wa Msondo Ngoma, na pia ni kipenzi cha watu, hata kama anajiamini anapendwa, analazimika kuvishwa BP, hata kama anaipenda Msondo anauliwa kwenda kwa wanakumbuka kisa cha Alof Palme hili wanalijua.

Stahili ni mambo ambayo mtu wa level fulani anastahili kuhudumiwa, ndio maana Spika Sitta alipangishiwa nyumba ya hadhi yake iliyogharimu kodi ya Shilingi milioni kumi kwa mwezi, ambayo ni milioni 120,000,000 kwa mwaka na ameikalia kwa miaka 5, jumla ni milioni 600,000,000 na huu sio ufujaji bali ndio stahiki.

Baada ya kuuziana nyumba za serikali, wateuliwa wote wapya huwekwa hotelini zenye hadhi ya nyota 5 kama stahiki zao wakati wakisubiri nyumba za hadhi zao zipatikane.

Yote hayo ni tisa, kumi, kitu ambacho Salva hakukisema, ni ile outfit allowances yetu haiko pagged kwa percentage ya kipato kama zilivyo posho nyingine lukuki, yenyewe iko fixed and very unfortunately, haitoshi kununua suti 5 za Saville, hivyo hoja ya mkuu wetu kununuliwa Suti 5 za Saville bado imesimama, na kwa minajili ya kidplomasia , Ubalozi wa Marekani utaissue statement hivi karibuni kudai Wiki leaks wametunga na kumsingizia balozi wao, na Mwarabu pia atatuma Statement itakayofanyiwa press conference kukanusha kuwa hakuwahi kumpeleka mkuu wetu wa nchi kwenye shopping ya London wala kumlipia chumba cha Dola 1,000 kujipumzisha. Hii ni process ya 'demage controll', lakini facts zinabaki kuwa facts. Tena kama mimi ndio JK, na ni ukweli nina Saville suits, hata kama nilizinunua kwa fedha yangu au ya ikulu, kamwe stazivaa tena!.
 
Hivi kuna Ikulu yeyote ambayo haitoi huduma kama kuvalisha, kulisha, malazi, usafiri, ulinzi kwa rais wake???... Najiuliza tu, ili kupanua mjadala zaidi na kuufanya usionekane too personalised against Rais Kikwete...

Na hizo suti zinazosemekana alinunuliwa, alinunuliwa akiwa Waziri wa Mambo ya Nje, au akiwa Rais wa JMT? Maana naona kama kuna upotoshaji wa wazi, sijui ni kwa makusudi au kutofahamu.
 
Kwenye JF tunawajua wenye mawazo hasi na chanya.Sasa hapa naona tuache tuone....Mkapa aliwahi kushutumiwa na rushwa ya mil 900 na mzee mmoja. na kesi ikanguruma ukweli ukawa kweli.Sasa mwanzo walimwona babu kama taahira fulani..Sasa leo week leaks wamekuja na page ya suti na JK twaona kama wajinga..Hamjui waliona wapi hiyo movie jamaniiii..Msiamini sana masharobaroooo....ohoooo..PEOPLESSSS POWERRRR
 
Mkjj saa nyingine unabore na maandiko yako. Huwa unakosa vya kuandika au ndio chuki binafsi kwa Kikwete? Unanchekesha!
,
EFU EFU (FF), Mwanakijiji si ameuliza tuu, "Je Kikwete arudishe fedha za nguo anazonunuliwa na nchi yake "maskini'? atumie mshahara wake?".

Sasa kama unajibu, unajibu, kama huna unajinyamazia na kusoma majibu ya wenzio, hili la Chuki binafsi limetoka wapi?, wasiulizwe waliomzingizia kununuliuwa suti na kupangishiwa chumba kama wana chuki binafsi, sasa anaulizwa aliyeuliza kama mshahara wake utumike kununulia mavazi?

Hata hivyo nakushukuru kwa kuishia hapo hapo kwenye chuki binafsi, maana hukumalizia ni chuki binafsi dhidi ya nini, asante kwa hili.​
 
Hivi wakulima wa Tanzania wanapewa posho gani kama mastahili yao?
Mzee Mwanakijiji, stahili, ni vitu avipatavyo mtu kama haki yake kutokana majukumu yake, haki hii huendana na wajibu.

Mkulima nae anazo stahili zake, zikiwemo kulima anachotaka, kuanza kazi muda anaotaka, na hatoziwi kodi, japo pia anapewa wajibu wa kupangiwa bei mazao yake hata kama ni kwa bei ya hasara.
Ukubwa raha, udogo shida!
 
Mwanakijiji huna lolote!.Wala huumwi na fedha za wananchi zinazotumika kiholela.Kinachokusumbua ni ujinga na kidomodomo.
Kwanza ungemtaka Kikwete na Serikali yake warejeshe pesa zote ilizoyapatia makanisa kwa kuwanyima waislamu ili zitumike kwa maendeleo ya wananchi wote


Ila we mtu wewe...hivi umekumbuka kupiga mswaki leo? Mwenzio Gadafi ndio hivyo tena...
 
Kwa utaratibu wa serikali,


Officer yeyote anayesafiri nje ya nchi anastahili kulipwa karibia dola 300 kila baada ya miaka 3 kwa ajili ya kununulia nguo (out fit).

Kumbe mshua anapelekwa tu shopping na kuchagua kama mtoto wa kindergarten (zamani tuliita vidudu)???

Haya ni mambo ya hovyo sana na ndiyo maana watu wanakesha kwa waganga kutafuta ukubwa!!
 
Mzee Mwanakijiji, stahili, ni vitu avipatavyo mtu kama haki yake kutokana majukumu yake, haki hii huendana na wajibu.

Mkulima nae anazo stahili zake, zikiwemo kulima anachotaka, kuanza kazi muda anaotaka, na hatoziwi kodi, japo pia anapewa wajibu wa kupangiwa bei mazao yake hata kama ni kwa bei ya hasara.
Ukubwa raha, udogo shida!

Hatozwi kodi?
 
Mkuu Pasco nimekukubali. ni kweli rais anasafiri na msafara mkubwa ajabu. jamaa hasa wa protocol pale foreign wakirudi ni pilika pilika tu za kufanya retirements fedha walizopewa kugharamia kule lakini wakakuta ubalozi ama mwenyeji kagharamia kila kitu so wanajiingizia mifukoni.
 
Watumishi woote wana mahitaji kama JK,so yeye pamoja na vingozi woote serikalini plus wabunge wana uspesho gani wa kufanyiwa vitu kama vile ni walemavu?
Mbona kima cha chini na wafanyakazi wengine tunatumia mishahara yetu kujihudumia na kuhudumia familia zetu kwa KCC?Mbona hatupewi mgawo wa nguo hata uniform ni za kubahatisha kama zipo.

Mwanakijiji yupo sawa sheria za kipuuzi na za kikoloni za kuona kuna watu ni bora kuliko wengine ndio zinpelekea yote haya.


Mwanakijiji
Sipingani na mawazo yake na naheshimu uhuru wa kutoa mawazo. Lakini natofautiana kidogo sana nawe kwasababu sidhani kama kazi ya mshahara ni kununua nguo pekee. JK ana watoto ambao inabidi wasome, sidhani kama Ikulu inawasomesha ama inawalipia ada, anatakiwa kutoa pesa yake mfukoni kulipia ada ya watoto wake. Atapata wapi pesa kama sio mshahara wake na posho zake?
Pia JK ana ndugu ambao kwa namna moja ama nyingine wanamtegemea yeye, Mama, babu, bibi na hata wakwe kama tujuavyo extended family zetu waafrika. Fedha ya kuwasaidia haitoki kwenye kasma tu ya Ikulu, ni ile ya mshahara wake.
Hiyo ni mifano tu michache lakini naamini yapo mambo mengi ambayo anatakiwa kuyafanya kwa fedha ya mfukoni mwake na sio kufanyiwa na IKULU> Kama hoja yako ya kwamba kwakuwa anapata mshahara basi hapaswi kufanyiwa mambo mengine bali atumie mshahara wake, nauliza kitu kimoja kwamba vipi kuhusu wakurugenzi na makatibu waku na hata watendaji wengine ambao wanapewa fedha ya mafuta, simu, umeme majumbani na bado wanapewa mishahara mikubwa? Mbona hao hatuwaulizi na hatusemi wasipewe mshahara?
Narudia sipingani na hoja yako na naheshimu mawazo yako, na huu ni mtazamo wangu tu.
 
Mzee Mwanakijiji

Which is better kuzilipia au kuzichoma moto hadharani? Au kumfukuza na uwekezaji wake wote Tanzania. Lakini kwa FP hiyo ni ndoto.

NB: FP = Fisadi papa.
 
Back
Top Bottom