Je, katika suala la Mikataba na Tenda mbalimbali, tukivaa viatu vya Hayati Magufuli vitatutosha?

Nehemia Kilave

JF-Expert Member
Jan 9, 2022
449
1,009
Kwanza kabisa tumsikilize Tundu lissu kuhusu Mali za Tanzania ..

Pili, binafsi sina shaka na alichokiongea Tundu lissu kuhusu JPM .

Mwisho, kama wewe ungekuwa ndio Hayati JPM umeingia madarakani na kukuta kuna Tenda au Mikataba ya hovyo inaumiza taifa kama anavyoiita Tundu Lissu ,ungefanyaje ?

Na ukishapata jibu ,jiuliza tuendelee kumlaumu au tumpongeze kwa ujasiri wake japo tumepata hasara .​
 
Kwanza kabisa tumsikilize Tundu lissu kuhusu Mali za Tanzania ..
View attachment 2692191
Pili .. binafsi sina shaka na alichokiongea Tundu lissu kuhusu JPM .

Mwisho...kama wewe ungekuwa ndio Hayati JPM umeingia madarakani na kukuta kuna Tenda au Mikataba ya hovyo inaumiza taifa kama anavyoiita Tundu Lissu ,ungefanyaje ?

Na ukishapata jibu ,jiuliza tuendelee kumlaumu au tumpongeze kwa ujasiri wake japo tumepata hasara .​
Upuuzi
 
Naona baadhi wakiona jina Magufuli huwa bongo zao zinaganda, fikra zinasimama, matokeo yake wanakuja na majibu waliyokariri miaka karibia mitatu iliyopita, hawataki kujiuliza jambo gani lipo mezani linajadiliwa kumhusu Magufuli, kisha wapime kama lina ukweli au hapana.

Suala la kuvaa viatu vya JPM kwenye kulinda rasilimali zetu halihitaji mjadala, hilo ni la lazima ili kizazi chetu, na vile vijavyo vije kufaidi utajiri tuliopewa bure na muumba.

Hata kama hatuwezi kuziendeleza sisi, maneno ya ajabu kabisa, aliyasema Nyerere karibia miaka thelathini iliyopita, bado mpaka leo tunayarudia, basi tukiachie kizazi kijacho kije kuzitumia kwa ufanisi.
 
Kwanza kabisa tumsikilize Tundu lissu kuhusu Mali za Tanzania ..
View attachment 2692191
Pili .. binafsi sina shaka na alichokiongea Tundu lissu kuhusu JPM...​

Ukivunja mkataba utashtakiwa na uhakika wa kushindwa ni 100%.

Namna ya kwanza ya kujinasua ni kujadiliana na ulioingia nao mkataba ili kurekebisha.

Namna ya pili ni kusubiri mpaka mkataba uishe na baada ya hapo kukataa kuongeza, au kuuongeza kwa namna isiyokutia hasara.

NB:
Hatua za kuvunja mikataba zimepelekea kushindwa kesi nyingi na kuamriwa kulipa mabilioni ya fedha.
 
Naona baadhi wakiona jina Magufuli huwa bongo zao zinaganda, fikra zinasimama, matokeo yake wanakuja na majibu waliyokariri miaka karibia mitatu iliyopita, hawataki kujiuliza jambo gani lipo mezani linajadiliwa kumhusu Magufuli, kisha wapime kama lina ukweli au hapana...
Kwa mchango huu mkuu, unapaswa kuwa ngazi za juu kabisa za kiuongozi katika nchi yangu hii Tanzania

Nitakuombea kwa anayegawa vipawa aridhie ombi langu!
 
..ukivunja mkataba utashtakiwa na uhakika wa kushindwa ni 100%.

..namna ya kwanza ya kujinasua ni kujadiliana na ulioingia nao mkataba ili kurekebisha...
Mikataba ya kinyonyaji iliyoingiwa na waliokuwa wakidhani ni wasomi kwa nyakati hizo, kumbe ni vilaza wakubwa, mikataba ya 2% na 98% anachukua mwekezaji ni bora kuvunjwa ili tuanze upya
 
Kwanza kabisa tumsikilize Tundu lissu kuhusu Mali za Tanzania ..
View attachment 2692191
Pili .. binafsi sina shaka na alichokiongea Tundu lissu kuhusu JPM...​
Kwani wakati nchi inaingia hiyo mikataba ya hovyo yeye si alikuwa kwenye baraza la mawaziri? Unasema alipoingia madarakani kana kwamba alitoka nje ya nchi? Ni lini aliwahi kujitokeza hadharani kuonyesha kuwa nchi inaingia mikataba mibovu?
 
Kuwa na uchungu bila kutumia akili ni ujinga mtupu. Unavunja mkataba kibabe wakati unajua ni suala la muda tu utakuja kulipishwa mabilioni? Nchi inaingozwa kwa mashauriano sio ubabe wa mtu mmoja.

Viatu vya Magu vinavalika. Mama Samia kavivaa vizuri na anafanya mambo makubwa kwa njia za kidiplomasia. Awamu ya 5 ilitudanganya tunaidai Barrick trilioni 495.

Jiulize kama uongozi wa juu kabisa unaweza kuwadanganya wananchi huo uongozi ulikuwa wa aina gani?
 
Kuwa na uchungu bila kutumia akili ni ujinga mtupu. Unavunja mkataba kibabe wakati unajua ni suala la muda tu utakuja kulipishwa mabilioni? Nchi inaingozwa kwa mashauriano sio ubabe wa mtu mmoja. Viatu vya Magu vinavalika. Mama Samia kavivaa vizuri na anafanya mambo makubwa kwa njia za kidiplomasia. Awamu ya 5 ilitudanganya tunaidai Barrick trilioni 495. Jiulize kama uongozi wa juu kabisa unaweza kuwadanganya wananchi huo uongozi ulikuwa wa aina gani?
Ni upumbavu kuendelea kulea mimba yenye upepo ndani hakuna mtoto!

Ni aheri kufanya operation na kuanza upya!
 
Back
Top Bottom